Serikali ya Tanzania haina dini

Serikali ya Tanzania haina dini

SERIKALI YA TANZANIA HAINA DINI
Katika katiba ya Tanzania inasema Tanzania haina dini ila watu wake wana dini nafikiri kipengele hiki kina utata;
1. Hakuna uhuru wa kuchinja
2. Kwanini kuna ubalozi wa VATICAN wakati Tanzania haina dini
3.kwanini kuna MOU kwa kundi moja na kuacha kundi jingine
4. kwanini takwimu za kisensa zisitambue wananchi wake pamoja na dini zao
Tunaomba katiba ibadilishwe kwani ina mapungufu
Hili ndilo tatizo la serikali hii. Kama tu ingejitokeza na kuelezea mambo haya, malalamiko kwa Waislamu yangekwisha. Hakuna tofauti kati ya kuwa na ubalozi wa Saudi Arabia auj Iran na Vatican. Ingesemwa na Raisi kwa mfano ingeeleweka na kukubalika zaidi kuliko nikisema mimi. MOU imelalamikiwa sana lakini wala hawajajitokeza kuielezea hivyo kuwaacha waislamu katika mashaka makubwa. Masuala ya kuchinja kama yangeshughulikiwa na kuelezwa kwa mtazamo wa Katiba, haya yangeisha. Nafikiri serikali ihusike kutoa msimamo ili kuwaelimisha waislamu na wengine wasioelewa mambo hayo.
 
KAMANDA ISA MATTER OF TIME JUST RELAX

4030902_orig.jpg






4363460_orig.jpg




8167085_orig.jpg




8316457_orig.jpg



Sheikh PONDA akizungumza na Wakili Wake


9534231_orig.jpg



Watu Waliofika kusikiliza kesi zao Wakipekuliwa na Walinzi

527391_orig.jpg



8760817_orig.jpg



3764028_orig.jpg



1201477_orig.jpg



3008529_orig.jpg



737260_orig.jpg



POLISI Hatari Wa Nchi

4903072_orig.jpg



Inaonekana Nimeonekana BONGO Muda Mrefu - Sikujua MAPOLISI wetu wana VIFAA HIVYO Ndio Maana ni Wagomvi

3955375_orig.jpg



2797987_orig.jpg



819344_orig.jpg



1686075_orig.jpg



1653818_orig.jpg







 
SERIKALI YA TANZANIA HAINA DINI
Katika katiba ya Tanzania inasema Tanzania haina dini ila watu wake wana dini nafikiri kipengele hiki kina utata;
1. Hakuna uhuru wa kuchinja
2. Kwanini kuna ubalozi wa VATICAN wakati Tanzania haina dini
3.kwanini kuna MOU kwa kundi moja na kuacha kundi jingine
4. kwanini takwimu za kisensa zisitambue wananchi wake pamoja na dini zao
Tunaomba katiba ibadilishwe kwani ina mapungufu

Inaelekea umewakodishia watu AKILI ZAKO
 
Ngoja kuna moja linaenjoy ila muda si mrefu litalia sana just wait
 
Hili ndilo tatizo la serikali hii. Kama tu ingejitokeza na kuelezea mambo haya, malalamiko kwa Waislamu yangekwisha. Hakuna tofauti kati ya kuwa na ubalozi wa Saudi Arabia auj Iran na Vatican. Ingesemwa na Raisi kwa mfano ingeeleweka na kukubalika zaidi kuliko nikisema mimi. MOU imelalamikiwa sana lakini wala hawajajitokeza kuielezea hivyo kuwaacha waislamu katika mashaka makubwa. Masuala ya kuchinja kama yangeshughulikiwa na kuelezwa kwa mtazamo wa Katiba, haya yangeisha. Nafikiri serikali ihusike kutoa msimamo ili kuwaelimisha waislamu na wengine wasioelewa mambo hayo.

Hayo ni maoni yako na unahaki kabisa ya kuamini hivyo! lakini usijidanganye kuwa Waislamu wataridhika pindi Serikali ikija kufafanua hayo uliyoyaeleza! Kamwe Serikali haiwezi kukanusha hayo sababu Waislamu wanaushahidi wa Kisayansi unaothibitisha madai yao ndio maana Serikali haina uso wa kukanusha madai mazito na ya msingi ya Waislamu? labda iwe ni Serikali ya kiwendawazimu ndio itakuwa na ubavu wa kukanusha madai ya Waislamu! ni zaidi ya nusu karne sasa Serikali inaimba majukwaani kuwa haina dini huku ikilipa Kanisa upendeleo maalum dhidi ya dini ya Kiislamu! ushahidi mdogo, ktk miaka ya 70 Rais wa Tz alimteua Padre asimamie kitengo cha siasa ktk halmashauri kuu ya TANU na kumhakikishia mwakilishi wa Papa kuwa amemchagua Padre huyo kwasababu ya uchamungu wake na yeye Mwalimu atahakikisha Kanisa linalindwa vizuri TZ kuliko mahala pengine popote!

Kwanini na Shehe hakuchaguliwa? huo kama sio udini ni nini?
Waislamu msimamo wao ni Serikali isimamie haki na uadilifu na kamwe Waislamu hawataki upendeleo bali haki sawa kwa wote! dini inayopenda kubebwa na kubembelezwa inajulikana!
 
SERIKALI YA TANZANIA HAINA DINI
Katika katiba ya Tanzania inasema Tanzania haina dini ila watu wake wana dini nafikiri kipengele hiki kina utata;
1. Hakuna uhuru wa kuchinja
2. Kwanini kuna ubalozi wa VATICAN wakati Tanzania haina dini
3.kwanini kuna MOU kwa kundi moja na kuacha kundi jingine
4. kwanini takwimu za kisensa zisitambue wananchi wake pamoja na dini zao
Tunaomba katiba ibadilishwe kwani ina mapungufu
Nitakujubi swali moja baada ya jingine.

