Serikali ya Tanzania huwanyonya Wakulima wa Tanzania?

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Ukisikiliza kauli mbiu za Kilimo Kwanza, unasikia wakulima wakubwa wa mashirika na kutoka nje ya nchi wakipewa kipaumbele. Wale wadogo waliolibeba Taifa kwa maiak yote 49 ya Uhuru, wanaambiwa watapewa plau waanze kulima kwa kutumia plau za ng'ombe. Pembejeo na Ruzuku kwao ni finyu na ubora wa maisha yao si mzuri.

Zaidi serikali inashinikiza kuendelea kwake kuwa dalali kwa kupanga bei za mazao nahata kuuza mazao nje ya nchi.

Je mkulima wa Tanzania atapataje maendeleo na kuondokana na umasikini ikiwa Serikali inatumia mbinu kuhakikisha inamkamua mkulima kila kitu?

Nimekutana na takwimu moja leo na ni kauli ya Katibu Mkuu wa Kilimo Muya ambao amesema kuwa Tumbaku huliingizia Taifa dola Millioni 217 na kuwa kuna wakulima 80,000 wa tumbaku Tanzania.

Swali langu ni kipato hicho alichokisema ni cha mwaka jana, ni kiwango gani na asilimia gani ilikwenda kwa wakulima?

Je wangeuza wenyewe na kupata hizo pesa na kulipa kodi kwa Serikali je maisha yao na jamii jirani yangekuwa wapi?

Mchungaji hupenda kukokota mahesabu rahisi. Ukigawanya hilo pato kwa hawa wakulima, kila mkulima angepata dola 2712.

Je hiki ni kiwango ambacho mkulima kapata kwa mauzo yake ya tumbaku?

Je wale wa kahawa, chai, katani, korosho, ufuta, karafuu, alizeti, pamba, mchele, mahindi na mazao mengine yawe ni ya biashara au chakula, pato lao ni kiasi gani?

Je mkulima huyu wa tumbaku kama angeipata hiyo dola 2712 na tuseme kodi kwa Serikali ni asilimia 30, hivyo kulipa kodi ya dola 813, je tungeona anapiga hatua mbele kimaisha na kujiimatisha tofauti na Serikali kushikilia asilimia 70 ya pato?

Je bei aliyotupa mheshimiwa Katibu ni pato zima kwa Taifa au ni mgawanyo kwa wakulima huku pato lingine likiwa limekwenda Serikalini moja kwa moja?

Tumapoendelea na mfumo huu wa Serikali kuwa mdhibiti wa uzalishaji, dalali na muuzaji wa bidhaa na mazao na huku tunadai tuko kwenye mfumo wa soko huria, hatuoni kuwa tunaendelea kumnyonya Mtanzania kwa Serikali kujiingiza katika mchakato mzima na si ikae kando ikitegesha mikono kukusanya kodi?

Je hatuoni kuwa kujishughulisha huku kwa Serikali si kwamba kunawanyima na kuwapunguzia Watanzania mapato yao bali ni kuwaongezea mzigo kutokana na Serikali kuwa kubwa na kuunda idara ya kufanya kila kitu na hatimaye ni Watanzania kutumika kuiendesha Serikali isiyo fanisi yenye kubugia fedha nyingi kujiendeshana hivyo kupunguza kasi ya ujenzi wa maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi?

Just wondering!
 
Ukifika mkoa wa kagera hasa wilaya za Karagwe, Misenyi, Bukoba vijijini na Muleba utaona namna serikali inavyotumia nguvu na raslimali nyingi kudhibiti wakulima wasipelee kahawa yao kwenye soko lenye bei nzuri la Uganda.
Barriers kila mahali, polisi na hata mgambo, kisa Kahawa - mkulima asipate bei nzuri
Kibaya kingine ni kwamba huu umekuwa kama mradi wa watu kwani kuvusha gari moja ni karibu tshs 100,000.
Bei ya uganda ni kubwa kiasi kwamba lazima kahawa ivuke. Kwa mfano, wakati mwaka jana bei ya TZ ilikuwa kati ya shs 500 - 750 kwa kilo, bei ya uganda ilikuwa 1,400. Tofauti ya shs 650 kwa kilo ni hela nyingi kwani gari la tani 10 ni swa na Tshs 6,500,000/= Hizi ni hela anazonyonywa mkulima na serikali yake aliyoiweka mwenyewe madarakani!
 
Back
Top Bottom