Harald Dad
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 353
- 263
Watanzania wenzangu naombeni ushauri wenu, hapa nilipo nimevurugwa vibaya sana kwa sasa kila ninalojaribu kufanya kwangu naliona kama halina tija tena kwangu. Hali hii imenijia baada ya kugundua kuwa serikali ya Tz ilinilaghai na kisha kunitapeli zaidi ya sh.milioni 10. Mara nyingi nawaza na kujiuliza hivi hawa akina Karl Peter na sisi akina Chief Mangungo wa Msovero bado tupo dunia ya sasa? Kwa nini mikataba hewa kama ile ile ya kikoloni bado ipo? Au wakoloni wamekuja tena na mambo yao yale yale? Nahisi wakoloni ni wale wale ila tu wamebadilika tu rangi walikuja weupe wa sasa ni weusi. Wanatuaminisha karatasi nyeupe tuiite nyeusi na nyeusi tuiite nyeupe. May mosi nilikuwa hapa Mbeya jambo la kushangaza mc wao Mavunde kabla ya mkuu kufika alisisitiza sana akija tu tujitahidi kuonyesha nyuso za furaha na tumshangilie kwa furaha. Nilijiuliza sana ya nn kujifanyisha kuwa nina furaha usoni wakati moyoni ninalia? Kwa nn niishangilie serikali hii wakati wao mimi wamenitapeli. Serikali iliyochukua zaidi ya 10 milioni huku mm wakinitunuku karatasi? Wamechukua hela yangu na mm wamenipa karatasi ety wenyewe wakaliita degree huu ni utapeli kama ilivyovyo utapali mwingine. Mungu anawaona wakuu.