  1. Hakuna Uhuru wa Kuchinja, haki ya kuchinja wamepewa waislam peke yao na ndio wanaoamini kuwa ni haki yao, wakristo hawana uhuru wa kuchinja, ila waislam wana uhuru wa kuchinja. nyama zote tz lazima zichinjwe na muislam, sio mkristo au mtu wa dini nyingine.
  2. kwanini kuna ubalozi wa vatican wakati tanzania haina dini? kwasababu vatican ni nchi inayojitegemea kabisa, pia, usichanganye kuwa, vatican inawakilisha wakristo, hapana, inawakilisha the Holy see, nchi ile ya vatican pale roma. na zaidi ya yote, haiiwakilishi dini ya kikristo, na hata kam aingeiwakilisha dini ya kikristo sio kwa wakristo wote, wangekuwa wakatoliki tu, kwasababu sio wakristo wote wanaamini ukatiliki...hivyo futa akilini kwamba vatican inawakilisha udini wa kikristo, hapana, inawakilisha nchi ya vatican. kama hujui ile ni nchi, rudi darasani kasome vitabu, msikimbie shule.
  3. Kuna Mou kwa wakristo, kwasababu waislam hawana uwezo wa kuchanga sadaka ili wajenge hospitali na shule. wakristo walishafanya hivyo na wakapata pa kuongelea. hata hivyo, hospitali na shule hizo wamejaa waislam, hazibagui, wanatibiwa waislam wengi mno, pia wanasoma waislam wengi mno. shule za kiislam zinakimbiwa na waislam wenyewe, hivyo mou ni mkombozi wa tz nzima bila kujali dini. au unataka uugue ili uone kama utatibiwa hospitali zilizoanzishwa na sadaka za kikristo nini?
  4. kutambua wananchi wao pamoja na dini katika sensa?..hahaha, serikali inawaogopa watu kama wewe, watu ambao tayari walishaweka vichwani mwao kuwa waislam ni wengi kuliko wakristo. siku mkija kusikia wakristo ni wengi kuliko waislam mtaandamana kwasababu matango mwitu mlliyolishwa yamewakaa vichwani si rahisi kutoka. cha kuelewa ni kwamba, nafasi ya waislam na wakristo kuzidiana hapa tz ni ndogo sana, inawezekana tukawa sawasawa tu.zaidi ya yote, sisi hapa tz tunataka amani na mshikamano, hatutaki tuanze kutambuana kimakundi ya dini kama unavyotaka, haisaidii.
  5. kuishi kwa makundi ya kiislam na kikristo yakiwa yanatambulika kisensa, ni hasara kuuliko kama tungeishi hivihivhi. hivyo, kwa hivi tunavyoishi sasa, ni sahihi kabisa.
halafu, mbona unanukia kiudiniudini, au wewe ni mmoja wapo wa wale waliolipua lile bomu arusha? hata kama serikali haitawakamata, Mungu atawahukumu. kwasababu Mungu aliyeumba Mbingu na nchi hajaagiza watu wawauwe wenzao kwa namna hiyo, tena wakiwa wanasali kanisani. shetani ndio anaagiza hivyo. usijidanganye kuwa hapo ulipo unaabudu mungu, unaabudu shetani aliyezishika akili zako ukifanya mchezo hautakuja kufumbuka mamcho hayo uliyopigwa upofu milele. badilika.

KAMA UNATAKA KATIBA IBADILIKE, ELEZA IBADILIKE KIVIPI, HALAFU NENDA PALE OHIO KWA AKINA WARIOBA KAWASILISHE MAWAZO YAKO, watayapokea na kuyatilia mkazo. usilielile.
 
[h=3]Kuna jambo kubwa wakatoliki hawajasema..[/h]



*Wapo wangapi Baraza la Mitihani?*Kwa nini wanampa Nyerere ‘utakatifu'?*Kilio cha Wazanzibari kisipuuzwe

