Serikali ya JK imepoteza mwelekeo-Lipumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya JK imepoteza mwelekeo-Lipumba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Mar 31, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Serikali ya JK imepoteza mwelekeo-Lipumba


  Na Benedict Kaguo, Tandahimba

  MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Serikali ya Rais Jakaya imepoteza mwelekeo hadi inayosababisha migongano
  baina baina ya viongozi kwa viongozi akitolea mfano suala la Waziri wa Ujenzi John Magufuli kuumbuliwa na rais mbele ya mkutano wa hadhara.

  Badala yake alisema ingekuwa vema kwa rais kumuita katika Baraza la Mawaziri ili kumweleza udhaifu wake kuliko kumshambulia mbele ya umma wa Watanzania na kuifedhehesha serikali mbele ya wananchi.

  Akihutubia wakazi wa Mji wa Tandahimba Mkoani Mtwara katika mwendelezo wa mikutano ya operesheni Zinduka juzi jioni, Profesa Lipumba alisema kitendo hicho kimeonesha udhaifu mkubwa wa uongozi uliooneshwa na Rais Kikwete.

  “Ndugu zangu Serikali ya CCM inasambaratika, na hili suala la Waziri Magufuli kukanywa na Rais Kikwete kwenye mkutano wa hadhara ni kielelezo cha rais kushindwa kuongoza nchi, hii ni fedheha kubwa kwa serikali,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema hali hiyo wananchi wanapaswa kuiona kuwa ni ishara ya serikali ya CCM kushindwa kuongoza nchi, ndio sababu kumekuwepo na matukio mengi ya migongano kati ya viongozi wa juu wa serikalini.

  “Watu wanaoweza kukaa kwenye Baraza la Mawaziri wakazungumza lakini watu wanaumbuana hadharani, sasa Waziri Magufuli anakanywa mbele ya umma ni wazi uwezo wake katika maamuzi utakuwa umetetereka,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema jambo la msingi badala ya viongozi hao kulumbana hadharani wangekuwa ndani ya Baraza la Maziri na kutoa mawazo mazuri juu ya utekelezaji wa suala hilo la bomoabomoa kwani huwezi kumbomolea mtu nyumba wakati hakuna bajeti ya kujenga barabara.
  [​IMG]


  1 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Lipumba unafiki utakumaliza:
  Chadema wakisema maneno hayo hayo unasema wanachochea vurugu... yetu macho na masikio.
  Hata hivyo sipingi hoja yako ya msingi kuwa CCM inaenda mrama. Ninachoogopa ni kuwa wapinzani hamkai sawa ili kuziba ufa huo wa uongozi ili CCM wakiondolewa tuwe na timu nzuri ya kuongoza.
  Kingine cha kustaajabisha ni kutowasikia UVCCM, ambao wamejipachika ukiranja wakilisemea hilo la Kikwete kutotatulia tofauti za maamuzi ndani ya vikao husika.
  Sasa nitawakumbusha kama walikuwa hawajui/wamesahau: Tabia ya kusemea nje ya vikao halali imejikita zaidi kwa Mwenyekiti wao na si Sumaye
  March 30, 2011 11:47 PM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Lipumba ni kauli tata..........leo anamsifia JK kesho anamsigina.................................looks like he is a double dealer to me..................
   
 3. g

  gepema Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Prof **pumba ameshaka inabidi atulize kitenesi ili aweze pata angalau kajiheshima kadogo
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Mtu Mzima HOVYOOOOO! Kama kweli anamaanisha anachokisema basi CUF wajitoe katika Serikali ya mseto kule Z'bar, vinginevyo ni USANII MTUPU!
   
 5. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yuko huku na huku,kama chaja ya kobe 'kajiimbia babu ayubu' hivi si nlisikia lipumba si rizki,otherwize kweli atakua chaja ya kobe,anaenda kotekote,apiga na kupigwa.
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Katika mfumo wa demokrasia kwa jumla, upinzani hauna maana ya kupinga kila kitu. Sioni ubaya wa kusifia ikiwa mtu katenda linalopaswa na kumsigina ikiwa amechemsha. Bahati mbaya hapa JK ni mchemshaji sugu na kwa hiyo sikubaliani na unafiki wa CUF na viongozi wao.
   
 7. N

  Ntandalilo Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Ndugu zangu Serikali ya CCM inasambaratika, na hili suala la Waziri Magufuli kukanywa na Rais Kikwete kwenye mkutano wa hadhara ni kielelezo cha rais kushindwa kuongoza nchi, hii ni fedheha kubwa kwa serikali," alisema Profesa Lipumba.

  "Watu wanaoweza kukaa kwenye Baraza la Mawaziri wakazungumza lakini watu wanaumbuana hadharani, sasa Waziri Magufuli anakanywa mbele ya umma ni wazi uwezo wake katika maamuzi utakuwa umetetereka," alisema Profesa Lipumba.
  ............................................................. Charlatan!!!!!
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nina mashaka na watu anao wahutubia pia,sijui huwa hawana kazi za kufanya wanaenda kusikiliza pumba,...mtu wa kung'ata na kupuliza ni zaidi ya shetani
   
 9. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtapa maji! Lipumba ni pumba, huyu kwa mtizamo wa haraka haraka huyu profesa ni mbinafsi wa hali ya juu na sitashangaa Lipumba akigombea Urais 2015.
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Lipumbaaa!!!!
  Acha unafiki wewe!
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Lipumba asemee ndani ya chama, yaani ccm b:teeth:
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hatujui ANAOGA au ANAOGELEA kwenye dimbwi la siasa
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ha ha haaaaa. :bored:Duh prof
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ni hivi...hajawahi kumsifia kwa kuwa hakuna cha kumsifia....shida yake yeye ampinge JK sawa.....wengine wakimpinga yeye hakubali....ndio utata wake
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Lipumba anajikosha tu, hana lolote.
  CHADEMA wamefanya maandamano kuhusu hayo lakini Lipumba na akina Mrema wakaanza kuwaponda Chadema. Sasa iweje leo ajitokeze aanze kuona hilo wakati akiwaponda wenzake?

  Huu ni umalaya wa kisiasa, mchana uko majukwaani unaiponda serikali lakini wakati wa Usiku mko pamoja?
   
 16. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lipumba ni aina ya ndege waitwao Lipyoto, anauma na kupuliza kwahiyo hana msimamo! Lipumba wa sasa hivi ni mara mia ya Makamba na Tambwe Hiza maana wao ni wasema hovyo na waropokaji lakini wako CCM na si wanafiki kama Lipumba. Hata kama wamefunga ndoa na CCM inabidi awe na msimamo kwenye masuala ya msingi ya taifa hili. Inauma sana kuona wasomi mahiri kama Lipumba wamebakia kuwa wanafiki na wanadanganyika na ufisadi wa CCM kama watoto wadogo, unategemea nini kwa watu ambao hata mlo mmoja kwa siku ni shida? Lipumba ameshindwa siasa anatakiwa arudi tu kwenye kazi yake ya uhadhiri badala ya kuendelea na siasa za majitaka!!
   
Loading...