Serikali ya JK ilipwaya 2011; Mawaziri waliumbuana hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya JK ilipwaya 2011; Mawaziri waliumbuana hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145

  na Mwandishi wetu - Tanzania Daima


  UTENDAJI wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete umeelezwa kuwa uliyumba kwa kiasi kikubwa katika mwaka 2011 huku matukio ya ufisadi, wizi wa mali ya umma na tabia ya kuwalinda wazembe yakishamiri.

  Viongozi mbalimbali wa dini na siasa wakihojiwa na Tanzania Daima jana walisema kuwa serikali ya Kikwete ilijitahidi kufanya vema mwaka huu, lakini hata hivyo ilipwaya katika mambo mengi ya msingi.

  Walisema kuwa taifa limejikuta likikosa mwelekeo kutokana na kuzuka kwa mambo mengi ya kusikitisha na hata kushangaza, ikiwa ni pamoja na malumbano makubwa kati ya mawaziri wa serikali.

  Kauli ya Dk. Slaa
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alikuwa wa kwanza kuishushia lawama serikali, akidai kuwa hakuna mwaka ambao uendeshaji wa nchi ulikuwa wa kusuasua kama huu.

  Alisema hali hiyo ni ya hatari kwani serikali ilifika mahali ikakosa uamuzi katika masuala yanayohusu wananchi.


  "Katika historia ya nchi hii tangu tupate uhuru, haijawahi kuwapo kwa serikali iliyoonyesha udhaifu kama mwaka huu. Mawaziri wanagongana katika masuala ya msingi. Hii inaonyesha udhaifu na kutokuwapo kwa serikali," alisema.


  Alitolea mfano serikali kukwepa majukumu yake katika suala la kupanda kwa gharama za maisha na kusema imekuwa ikitumia kivuli cha kuwapo kwa mtikisiko wa uchumi duniani.


  "Nchi nyingine katika suala kama hili inatafuta suluhisho, lakini serikali yetu inatafuta visingizio na kujificha chini ya mwavuli wa dunia. Pia katika tatizo la umeme, badala ya kutafuta suluhisho inadai wao si Mungu hawawezi kuleta mvua.


  "Hali sasa imekuwa mbaya zaidi, sukari imefikia hadi sh 5,000. Tunarudi miaka ya nyuma ambako ilikuwa inapatikana kwa mgawo ambao nao unasababisha kuwapo kwa vitendo vya rushwa," alisema Dk. Slaa.


  Askofu Mkuu Ruwa'Ichi
  Naye Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Yuda Thadeus Ruwa'Ichi, alisema kuwa taifa lilipita katika hatua ngumu ya kiuchumi na kisiasa.

  Ruwa'Ichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, alisema uendeshaji wa serikali katika mambo mengi ulikuwa mgumu na uliyumbishwa kwa namna fulani kutokana na baadhi ya watendaji kuelekeza nguvu zao katika kinyang'anyiro cha urais wa mwaka 2015.


  Alisema badala ya serikali kukazania mambo ya msingi ya kitaifa, watendaji wake walielekeza nguvu zao katika msingi wa ubinafsi, makundi na kukosa upeo wa kuchukulia masuala kwa taswira pana yenye masilahi ya kitaifa.


  "Inashangaza kidogo kuona watu leo hii wanajenga makundi ndani ya vyama vyao kwa ajili ya kugombea urais mwaka 2015…hii ndiyo imezaa pia misingi ya udini na ukabila kama ambavyo wananchi walikuwa wanaaza kupotoshwa.

  Nawaomba wanasiasa kuangalia mbali ya siasa," alisema Askofu.


  Askofu Ruwa'ichi aliongeza kuwa changamoto hizo zitaondolewa ikiwa serikali itajipanga vema na kusimamia uwajibikaji wa kweli wa kila mtu kutimiza wajibu wake ipasavyo.


  Dk. Mokiwa: Hoja ya Katiba iliendeshwa vibaya
  Akizungumza na Tanzania Daima, Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa, alisema Serikali haikuwatendea haki Watanzania katika mambo mengi ya msingi.

  Dk. Mokiwa aligusia suala la mjadala wa Katiba kama moja ya mambo muhimu, mazito na ya msingi ambayo serikali iliyachukuliwa kwa namna inayotia shaka, wakati suala hilo ni zito kwa uhai wa taifa.


  Aliongeza kuwa viongozi wa juu wa serikali walilichukulia suala hilo kwa namna ya kishabiki zaidi na kwa msukumo wa kisiasa badala ya kuangalia kwanza masilahi ya nchi kwa vizazi vingi vijavyo.


  "Katiba ni suala zito na gumu, hivyo halikutakiwa kukingiwa kifua na mtu ama kulifanya kwa nia ya kumfurahisha wala kumkandamiza mwingine," alisema.