Na Omar Msangi
Mwaka 1965 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu-Tanzania Episcopal Conference (TEC), Father Robinson alitoa taarifa akikiri kwamba shule za Kanisa Katoliki zilikuwa zikitegemea fedha kutoka serikalini kwa asilimia 100. Kwa sababu hiyo akasema, kama serikali itasitisha utaratibu wake wa kuchota fedha kutoka Hazina ya kodi za ‘Watanganyika' na kuwapa Wakatoliki, basi itabidi shule hizo zifungwe.
Kabla ya hapo tunaambiwa kuwa serikali ilikuwa ikizipa shule za Kanisa ruzuku iliyofikia asilimia 66% ya bajeti ya shule hizo. Ruzuku hiyo ikitoka katika Hazina ya taifa inayochangiwa kwa kodi za Waislamu, Wakristo na watu wa dini nyingine.
Hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa. Huo ndio utaratibu wa mambo ulivyo katika nchi hii tunayotamba kwamba haina ubaguzi wala upendeleo wa kidini wala wa kikabila.
Hivi sasa Kanisa Katoliki lipo katika shamrashamra likitamba kuwa katika zile shule kumi bora katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni, basi saba ni za Katoliki.
"Katika kumi bora kidato cha nne, Wakatoliki wazoa 7", limeandika gazeti la Tumaini Letu linalotolewa na Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
"Katika idadi ya shule zilizoshika nafasi ya kumi bora kitaifa…shule saba zilizoshika nafasi hiyo zinaendeshwa na kumilikiwa na Kanisa Katoliki."
Limefafanua gazeti hilo namba 00401 la Ijumaa Februari 10-16, 2012.
Tumaini Letu likazitaja shule hizo kuwa ni St. Francis iliyoshika nafasi ya kwanza, St. Joseph Millenium nafasi ya tatu, wakati shule ya wasichana ya Marian, ikishika nafasi ya nne.
Shule nyingine ni Seminari ya Don Bosco iliyoshika nafasi ya tano, Kasita seminari nafasi ya sita, St. Mary's Mazinde Juu nafasi ya saba na shule ya Canosa iliyoshika nafasi ya nane.
Shule nyingine tatu katika kumi bora ni Feza Boys iliyoshika nafasi ya pili, Mzumbe nafasi ya tisa na shule ya sekondari Kibaha iliyoshika nafasi ya kumi.
Pamoja na kutupa taarifa hii kwamba katika zile shule kumi bora, saba ni za Katoliki, zipo taarifa nyingine muhimu na nyeti zaidi ambazo Wakatoliki hawajasema. Moja ni idadi yao katika Baraza la Mitihani la Taifa (Tanzania Examination Council). Na pili, idadi yao katika ile jumla ya Maofisa Elimu wa Wilaya na Mikoa (DEOs/REOs).
Katika shule kumi bora kwa kufaulisha, za Wakatoliki ni saba. Je, wakatoliki hawa katika Baraza la Mitihani wapo wangapi? Lakini si idadi yao tu katika Baraza, muhimu zaidi ni je, katika Idara na Vitengo muhimu na nyeti kwa shughuli za utungaji mitihani, usahihishaji, utoaji gredi na kuweka takwimu, Wakristo ni wangapi?
Katika kipindi hicho ambacho Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu akisema kuwa serikali ilikuwa ikilipa gharama zote za kuendesha shule za Kanisa Katoliki, kulikuwa na mgogoro katika wilaya ya Pare (sasa Mwanga) ambapo Wazee wa Kiislamu walitangaza kugoma kulipa kodi kwa kuona kuwa serikali ilikuwa inachukua kodi zao na kuwapa Wakristo kujenga na kuendesha shule, lakini nao walipoomba (kama ndio utaraibu, wakanyimwa). Lakini zaidi walikuwa wakizuiwa kuanzisha shule na kulazimishwa kupeleka watoto wao katika shule ya kanisa. Katika mgogoro huo ilibidi Mwalimu Nyerere kumtumwa (Marehemu) Rashid Mfaume Kawawa kuusuluhisha ambapo kikao kilifanyika Toloha. Wazee wanasimulia kuwa pamoja na kuwa waliandaa chakula kumkirimu mgeni, lakini walikubaliana kuwa kama Kawawa hatakuwa amekuja na jibu la kuwaridhisha, hawampi chakula chao.
Tunajua kuwa kwa maadili ya utumishi wa serikali, mtumishi anatakiwa kuwahudumia watu wote bila ya ubaguzi wala upendeleo. Lakini katika utaraibu huu (usio rasmi) aliotuambia Father Robinson, imani ya wananchi kuwa maadili ya utumishi wa umma yanafuatwa wanapokaa Wakatoliki/Wakristo watupu katika nafasi nyeti na muhimu kama Baraza la Mitihani, itatoka wapi?
Katika kitabu ‘Muslims and the State in Tanzania' kimetajwa kisa cha Waislamu wa Mtwara mjini kuomba eneo la kujenga Msikiti katika barabara (mtaa) maarufu kuliko zote mjini hapo, TANU Road. Ni kando kando mwa barabara hii ambamo zipo ofisi za kiserikali na taasisi mbalimba muhimu za kijamii. Pamoja na kuwa inakisiwa kuwa Waislamu katika mkoa wa Mtwara ni zaidi ya asilimia 85, lakini kulikuwa hakuna hata Msikiti mmoja katika barabara hiyo, wakati kuna makanisa matano (wakati huo 1997) ambayo ni: Kanisa la Katoliki Magomeni, Kanisa la KKKT, Anglikana, Sabato na Catholic Parish Church.
Katika miaka ya nyuma, baina ya kanisa la KKKT na Anglikana, karibu na uwanja wa Mashujaa, palikuwa na eneo ambalo halijatumika lililokuwa likimilikiwa na Wizara ya Elimu na Utamaduni. Mwaka 1995 Wizara ya Elimu kupitia gazeti la serikali ilitangaza kuachia sehemu kubwa ya eneo hilo ili ipangiwe matumizi mengine.
Ni wakati huo Waislamu wa Mtwanra wakaona watumie fursa hiyo angalau nao wawe na Msikiti katika eneo hilo la mjini. Wakaandika barua rasmi tarehe 11 Septemba, 1997 kwa Manispaa kuomba eneo hilo.
Ilipofika tarehe 8 Desemba, 1997, Mipango Miji waliwaandikia barua Waislamu wakiwafahamisha kuwa maombi yao yamekubaliwa. Hiyo ilikuwa barua kumbukumbu namba MM/TC/L.VII/12/89.
Taarifa zinafahamisha kuwa viongozi wa makanisa walipojua kwamba Mipango Miji wameidhinisha Waislamu kupitia taasisi ya MIDECE (Mtwara Islamic Development Centre) wapewe eneo hilo, walikutana wakajadili na kisha kuwaambia waumini wao kuwa Waislamu wanahangaika bure, Wizara ya Ardhi haitawapa eneo hilo.
Haya ndiyo yaliyotamkwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Nsa Kaisi. Mkuu huyo wa Mkoa alimwambia Sheikh, Mzee Nasuma ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bakwata kwamba atahakikisha Waislamu hawapati eneo hilo. Alisema, labda afe au ahamishwe. Lakini muda wa kuwa yupo hai na ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Waislamu hawapati eneo hilo.
Kilichofuatia hapo ni mlolongo mrefu ambao makala hii haitoshelezi kuyaeleza yote. Lakini moja ya mambo yaliyokuwa yakifanyika, ni pamoja na watu wa Ardhi Mkoa kushirikiana na viongozi wa makanisa kujadili namna ya kukwamisha maombi ya Waislamu. Mfano kwa mara ya kwanza Waislamu walipowasilisha maombi yao kwa Ofisi ya Ardhi, walijibiwa kwa kifupi kuwa eneo hilo halikutengwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za ibada. Waislamu wakaridhika wakaondoka. Huku nyuma baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo wakawasiliana na Kanisa la Assemblies of God wakaleta maombi harakaharaka na wakapewa eneo hilo walilokataliwa Waislamu kuwa sio kwa ajili ya Msikiti wala Kanisa. Hata hivyo baadae maofisa hao wa Ardhi walilazimika kuandika barua ya kuwasimamisha Assemblies of God kujenga kanisa katika eneo hilo baada ya Waislamu kuja juu.
Mfano wa pili, katika kuhangaikia suala hili, Waislamu walikuwa wakiwasiliana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wakati huo akiwa Bwa. Mwakatobe. Ambacho Waislamu walikuja kujua baadae ni kuwa wakati Mwakatobe kila siku akiwapa kauli nzuri kwamba atawasaidia, wakiondoka hukutana na viongozi wa kanisa na kuwapa taarifa na kupanga mikakati ya pamoja. Moja ya mikakati aliyowapa ya kuwakwamisha Waislamu ni kuwa waende Dar es Salaam wakamwone Waziri wa Ardhi, wakati ule Gideon Cheyo wamwambie kuwa maombi yao ya kupewa eneo la kujenga kanisa yamekataliwa wakati ya Waislamu yamekubaliwa.
Viongozi wa makanisa Mtwara walifanya kama walivyoelekezwa na RAS wakaenda Dar es Salaam wakamwona Waziri wa Ardhi akawaahidi kwamba atahakikisha kuwa Waislamu hawapati eneo hilo. Lakini Waziri akawaelekeza waende na Wizara ya Elimu na Utamaduni wakamwone Dr. Ndagala ili naye asaidie katika kukwamisha kwa vile eneo linaloombwa awali lilikuwa likimilikiwa na Wizara ya Elimu. Viongozi wa makanisa walimwona Dr. Ndagala naye akaahidi kukwamisha maombi ya Waislamu.
