Serikali ya Libya inasema mwandishi maarufu amekamatwa

Serikali ya Libya inasema mwandishi maarufu amekamatwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,436
Reaction score
5,078
Mwandishi wa habari maarufu wa Libya amekamtwa na kuwekwa kizuizini na chombo cha kijasusi ambacho kinatajwa kuwa na uhusiano na serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Chombo hicho kilimtia nguvuni Reda Fhelboom akiwa katika uwanja wa ndege nje kidogo ya mji wa Tripoli, muda mfupi baada ya kuwasili Jumamosi, akitokea taifa jirani la Tunisia.

Fhelboom ni mwasisi wa asasi inayopiginia uhuru wa upatikanaji habari "The Libyan Organization for Independent Media" ambayo imekuwa ikifanya kazi ya kuchunguza visa vya ukandamizaji dhidi waandishi wa habari wa Libya, pamoja na kuhamasisha uhuru wa habari na kupiga vita uchochezi wa mitandaoni.

Hata hivyo katika taarifa yake wizara ya mambo ya ndani ya Libya imekanushia kushiriki kwa namna yoyote kushiriki katika zoezi la kumkamata Fhelboon na kukionesha kidole kitengo cha huduma za usalama wa taifa hilo na kukitaka kitoe ufafanunzi kwanini ukamataji huo ukatekelezwa.
 
Back
Top Bottom