Philosodilia
Senior Member
- Jan 25, 2018
- 105
- 61
Ni jambo jema kufanya hivyo...
Wakati wa mapumziko km lunch break.Sawa tumekuelewa,ila huo wakati wa break kazini ni saa ngapi mkuu ? au ulikuwa unamaanisha ni baada ya muda wa kazi..?
Sawa kabisa kutumia internet ya kazini kwa matumizi binafsi ni kosa na ni vibaya.Watu ni wagumu kuelewa jamani,iyo ishu inahusu wale wanaotumia rasilimali gvt ikiwemo internet kwa matumizi binafsi wakati serikali inalipia.Ukihitaji mitandao ya kijamii+kudownload movies tumia rasilimali zako binafsi.mfano mzuri wakati tuko college kuna net ya bure ambayo wanafunzi tunaitumia vibaya ikiwemo kudownload movies,ngono kinyume na utaratibu.
it could have been done sooner…I wondered why our government tolerated this for too long! As usual, my responsible 5th government regime almost always spot on, took the correct measure! bravo!Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali wakati wa kazi, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.
Inaonekana serikali haijatambua 80% ya biashara za kisasa zinafanyikia mtandaoni,huko insta na facebook watu wanamobile electronic shops.
Wameshazoea kudraw pesa za mshahara kila mwisho wa mwezi wamesahau kuna vingine vinavyowapa wenzao kula kama biashara kupitia mitandao.
Wanadhani mitandao ni sehemu ya kutafutia mademu na kujionyesha La hasha hizi ni ofisi kama zilivyo zakwao.
Kama ukiweza kumanage biashara kiganjani kwako wewe ni bora kuliko mwenye fremu kibao anaeka kusubiri wanaopita.
Mimi nadhani ni muda wa serikali kutambua mitandao ya kijamii ni ofisi za watu.
Kama wanataka kufungia wadisconnect network katika majengo yao ya serikali tu.
View attachment 849176View attachment 849175View attachment 849174View attachment 849173
======
Serikali ya Tanzania imezuia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma wakati wa kazi kwa madai yanaathiri kasi ya mtandao wa intaneti ya Serikali.
Pia, imedai watumishi wengi wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kutekeleza majukumu yao.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro kwa taasisi zote za umma, imeonya juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ya Serikali na kwamba, hatua hiyo imelenga kudhibiti matumizi ya mitandao.
“Kasi ya mtandao wa Serikali inapungua kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii hususan inayopakua video, mfano “YouTube” na hivyo kusababisha watumishi wengine wanaotumia mtandao wa intaneti wa Serikali katika kutekeleza majukumu yao kuathirika,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Aidha, taarifa hiyo inaeleza juu ya upakuaji wa nyaraka zenye hatimiliki bila idhini ya wamiliki kwa kutumia Intaneti ya Serikali kinyume na utaratibu.
“Mitandao ya kijamii haitapatikana kwenye intaneti ya Serikali wakati wa muda wa kazi kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri,” inaeleza taarifa hiyo.
Hata hivyo, Menejimenti ya Utumishi imezitaka taasisi zenye mahitaji maalumu ya matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa saa za kazi, kuwasilisha maombi yao kwa katibu mkuu wa utumishi yakiambatana na sababu za maombi hayo.
“Watumishi wa umma hawataweza kupakua nyaraka, picha na video zenye hatimiliki kwenye intaneti ya Serikali bila idhini ya wamiliki.”
Kwa mara kadhaa, Serikali imekuwa ikitoa miongozo ya matumizi ya Tehama kwa taasisi za Serikali ikiwamo kukataza matumizi ya mitandao kupitia intaneti ya Serikali saa za kazi.
Sent using Jamii Forums mobile app
wenye akili kama hizi ni wachache sana mijitu inajua kukosoa tuuu haiangalii hata kuelewa kilichoongelewa.Watu ni wagumu kuelewa jamani,iyo ishu inahusu wale wanaotumia rasilimali gvt ikiwemo internet kwa matumizi binafsi wakati serikali inalipia.Ukihitaji mitandao ya kijamii+kudownload movies tumia rasilimali zako binafsi.mfano mzuri wakati tuko college kuna net ya bure ambayo wanafunzi tunaitumia vibaya ikiwemo kudownload movies,ngono kinyume na utaratibu.
Hii bado haitamzuia mfanyakazi wa serikali kutumia muda wake kama inavyopaswa, kwani anaweza kununua bando kwa gharama zake binafsi. Kubwa tu waseme wanapunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali... Sababu nyingine sizielewi japo najaribu kuzielewaBora unakuta mtu customer officer anaacha kuhudumia wateja yuko busy JF au kwenye ma blogs
Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali wakati wa kazi, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.