Lakini Dr. V. K. Ndagala akawaambia kwamba, haisaidii sana kuwakwamisha tu Waislamu, yeye angependa baada ya kuwakwamisha Waislamu, basi Wakristo wapewe eneo hilo. Kwa hiyo akawaelekeza wakamwone Afisa mmoja Ikulu ili naye atumie msuli wa Ikulu kuhakikisha kuwa Wakristo wanapata eneo hilo. Taarifa zinafahamisha kuwa Afisa huyo wa Ikulu, aliahidi kutimiza wajibu wake kwa Kanisa. Kuwakwamisha Waislamu na kuwapendelea Wakristo wenzake.
Labda niongeze mfano mmoja, baada ya RAS, Bwana Mwakatobe kukamilisha kuweka mtandao wa kuwakwamisha Waislamu, aliandika barua na kuituma kwa EMS, kuwasilisha maombi ya Waislamu Wizara ya Ardhi, Dar es Salaam. Waislamu walimteua Sheikh Marijani kufuatilia majibu ya barua hiyo Wizarani. Hata hivyo, kila alivyokuwa akifika ofisi inayohusika aliambiwa kuwa hakuna barua iliyopokelewa kwa EMS kutoka Mtwara. Marijani aliamua kwenda ofisi za EMS (Expedited Mail Service) Dar es Salaam ambapo alionyeshwa kuwa barua yao ilichukuliwa na Afisa wa Wizara ya Ardhi anayeitwa Bwana Magambo ambaye ofisi yake ipo ghorofa ya 9 katika jumba la Wizara. Bahati mbaya siku hiyo Magambo hakuwepo kazini. Watu wengine ikabidi wapekuwe na kukuta barua hiyo ikiwa imewekwa katika lundo la makaratasi ya zamani (yanayongojea kuchomwa moto au kufungwa na kuwekwa stoo.)
Hadithi ya kisa hiki bado ni ndefu, lakini tutosheke na kipande hiki. Ila tu niseme kuwa kimiujiza, kwa nguvu za Mwenyezi Mungu, Waislamu walipata eneo lile.
Kama huu ndio mtandao wa Wakristo katika Wizara ya Ardhi, ofisi ya Wakuu wa Mikoa mpaka Ikulu, swali ni je, mtandao kama huu haupo katika Baraza la Mitihani? Ndio maana nikasema, kama ambavyo Kanisa Katoliki limetufahamisha kuwa wanashikilia asilimia 70 katika zile shule bora, ni muhimu pia wakatufahamisha katika Baraza la Mitihani wapo kwa asilimia ngapi?
Kama mtandao wa Wakristo unaweza kujipanga kutoka wilayani, Mkoa, Wizara mpaka Ikulu kiasi cha Mkuu wa Mkoa na Waziri kutamba kuwa atahakikisha kuwa atawakwamisha Waislamu kupata ardhi ya kujenga Msikiti, kwa nini kusiwe na wasiwasi kuwa katika Baraza la Mitihani kunaweza kuwa na mtandao ambao unahakikisha kuwa shule na watoto wa Kikristo ndio wanaoongoza kila mwaka?
Hapa lazima tujiulize, ile kada ya uongozi wa Baraza, Waratibu wa Masomo, Maofisa wa Elimu Wilaya/Mkoa na watu wote muhimu wanaohusika na mitihani pamoja na kuchagua wanafunzi wa kuingia kidato cha kwanza, tano na vyuo mbalimbali, Wakristo wapo wangapi na watu wa dini nyingine wangapi?
Katika hali kama hii ya kisa cha Mtwara, wasio kuwa Wakristo watakuwa vipi na imani na Baraza la Mitihani iwapo itaonekana kuwa nafasi zote nyeti zimeshikwa na Wakristo?
Baada ya kuwa walikuwa na Mkuu wa Mkoa aliyeapa kuwa muda wa kuwa yupo hai na ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, atahakikisha kuwa Waislamu hawapati ardhi TANU Road; sasa Mtwara wamepelekewa Mkuu wa Mkoa ambaye mwaka jana alipewa Nishani ya mtakatifu Gregory Daraja la kiraia kwa utumishi uliotukuka kwa Kanisa Katoliki Mkoa wa Kigoma. Nishani hiyo alipewa na Papa Benedikto wa 16. Na kazi yake imeanza kuonekana katika suala la kufukuzwa kwa wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita Ndanda.
Itakumbukwa kuwa Wizara ya Elimu ilitoa uamuzi kuwa wanafunzi Waislamu waliofukuzwa wakilalamika kuwa walikuwa wakinyanyaswa na Mkuu wa Shule, warudishwe shule na wafanye mtihani.
Hata hivyo baadae Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bwana Joseph Simbakalia anadaiwa kutoa tamko mbadala akidai kuwa msimamo wa kuwafukuza wanafunzi hao uko pale pale na kwamba, vijana 15 kati yao wataruhusiwa tu kuingia katika chumba cha mtihani kama watahiniwa wa nje ya shule (private candidate).
Aidha, Joseph Simbakalia alidaiwa kusema kuwa wanafunzi hao 15 watalazimika kwanza kukubali mashariti watakayopewa kabla ya kuingia katika chumba cha mtihani.
Katika hali hii ya kuwa na watumishi wa serikali ambao wanafikia kiwango cha hali ya juu cha kutumikia makanisa yao mpaka kupewa tuzo na wakuu wa dini zao, je, bado wasio kuwa Wakristo waamini kuwa watu hawa watawatumikia bila ya ubaguzi na upendeleo?
Hivi sasa Kanisa Katoliki lipo katika mchakato wa kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa ni mtakatifu. Hapana shaka hapewi heshma hii kutokana na jinsi alivyowatumikia Watanzania mpaka kuwafikisha mahali wanapanga foleni kutwa wakisubiri robo kilo ya unga wa njano au muhogo. Hawakumpa nishani hiyo kwa kuifikisha nchi hii ambapo kila bidhaa muhimu ikawa haipo, na rushwa kutawala, usemi "mnyonge hana haki" ukatawala kama alivyosema Padiri John Sivalon. ‘Utakatifu' anapewa kutokana na jinsi alivyotekeleza ahadi yake ya kulipa kanisa katoliki "a better chance". Na ni kutokana na "better chance" hiyo, leo Wakatoliki wanatamba.
Swali ni je, hali hii mpaka lini? Sifa gani ambazo zinahitajika kushika nafasi ya uongozi wa Baraza la Mitihani, ambazo watu wengine hawana ila Wakristo tu?
Wapo viongozi watendaji wa ngazi za juu kama Katibu Mtendaji wa Baraza na wasaidizi wake, wapo wakuu wa vitengo muhimu, wapo waratibu wa masomo n.k, je, Wakristo wangapi na Waislamu wangapi?
Kama nafasi hizo watakuwa wamehodhi Wakristo, tufahamishwe, sifa gani zinahitajika ambazo Waislamu hawana mpaka serikali ilazimike kuweka Wakristo watupu?
Malalamiko ya Wazanzibari yasipuuzweWakati Wakatoliki wakisherehekea kwa shule zao kuchukua nafasi 7 katika zile kumi bora, Zanzibar ni kilio. Wanasiasa, walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla, wanajiuliza, imekuwaje idadi kubwa ya shule na wanafunzi waliofutiwa matokeo yao iwe kutoka Zanzibar? Inakuwaje matokeo yao kila mwaka yawe mabaya?
Inawezekana kuna uzembe mkubwa unafanyika katika shule za Unguja na Pemba kiasi cha kuwafanya wanafunzi kufanya vibaya. Labda walimu hawajitumi kusomesha kwa juhudi na wanafunzi hawajali masomo. Inawezekana pia kuna udanganyifu mkubwa na ukiukwaji wa kanuni za mitihani unaofanywa na walimu na wanafunzi wa Zanzibar.
Hata hivyo, kama Mkuu wa Mkoa, anaweza kuapa kwamba atatumia madaraka yake kukwamisha maombi ya Waislamu kupata ardhi, je, hatuoni kuwa watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuwa huenda hata katika Baraza wakawepo wakuu ambao nao wanaapa kwamba watahakikisha kuwa hakuna Mzanzibari (Muislamu) anayeongoza katika mtihani wa kidato cha nne na sita?
Kama Waziri anaweza kukutana na viongozi wa makanisa wakala njama za kuwahujumu Waislamu, kwa nini kusiwe na wasiwasi kuwa viongozi hao wa makanisa wanaweza kukutana na walioshikilia nafasi nyeti katika Baraza na kula njama za kuhujumu watoto wa Kiislamu?
Katika kadhia ya MIDECE na viongozi wa serikali mkoani Mtwara, tumeona jinsi RAS, kinyume na maadili ya utumishi wa serikali, alivyokuwa akikutana na viongozi wa makanisa. Je, mahusiano kama haya hayawezi kutumika katika Baraza la Mitihani kuhujumu wasio Wakristo?
Mtu ambaye ana chuki, upendeleo na ubaguzi dhidi ya Waislamu kama wale waliojitokeza katika mtandao wa watumishi wa serikali katika kadhia ya MIDECE, je hata ikitokea kuwa wilaya au mkoa mmoja katika mikoa ya Zanzibar umeongoza kwa kiwango cha kufaulu, atathubutu kutangaza au ‘atachakachua'?
Labda nimalizie kwa swali, katika matokeo ya mwaka 2010, mkoa gani uliongoza kwa kiwango cha ufaulu?
Baadhi ya taarifa zinasema kuwa ulikuwa Unguja. Je, mkoa huo ulitajwa?
Kama haukutajwa kwa nini wakati tunaona fahari kutaja watoto wa Kikristo na shule za Kikristo zilizoongoza?
Mwaka huu je, Mkoa gani unaongoza kwa kiwango cha kufaulu? Kwa nini ‘data' hiyo muhimu haikutajwa hadharani wakati wa kutangaza matokeo?
Haki inatakiwa itendeke na ionekane kwamba imetendeka. Katika mazingira kama haya ya kuwa na mtandao wa akina Mwakatobe, Gideon, Dr. Ndagala, wakihodhi ofisi za serikali, itakuwa kujidanganya kudhani na kuamini kwamba hakuna hujuma wanayofanyiwa wasio wa dini ya wale waliotupa barua ya MIDECE katika kapu la taka.
 
