zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,683
- 3,226
Nafikiri kuna watu walikitumia kifo cha Magufuli ili kujaribu kumshawishi mama ajipambanue kama yeye nje ya dira, falsafa na wingu vilivyotanabaisha kile wanachokiita "Serikali ya Magufuli".
Wengi wa hawa watu ni wa kutoka upinzani na wale ambao kwa namna moja walimwona kama Magufuli aliwaletea kiwingu kwenye mambo yao. Hao wanaitaka Tanzania "mpya" kabisa tofauti na Tanzania ilivyokuwa chini ya Magufuli.
Kwa bahati mbaya sana kwao Magufuli had a lot of common sense katika siasa zake. Hakuna alichokifanya Magufuli ambacho kwa namna moja au nyingine hakikuwa inspired na matamanio ya watanzania walio wengi, hasa baada ya miaka 10 ya JK.
Magufuli alikuwa very suspicious na motives za western powers kwa nchi za Afrika, pamoja na ukoloni mamboleo unaolenga kuifanya Afrika liwe dampo au soko la bidhaa kutoka nchi za magharibi.
Na ufanisi wa JPM katika mambo yake ni kwa sababu ya falsafa zake hizo. Sasa mama ana kibarua kizito mbele zake. Kama anataka kuwafurahisha wale ambao waliona Magufuli hafai basi awe tofauti na Magufuli kwa kila kitu. Kwenye siasa za ndani, basi aturudishe enzi za JK ambako kila kukicha wapinzani ilikuwa kuandamana huku na kule wakitangaza maovu ya serikali na ufisadi wake. Walau leo hii Mbowe ameizunguka Tanzania sijamsikia akihubiri ufisadi (sijajua kwa nini). Kwenye siasa za kimataifa mama alianza kwa kutaka "kuifungua" nchi, as if nchi ilikuwa imefungwa. Matokeo yake nadhani ndio haya ya wamarekani kutoa msaada wa chanjo ya corona. Yikes!