Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali

Sema tatizo ni kwamba kwa hali ya nchi yetu ilivyo hilo agizo halitawezekana kwa sababu ofisi nyingi hazina vifaa vya kuwezesha tamko hilli kutekelezeka, unakuta ofisi haina routers zenye uwezo wa kukubali access control list policy, kinachoenda kutokea ni kuwalaumu wataalamu wa ICT watakaokuwa maofisini....
 
Sa 1 asubh mpaka saa 9 alasiri.....vip wale wa overtime????
Ukiamua kukaa mpaka saa 12 jionin je?
 
Kila kitu ni kwa mawasiliano ya internet siku hizi. hata serikalini kila kitu ni kwa internet. Kweli awamu hii hadi ipite tutaona maajabu mengi.
 
Wap...uzi wasije wakakaa waderive baadae sababu ya kufungia mitabdao ya kijamii hadi kwenye simu zote kama walivyofanya .madikteta sehemu zingine maana mnazoeshwa taratibu hilo swala ila nyie na uelewa wenu mnaona wataishia hapo tu, wakati yalishawahi kutamkwa kinywani mwake mwenyewe... nyie si wepesi wa kisahau mtawezaje kujua kuwa anatekeleza maneno yake sasa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali iandae budget tu ya kutosha ya kuinstall filters za hiyo mitandao ya kijamii!

1. Najua watakuwa wanalenga Facebook na JF zaidi, lakini kuna websites kibaooo duniani, zikiwemo za habari, gossip, michezo, siasa, celebrities watu bado wataingia kwenye site hizo

2. Watu watajifunza jinsi ya kutumia proxies na free VPN online zitakazoweza kubypass hizo filters na kuaccess hizo websites

3. Mitandao mingi ya kijamii inapatikana pia katika simu, ukiziba kwenye computer, watu wanaendelea kumkoma nyani giladi kama kawaida kupitia simu zao!

4. Ni gharama kwa serikali kuinstall firewalls kwenye kila ofisi ya serikali nchini, watawalaumu bure tu masystem administrators
.

5. Hili agizo lingewezekana kama Tanzania ina uchumi wa kati wenye kuiwezesha kununua vifaa vya kumonitor hii kitu, lakini kwa nchi hii masikini na population ya watu iliyokwishazoea mtandao, Hili ni tamko tu kama matamko mengine

Mkuu, Malaika yule hajali hizo gharama nakuambia kama anataka kufungia atalazimisha afungie tu. Huu ndio uongozi tulionao, kwani huoni gharama za marudio ya uchaguzi zimefika Billioni ngapi kwa sasa ilihali wakati huo huo kuna maeneo mengi ya nchi hii yanahitaji hizo hela kwa ajili ya kujenga visima vya maji, barabara mbovu,zahanati nk.
 
Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali wakati wa kazi, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.

Inaonekana serikali haijatambua 80% ya biashara za kisasa zinafanyikia mtandaoni,huko insta na facebook watu wanamobile electronic shops.

Wameshazoea kudraw pesa za mshahara kila mwisho wa mwezi wamesahau kuna vingine vinavyowapa wenzao kula kama biashara kupitia mitandao.

Wanadhani mitandao ni sehemu ya kutafutia mademu na kujionyesha La hasha hizi ni ofisi kama zilivyo zakwao.

Kama ukiweza kumanage biashara kiganjani kwako wewe ni bora kuliko mwenye fremu kibao anaeka kusubiri wanaopita.

Mimi nadhani ni muda wa serikali kutambua mitandao ya kijamii ni ofisi za watu.

Kama wanataka kufungia wadisconnect network katika majengo yao ya serikali tu.
View attachment 849176View attachment 849175View attachment 849174View attachment 849173

======

Serikali ya Tanzania imezuia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma wakati wa kazi kwa madai yanaathiri kasi ya mtandao wa intaneti ya Serikali.

Pia, imedai watumishi wengi wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kutekeleza majukumu yao.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro kwa taasisi zote za umma, imeonya juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ya Serikali na kwamba, hatua hiyo imelenga kudhibiti matumizi ya mitandao.

“Kasi ya mtandao wa Serikali inapungua kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii hususan inayopakua video, mfano “YouTube” na hivyo kusababisha watumishi wengine wanaotumia mtandao wa intaneti wa Serikali katika kutekeleza majukumu yao kuathirika,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Aidha, taarifa hiyo inaeleza juu ya upakuaji wa nyaraka zenye hatimiliki bila idhini ya wamiliki kwa kutumia Intaneti ya Serikali kinyume na utaratibu.

“Mitandao ya kijamii haitapatikana kwenye intaneti ya Serikali wakati wa muda wa kazi kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri,” inaeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, Menejimenti ya Utumishi imezitaka taasisi zenye mahitaji maalumu ya matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa saa za kazi, kuwasilisha maombi yao kwa katibu mkuu wa utumishi yakiambatana na sababu za maombi hayo.

“Watumishi wa umma hawataweza kupakua nyaraka, picha na video zenye hatimiliki kwenye intaneti ya Serikali bila idhini ya wamiliki.”

Kwa mara kadhaa, Serikali imekuwa ikitoa miongozo ya matumizi ya Tehama kwa taasisi za Serikali ikiwamo kukataza matumizi ya mitandao kupitia intaneti ya Serikali saa za kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
fungueni tu ili sie wauza bando tunafaike wateja nadhani sasa mtaongezeka tena kwa hasira sana
Sky Eclat
 
fungueni tu ili sie wauza bando tunafaike wateja nadhani sasa mtaongezeka tena kwa hasira sana
Sky Eclat
Mkuu lakini ukiangalia ni kama strategy ya kulimit information. Wale waliokuwa wanapata habari za michepuko ya jiwe kupitia kwa Mange c/o JF itakuwaje?
 
Mkuu lakini ukiangalia ni kama strategy ya kulimit information. Wale waliokuwa wanapata habari za michepuko ya jiwe kupitia kwa Mange c/o JF itakuwaje?
Kwan si unasimu yako tatizo ni nn hapo na Hata HIZO Habar za MANGI sijui nan ukirud Toka Kazin hutazipata nyie Ndio mnaotumia muda WA kazi kuchat chati
 
Si serikali tu, bali hata baadhi ya taasisi binafsi zinadhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii muda wa kazi. Hata hizo downloads na uploads zimezuiwa.
 
Back
Top Bottom