Kiini cha Hali hii ya Kisiasa
Hali hii ya kisiasa tunayoishuhudia leo nchini mwetu ni matunda ya mbegu liliyopandwa na kupaliliwa kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Wakoloni walikuwa na kanuni yao waliyoiita divide et impero yaani wagawe ili uwatawale. Huko Rwanda wakoloni waliwagawa wananchi kwa misingi ya kikabila. Watusi ambao ni watawala wapewe elimu ya juu na wanfundishwe kwa Kifaransa, na Wahutu ambao ni watawaliwa wapewe elimu duni na wafundishwe kwa Kiswahili. Ubaguzi huo wa kuwagawa raia wa nchi moja ulipandikiza sumu iliyokuja kusababisha Wanyarwanda kuuana.


Hapa kwetu wakoloni walitugawa kwa misingi ya dini. Kabla ya uhuru wa Tanganyika, wakoloni kwa kushirikiana na makanisa waliwaona Waislamu kama ni mahasimu wao kidini na kisiasa. Na kwa sababu hiyo serikali za kikoloni zikaweka mikakati maalum ya kuwakandamiza Waislamu katika maeneo matatu: kwanza kuwawekea vikwazo katika kutangaza dini yao ili wasiongezeke; pili kuwabana katika elimu na ili kuhakikisha kuwa Waislamu wanabanwa jukumu la kuwaelimisha Waafrika likawekwa mikononi mwa makanisa na kazi ya serikali ni kuzigharimia tu shule hizo. Lengo likiwa ni kuwabatiza Waislamu wachache watakaoruhusiwa kusoma, na tatu kuwabana katika ajira serikalini kwa sababu makanisa yote yalisisitiza kuwa kuwaajiri Waislamu serikalini ni kusaidia kuenea kwa Uislamu..


Kwa kuwa ubaguzi huo haukuwa na kificho chochote, Waislamu wengi walijitokeza kupambana na ukoloni kwa matarajio kuwa serikali huru itaondosha chuki na uadui huo dhidi ya Waislamu. Lakini msiba mkuu wa taifa hili ni kwamba kinyume chake, baada ya uhuru msimamo ukawa ni ule ule wa kuwaona Waislamu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na mikakati ya kuwabana Waislamu katika maeneo yale matatu ikaimarishwa zaidi wakati wa utawala wa Nyerere. Kuanzia 1957 mkakati uliopangwa na Kanisa Katoliki ukawa ni kuhakikisha kuwa nafasi zote muhimu za uongozi na serikali zinashikwa na wao. [Taz. Confidential Diary – Tanganyika, March-April 1957, uk. 3-4 Maryknoll Central Archives, New York ]. Na ni mkakati huu ndio ambao Mwalimu Nyerere aliokuwa akimuhakikishia Askofu Rweyemamu mwaka 1970 kuwa anatumia mamlaka yake kama Rais na kama kiongozi wa TANU kuhakikisha kuwa anatoa upendeleo maalum kwa Wakristo ili wasimamie sera za Chama. Na kwamba amemteua padiri katika nafasi nyeti ya Chama si kwa sababu anajua siasa bali kwa sababu ni Mkristo safi. Lakini Nyerere huyo huyo akisimama hadharani alijidai kukemea udini. Na kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuliimarisha kanisa na kuwadhoofisha Waislamu, leo Kanisa lake limo katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa ni Mtakatifu!


Sivalon anaarifu katika kitabu chake kuwa mara baada ya uhuru Kanisa katoliki liliwahamasisha Wakristo wote na hasa watendaji wa serikali juu ya hatari ya Ukomunisti na Uislamu na walikusanya nguvu zao zote katika kukabiliana na maadui hao.


Matokeo ya Hujuma Hizo
Matokeo ya hujuma hizo za kichinichini ni kwamba katika sura ya nje na katika propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na kisiwa cha amani. Lakini uhalisia wa mambo ni kuwa Tanzania ni nchi yenye jamii kubwa mbili. Jamii ya Wakristo wanaopewa msaada, upendeleo, ulinzi na heshima, na jamii ya Waislamu ambao wanachukiwa, kudharauliwa na kudhoofishwa na serikali kabla na baada ya Uhuru. Ifuatayo ni mifano michache tu ya baadhi ya hujuma hizo baada ya Uhuru.
<!--[if !supportLists]-->(1) <!--[endif]-->Mwaka 1963 katika Barua ya Kichungaji, Kanisa Katoliki lilisema Waislamu walikuwa wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao, jambo ambalo ni "hatari kubwa kwa hatima ya Wakristo wetu" na Sivalon anabainisha kuwa Wakristo walimwomba Nyerere awasaidie kuvuruga umoja huo wa Waislamu. Ndio sababu ya Nyerere kutumia dola kuiparaganya EAMWS. Kwa kuwa Waislamu ni jamii inayotakiwa kuwa dhalili, hawatakiwi kuwa na umoja. Ndio maana tangu wakati wa Nyerere hadi leo, uchaguzi wa viongozi wa Waislamu husimamiwa na vyombo vya dola. Nia ikiwa ni kutokuwapa Waislamu uhuru wa kuwachagua viongozi wao. Katika taifa moja haki hiyo ni ya Wakristo peke yao. Sote ni mashahidi kuwa mwaka 1994 serikali ilimwagiza Naibu Waziri Mkuu Mh. Augustino L. Mrema kuhakikisha kuwa Bakwata inapitisha katiba mpya inayotakiwa na serikali. Na Maaskofu wakachangia gharama. Waislamu ni maadui kidini na kisiasa, lazima wadhibitiwe.


<!--[if !supportLists]-->(2) <!--[endif]-->Mwaka 1992 Serikali ya Tanzania ilitiliana saini Makubaliano ya Itifaki rasmi na Makanisa ya TEC na CCT. Kwa mujibu wa makubaliano hayo ambayo yalitiwa saini na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye wakati huo alikuwa Mh. Edward Lowasa serikali imewajibishwa pamoja na mambo mengine, kutenga nafasi za masomo kwenye vyuo vyake vya Ualimu mahsusi kwa ajili ya wanafunzi wanaopangwa kufundisha katika shule za Kanisa; pia kutoa ruzuku ya kuendeshea taasisi za Makanisa. Kuanzia 1992 hadi leo serikali imetoa mabilioni ya kodi za wananchi kwa Makanisa. Katika kipindi chote hicho Waislamu wamepinga ubaguzi huo. Lakini kwa kuwa lengo ni kuwaimarisha Wakristo ambao ni jamii inayotakiwa kupewa nguvu zaidi dhidi ya jamii ya Waislamu ambao wanatizamwa kama maadui, serikali imeyapuuza malalamiko ya Waislamu. Lakini propaganda zinaendelea kuwa Tanzania ni nchi moja yenye mshikamano na umoja na ni kisiwa cha amani.


