dosama
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 912
- 957
Benki ya dunia, ikisaidiwa na serikali kuu ya Ujerumani imeachilia mbali mwongozo wake wa hifadhi ya wakaazi asili nchini Tanzania. Benki ya dunia imeidhinisha mkopo wenye thamani ya dola bilioni moja, kugharimia mradi mkubwa wa shughuli za kilimo nchini Tanzania.
Serikali mjini Dar es salaam inataka kuutumia mradi huo kuyashawishi makampuni mfano wa lile la Nestlé na Bayer yawekeze katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Uchunguzi umebainisha kwamba Ujerumani imeishawishi Benki ya Dunia iachane na desturi zake za kutanguliza mbele hifadhi ya wakaazi asilia. Wanaharakati wa haki za binadamu wanalalamika wakisema hata kabla ya mradi huo wa kilimo kuanza, maelfu ya wakaazi asilia wamelazimika kuzipa kisogo maskani zao. ..