<!--[if !supportLists]-->(3) <!--[endif]-->Waislamu wameiomba serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo itakayowezesha nchi yetu kupata misaada itakayotumika kuinua hali za Waislamu ambao wameachwa nyuma sana katika elimu na uchumi. Makanisa yote kwa kauli moja yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hilo. Sababu ya kupinga kwao ni kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanadhoofishwa katika kila hali, na ni makosa makubwa kuwaimarisha kiuchumi au kielimu maadui hao. Serikali ilipofanya utafiti wake wa kina ikajiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote. Na Mh. Bernard Membe alitamka hilo Bungeni. Mara akaitwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Cardinali Pengo na kukumbushwa mkakati wa kuwadhoofisha Waislamu. Msimamo wa serikali ukabadilika. Lakini propaganda za kuwazuga Waislamu zinasema Watanzania wote ni kitu kimoja na nchi hii haina ubaguzi!


<!--[if !supportLists]-->(4) <!--[endif]-->Kwa kuwa tangu wakati wa ukoloni hadi leo mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa Waislamu wanaminywa kadiri iwezekanavyo katika nafasi za uongozi na ajira, ndio maana hadi leo, miaka 50 baada ya Uhuru Waislamu ni wachache sana katika nafasi zote za uongozi na ajira katika sehemu muhimu serikalini na katika vyombo muhimu vya maamuzi. Kisingizio kinachotolewa ni kuwa Waislamu hawataki kusoma. Lakini ukitazama orodha ya Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa na sifa zao, utaona dhahiri kuwa wapo Waislamu wengi wenye sifa bora zaidi ambao wangestahili kuwa ma-DC. Waislamu hawateliwi kwa sababu mkakati uliopo ni kuwatenga Waislamu na ikiwezekana kuwaondosha kabisa katika sehemu muhimu za uongozi, kwa sababu kama wao hawajui ukweli ni kwamba hawatakiwi kushika nafasi zozote muhimu za uongozi au ajira. Ndio maana asilimia 75 ya Ma-DC wote ni Wakristo na karibu wasimamizi wote wa Uchaguzi katika wilaya ni Wakristo. Wabunge asilimia 75 pia ni Wakristo, na hali ni hiyo hiyo katika Vitengo vya serikali na Mashirika ya uma. Ndio maana hakuonekani tatizo lolote pale taasisi yote inapokuwa na Wakristo watupu. Na kelele nyingi maadui wa serikali na Kanisa wanapopewa nafasi hata kama wana uwezo kiasi gani. Katika sura ya nje Tanzania ni taifa moja, katika uhalisia wake ni kuna mataifa mawili, moja nyonge na jingine lenye nguvu.


<!--[if !supportLists]-->(5) <!--[endif]-->Kwa kuwa Waislamu wanahesabiwa kuwa ni maadui, ule mkakati uliowekwa na wakoloni wa kuwawekea vikwazo Waislamu katika kutangaza dini yao unaendelea hadi leo. Ipo mifano mingi sana ya Waislamu kukamatwa, kutiwa ndani na kunyanyaswa na vyombo vya dola kwa sababu tu ya kulingania hadharani dini yao. Kwa kuwa Waislamu ni maadui, basi ni muhimu kuhakikisha kuwa hawaongezeki. Wakristo wanayo haki ya kuitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa Yesu ni Mungu. Wao ni jamii inayostahiki ulinzi wa dola. Lakini pindi Mwislamu atakaposema hadharani kuwa Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi siyo Yesu mwana wa Mariamu atakuwa amekashifu dini ya dola na atakamatwa na kubughudhiwa. Lakini kipropaganda, Tanzania ni nchi moja na inafuata katiba moja. Lakini uhalisia ni tofauti.


<!--[if !supportLists]-->(6) <!--[endif]-->Msimamo wa serikali na makanisa kuhusiana na mauaji ya Waislamu katika msikiti wa Mwembechai ni kielelezo kingine cha ukweli kuwa Tanzania ni mkusanyiko wa jamii mbili zenye haki na hadhi tofauti katika taifa moja. Kwa kushinikizwa na Maaskofu serikali iliwauwa Waislamu watatu Mwembechai pasi na hatia yoyote. Waislamu waliiomba Mahaka, Bunge na hata Rais aunde Tume ya uchunguzi. Mihimili yote ya dola ilikataa. Kiongozi wa Kanisa Katoliki akenda mbali zaidi. Akahalalisha mauaji hayo. Kwa sababu waliouliwa ni wale maadui wa ile jamii nyoge isiyotakiwa kustawi. Lakini alipouliwa mbwa "Imigresheni" mwaka huo huo wa 1998, Jaji Mkuu wa wakati huo Mh. Francis Nyalali aliamuru uchunguzi wa kuuliwa mbwa huyo na hakimu akaadhibiwa. Jaji Mkuu alichukua uamuzi huo bila kuombwa na mtu. Lakini wale waliowauwa Waislamu walipongezwa na kupandishwa vyeo. Uhasama wa serikali na makanisa dhidi ya jamii ya Waislamu ni wa kiwango cha kutisha. Msimamo ukawa huo huo walipouliwa Waislamu Unguja na Pemba 2001 kwa kuandamana kudai Katiba Mpya. Lakini kipropaganda tunaambiwa Watanzania wote wanahaki sawa.


<!--[if !supportLists]-->(7) <!--[endif]-->Rais wa Marekani George W. Bush alipotangaza Vita vya Msalaba dhidi ya Waislamu mwaka 2001, serikali ya Tanzania ikapata uhalali zaidi wa kuzidi kuwakandamiza Waislamu. Serikali ikawa radhi kuvunja Katiba ya nchi kwa kupitisha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya 2002 ili zipatikane fursa zaidi za kuwanyoongesha Waislamu. Waislamu waliipinga sheria hiyo kwa nguvu zao zote, lakini kwa kuwa wao ni jamii inayotakiwa kupigwa vita hawakusikilizwa. Bunge ambalo nalo lina Wakristo wengi likaipitisha haraka sheria hiyo. Naam, tangu imepitishwa hadi leo, sheria hiyo imetumika kuwadhuru Waislamu wasiokuwa na hatia yoyote, na kufunga taasisi zilizokuwa zikiwasaidia Waislamu. Misaada ni haki ya Wakristo, siyo Waislamu. Pamoja na madhila yote hayo Waislamu wanatakiwa waendelee kuamini kuwa Tanzania ni nchi moja inayojali raia wake wote.


<!--[if !supportLists]-->(8) <!--[endif]-->Wakati serikali ikidai kuwa Tanzania ni taifa ambalo raia wote wana haki sawa, lakini serikali hiyo hiyo kwa makusudi kabisa inafanya jitihada za waziwazi za kuwahamasisha Wakristo wawaone Watanzania ambao ni Waislamu kuwa ni maadui zao na maadui wa taifa lao. Januari 2001 Waziri Mkuu Mh. Frederick Sumaye alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa serikali inazo taarifa kuwa kundi la magaidi waliopata mafunzo nchi za nje limerejea nchini na magaidi hao wanapanga kuilipua hospitali ya Muhimbili. Kufuatia kauli hiyo Waislamu watatu wa Muhimbili ambao ni Waislamu akiwemo Profesa wa Micro-Biology walitiwa mbaroni. Japo baadaye waliachiwa kwani hawakuwa na hatia yoyote, lengo la serikali la kupandikiza sumu ya chuki lilikuwa limetimia. Tarehe 24 Agosti 2001 Waislamu walifanya maandamano kupinga kufungwa kwa Dibagula kwa kusema Yesu si Mungu. Serikali kupitia jeshi la polisi likawatangazia wananchi wote kuwa Waislamu wamepanga kuyalipua makanisa siku ya Jumapili ya tarehe 2 Septemba 2001. Na serikali ikawahakikishia Wakristo kuwa itaweka maaskari wa kuwalinda na hiyo shari ya Waislamu. Lengo la uzushi huu ni kuwachochea Wakristo wawachukie Waislamu na hivyo waunge mkono hatua za serikali za kuwapa kipondo. Hivi sasa huo umekuwa ni mchezo wa kawaida. Kila baada ya muda Fulani serikali kwa kpitia jeshi la polisi hutoa taarifa za kuonesha kuwa kuna mpango wa shambulio la kigaidi. Na watuhumiwa siku zote ni Waislamu. Serikali na makanisa yanawachukia Waislamu kiasi cha kuwa tayari kushirikiana na wasiokuwa Watanzania katika kuwahujumu Waislamu. Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, Maaskofu wakipata kisingizio chochote watakuwa tayari kuwauwa Waislamu kama walivyoshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda.


<!--[if !supportLists]-->(9) <!--[endif]-->Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania. Katika ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita [Commission of Armed Forces] ndani ya Kanisa hilo. Tangu wakati huo hadi leo Waislamu wameitaka serikali iwaondoshe hofu kwa kuweka wazi kazi za Tume hiyo ya Majeshi ya Kivita ndani ya Kanisa. Serikali haijajibu na wala haijajishughulisha na taarifa nzito kama hizo. Hatujui kama Tume hiyo ya Majeshi ya kivita inafanya kazi ndani ya Jeshi la Wananchi au nje ya jeshi hilo. Lakini kwa muktadha wa hali ya uhasama wa serikali na hasa wa Maaskofu dhidi ya Waislamu wanaowahesabu kuwa ni maadui zao, si vigumu kukisia kwa nini Kanisa Katoliki limeunda Tume ya Majeshi ya Kivita. Lakini serikali ambayo haishughulishwi kabisa na Tume ya Majeshi ya Kivita ya Wakatoliki imekuwa na tabia ya kuwakamata na kuwatia ndani Waislamu kwa kesi za kuwabambikia zisizokuwa na kichwa wala miguu. Lakini propaganda zinasema Tanzania ni nchi moja yenye katiba inayolinda haki za watu wote. Mwenye mach haambiwi tazama.


Dalili ya Mvua ni Mawingu
Alipokuwa akitoa mada yake juu ya "Mifumo ya Viashiria vya Migogoro" katika Mkutano wa Kumi na Moja wa Hali ya Siasa Tanzania ulioandaliwa na REDET mwaka 2003, Mh. Bernard L. Membe alisema kwamba migogoro mingi duniani na hasa vita vya wenyewe kwa wenyewe vina dalili na viashiria vyake. Akasema miongoni mwa dalili kubwa kuwa nchi karibu itaingia katika machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kutokea kwa mgawanyiko au kutokea kutoelewana kwa viongozi ndani ya chama au serikali tawala.


Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri wakipingana hadharani juu ya maamuzi waliyoyafanya wenyewe. Lakini pia katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia pia mgongano wa waziwazi kati ya wabunge wa CCM na Chama chao. Na wote hao hawachoki kujisifu kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere. Lakini mwaka 1993, Nyerere katika Kitabu chake Tanzania! Tanzania! Aliandika na tunanukuu:
Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hoja ya hadhi ya Bunge. Ni nani huyu anayefanya kazi hii? Ni haki kabisa ya vyama vya upinzani kujaribu kugombanisha Wabunge wa chama kinachotawala na chama chao. Lakini viongozi wa chama kinachotawala pamoja na Serikali yenyewe wanapojaribu kufanya mambo ambayo yatagombanisha Wabunge wa CCM na chama chao, tuna haki ya kuwauliza viongozi hao wanafanya kazi hii kwa niaba ya nani, na chama chao ni chama gani? [uk. 41]
Pamoja na kuyajua yote hayo hivi sasa kuna msuguano ulio dhahiri kabisa baina ya Wabunge wa CCM na Chama chao. Kiashiria kingine alichokitaja Mh. Membe ni kwa serikali kushindwa kuyashughulikia malalamiko mbalimbali ya wananchi yanayoelekezwa serikalini.


Maazimio ya Waislamu
Kwa kuzingatia muktadha wa hali ya kisiasa ilipofikia hivi sasa, Waislamu tumefikia maamuzi yafuatayo:


(1) Maadam Mfumo Kristo umeimarika kiasi cha kuweza kuitisha serikali na viongozi wake na wakatishika, na maadam Mfumo huo Kristo una nguvu za kuweza hata kuvitisha na kuvikemea vyombo vya dola na vikasalimu amri, Waislamu tutake tusitake, kama alivyohadharisha Mh. Membe, ukweli unabaki kuwa hautapita muda mrefu, dhulma hii ya udini italisambaratisha Taifa letu, kama udini ulivyoisambaratisha Ivory Coast ambayo katika miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa mfano wa kuigwa.


Hivyo basi wajibu wetu wa mwanzo ni kuufikisha ujumbe huu kwa Waislamu wote nchini, na kuwataka wazingatie kuwa kwa kuwa wanabaguliwa na kudhalilishwa katika nchi hii kwa sababu ya Uislamu wao, basi ni wajibu wao na wao kushikamana kama Waislamu.


(2) Kwa kuwa kila wanchosema Maaskofu ndicho kinachofuatwa na serikali, na kwa kuwa Maaskofu wamekwishatamka hadharani na kwa sauti kali kuwa katika nchi yetu hakuna kabisa udini na atakayesema kuna udini basi ni yeye ndiye anayetaka kuleta udini, na kauli hiyo kudakwa na mawakala wa Maaskofu katika serikali, ni dhahiri kuwa dhulma za udini zinazoendelea kuwakandamiza Waislamu miaka 50 baada ya Uhuru hazitaondoshwa na Katiba mpya. Hivyo wajibu wetu mwingine ni kupigania ukombozi wa Waislamu ili washiriki katika kuandaa katiba mpya wakiwa ni raia huru na sawa na wenzao. Waislamu popote tulipo tunao wajibu wa kuorodhesha dhulma zote za udini tunazofanyiwa na kupigania ziondolewe kwanza na kulipwa fidia.


(3) Kwa kuwa tangu ukoloni hadi leo Waislamu wanahesabiwa na serikali na Maaskofu kuwa ni maadui wa kupigwa vita na wasiostahiki haki sawa na wengine, na kwa kuwa Waislamu wameazimia kutokukubali tena kudhulumiwa na kuonewa kwa namna yoyote ile iwayo, ni wazi kuwa hakuwezi kuwa na katiba itakayoweza kulinda haki za madhalimu na wadhulumiwa kwa wakati mmoja. Ingawa kwa propaganda za kisiasa Tanzania ni nchi moja, lakini kiuhalisia ni nchi yenye jamii mbili zenye hadhi na haki tofauti kabisa. Umefika sasa wakati wa kugawana nchi ili Waislamu wanaochukiwa na kunyimwa fursa sawa na Wakristo waishi katika maeneo yenye Waislamu wengi na Wakristo waishi katika maeneo yenye Wakristo wengi. Mwalimu Nyerere alipigania kwa nguvu zake zote Nigeria igawanywe ili Wakatoliki ambao walikuwa wanadhulumiwa Nigeria wajitenge na waruhusiwe kuishi katika nchi ya Biafra. Na katika kijitabu alichokiandika 1966 Nyerere alisema madai ya kuhifadhi umoja wa kitaifa wa Nigeria hayana maana yoyote pale ambapo baadhi ya raia wa taifa hilo wanadhulumiwa. Ushahidi wa dhulma za Waislamu upo wazi. Kugawana nchi kutawawezesha Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC bila ya kuwakera Maaskofu. Ni wajibu wetu kulifikisha hili kwa Waislamu wenzetu nchi nzima ili lijadiliwe zaidi kabla halijafikishwa rasmi
(4) Kwa kuwa hakuwezi kuwa na amani ya kweli bila ya haki, na kwa kuwa amani ya Tanzania inashikiliwa na Waislamu walioruhusu dhulma hiyo, Waislamu tunayo dhima kubwa kwa kustawi kwa Mfumo Kristo ambao sasa hapana shaka yoyote unalisambaratisha Taifa. Lakini kama alivyosema Nyerere, anayedhulumiwa ni mtu anayeteseka. Asipopambana na huyo dhalimu, yeye ataendelea kuteseka wakati dhalimu anastarehe kwa amani. Akiamua kupambana, wote yeye na dhalimu watateseka. Baada ya miaka 50 ya kuachia kundi moja la jamii likistarehe na hali Waislamu wanateseka, umefika wakati sasa wa kugawana machungu ya udini tuliyoyabeba peke yetu kwa miaka hamsini.
 
SERIKALI YA TANZANIA HAINA DINI
Katika katiba ya Tanzania inasema Tanzania haina dini ila watu wake wana dini nafikiri kipengele hiki kina utata;
1. Hakuna uhuru wa kuchinja
2. Kwanini kuna ubalozi wa VATICAN wakati Tanzania haina dini
3.kwanini kuna MOU kwa kundi moja na kuacha kundi jingine
4. kwanini takwimu za kisensa zisitambue wananchi wake pamoja na dini zao
Tunaomba katiba ibadilishwe kwani ina mapungufu
Serikali ya Tanzania ina dini, nayo ni UKRISTO (MFUMO KRISTO). Ndo maana MoU imeruhusiwa kwa serikali kugawa pesa za walipa kodi kwa kuliendesha kanisa na kukubali Ubalozi wa PAPA kwa maslahi ya KANISA huku ikikataa kuwa mwanachama wa OIC ili waislamu wasinufaike na misaada toka kwa waislamu wenzao. Hii imewafanya waislamu kukosa biashara isiyo na riba na kutumbukia kwenye lindi la RIBA
 
Mtot hoja hapo juu anasema serikali imeingia mnataka na Vatican kama kanisa. We unaesema jeshi la Vatican liko wapi naomba unioneshe jeshi la nchi ya Costa Rica
 
Hayo ni maoni yako na unahaki kabisa ya kuamini hivyo! lakini usijidanganye kuwa Waislamu wataridhika pindi Serikali ikija kufafanua hayo uliyoyaeleza! Kamwe Serikali haiwezi kukanusha hayo sababu Waislamu wanaushahidi wa Kisayansi unaothibitisha madai yao ndio maana Serikali haina uso wa kukanusha madai mazito na ya msingi ya Waislamu? labda iwe ni Serikali ya kiwendawazimu ndio itakuwa na ubavu wa kukanusha madai ya Waislamu! ni zaidi ya nusu karne sasa Serikali inaimba majukwaani kuwa haina dini huku ikilipa Kanisa upendeleo maalum dhidi ya dini ya Kiislamu! ushahidi mdogo, ktk miaka ya 70 Rais wa Tz alimteua Padre asimamie kitengo cha siasa ktk halmashauri kuu ya TANU na kumhakikishia mwakilishi wa Papa kuwa amemchagua Padre huyo kwasababu ya uchamungu wake na yeye Mwalimu atahakikisha Kanisa linalindwa vizuri TZ kuliko mahala pengine popote!

Kwanini na Shehe hakuchaguliwa? huo kama sio udini ni nini?
Waislamu msimamo wao ni Serikali isimamie haki na uadilifu na kamwe Waislamu hawataki upendeleo bali haki sawa kwa wote! dini inayopenda kubebwa na kubembelezwa inajulikana!

Kadogoo uko sawa, hawa jamaa wamezoea kubebwa ndo maana hata muislamu akisema ukweli kuhusu uislamu wao hukimbilia kutafuta msaada wa polisi maana hawana hoja za kuutetea huo upotofu wao
 
Watu wanaotaka ubalozi wa Vatican uondolewe watwambie pia balozi za Saudia Arabia, kuwait, Iran sasa Egypt n.k nazo zinafanya nini hapa Tanzania, hizi nchi nilizozitaja zinajulikana kama ni nchi za kidini, nchi kama Iran imefika mbali zaidi, inatesa sana Wakristo, sielewi kwanini mleta uzi na wanaoshabikia hilo la Vatican haya mengine hua hajiulizi? Utafiti mdogo nilioufanya kwa wale wanaopenda sana mambo ya udini kua, mara nyingi jambo linapofanya na dini yao hata kama lingekua baya kiasi gani (au mtu wa dini yao angefanya jambo baya kiasi gani) hua halionekani kama ni baya, ni mtu mpumbavu tu na kipofu anaye weza kuhoji uwepo wa balozi wa Vatican and then anasahau presence ya mabalozi wa nchi za Kislam hapa. Misaada inayoletwa kwa mwavuli wa dini kwa Wakristo utakuta hata Waislam wanafaidika lakini mingi ya Kislam inabagua, hivi hapo mdini nani? Angalia chuo cha kislam Morogoro, staff na wanafunzi wote ni dini moja, nenda Tumaini, SAUT n.k utakuta hadi Wapemba kule, bado napata shida hii, zamani watu walikua wanajichagulia vyuo vya kwenda (bado waislam wengi walikua wakiomba kwenda huko kwenye vyuo vya Kikristo) sasa hivi TCU ndio wanaodahili, sielewi hvi kigezo cha pale Morogoro hua inakuaje na TCU? kama nao wanadahili kwa kutumia dini, basi nchi hii ni ya Kislam na kama sio hivyo, watwambie wanafanyaje hadi wanaokwenda pale ni wa dini moja tu?

Kwenye mashule, sasa hivi unaweza kuwatambua watoto wa kike kwa dini zao, mavazi, nenda hata sehemu za kazi nako ni hivyo hivyo tu, nchi hii kwasasa ni ya Kislam, tusiganganyane.
 
Back
Top Bottom