  Akizungumzia juu ya maafa yaliyolikumba taifa, Dk. Mokiwa alisema kama watendaji wakuu wa serikali wangesimamia kikamilifu wajibu wao, majanga makubwa ambayo yamelipata taifa yangeweza kuepukwa.


  Akifafanua zaidi, Dk. Mokiwa alitoa mfano wa ajali ya milipuko ya mabomu huko Gongolamboto na Mbagala kwamba yangeepukwa ikiwa kungekuwa na usimamizi na uangalizi makini kwa wahusika.


  "Hata mafuriko yasingefikia kiasi cha kuteketeza maisha ya wananchi kama kungekuwa na usimamizi mzuri wa watendaji katika miji, lakini kwa sababu ya rushwa na uzembe, leo tumewapoteza ndugu zetu" alisema Dk. Mokiwa.


  Uzembe mwingine alioutaja kiongozi huyo ni ule wa usimamizi mbovu katika sekta ya usafirishaji ambayo imesababisha barabara kugeuka kuwa machinjio ya wananchi.


  Alisema kuwa serikali makini na inayosimamia sheria kikamilifu, isingeweza kushuhudia wingi wa ajali za kila siku ambazo zimeteketeza maisha ya watu.


  Alishauri kuwa lazima sasa serikali ichukue maamuzi ya dhati ya kukomesha ajali nyingi ambazo alidai zinaepukika ikiwa watendaji katika sekta ya usafirishaji watakuwa makini.


  Alipendekeza kupiga marufuku magari yaliyochoka kutembea barabarani hasa yale ya abiria bila kujali yanamilikiwa na kigogo gani.


  "Napendekeza pia kuwanyang'anya leseni madereva wote ambao wamegundulika kutokuwa na uwezo kiakili wa kujali maisha ya watu, walevi, wahuni na wale ambao hawana uzoefu wa kutosha katika uendeshaji wa magari" alisema.


  Dk. Bana: Serikali ilijitahidi
  Mwenyekiti Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana alisema utendaji kazi wa serikali ulikuwa wa kiwango cha kati ingawa ulijitahidi kupanga vipaumbele vyake katika bajeti kuliko miaka mingine.

  Alisema changamoto iliyojitokeza ni tatizo la umeme ambalo lilitokana na serikali kutojipanga vizuri kulishughulikia ili kuwezesha uchumi wa nchi kuinuka.


  "Huduma za kijamii hazikuwa mbaya sana ikilinganishwa na bajeti zilizopita hasa katika sekta ya elimu afya na mengine" alisema.


  Aliisifu serikali kuwa sikivu hasa wananchi walipodai Katiba mpya, jambo ambalo alisema Kikwete alionyesha nia kwa wananchi wake kuipata.


  "Pamoja na suala hilo kushughulikiwa lakini kwa umoja na sauti moja za wananchi ziliifanya serikali kuandika upya muswada huo na kuupeleka tena bungeni.


  "Hilo lilikuwa ni jambo zuri kwamba wananchi wanaweza kuainisha chuya na mchele. Sote ni mashahidi kwamba uamsho wao uliwezesha muswada kuandikwa upya," alisema Dk. Bana.


  Nape Nnauye anena
  Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Nape Nnauye, alizungumza kwa kifupi alisema mwaka unaomalizika haukwenda vizuri.

  Bila kufafanua zaidi, Nape alisema kulikuwa na changamoto mbalimbali zilizoikabili serikali katika utendaji wake, lakini zilishughulikiwa kadiri ya uwezo wa watendaji.


  Hata hivyo, alishauri viongozi wa serikali kuzichukulia changamoto hizo na kuzifanyia kazi kwa mwaka ujao.

   
 2. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  "ilipwaya"... kwani sasa iko vipi??? msiume na kupuliza.
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Serikali inaendelea kupwaya na iko kwenye mtanziko usio na kifani. Utawala umezidi kuwa legelege na kukosa mustendi. Wanauza mafuta wanaigomea serikali, nayo inafyata mkia, inatangaza sukari ishushwe wafanya biashara wanapandisha halafu haichukui hatua.

  Mambo yanakwenda hobela hobela ki sege mnyege. Jamaa zetu nao wanazidi kuchukua chao mapema.
   
 4. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hata hawa nao wamepwaya mbona hawatoi nini kifanyike
   
 5. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Serikali ya jk ilichemka kwa 100% na kuivisha mambo yote, hakuna raha bali taabu tupu.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Huyu Bwana ni balaa kuu Eti anasema ''kwa watu wanao omba uwepo wa mgombea binafsi ni sawa na mtu anaye jaribu ujinga ''

  Hii ni kauli ya kiongozi wa juu sana ndani ya chama TAWALA chetu kupitia Star TV

   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  imevuka kabisa, aisee:A S embarassed:
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
  ....Serikali ya Kikwete imepwaya tangu alipoingia madarakani 2005. Katika miaka 6 aliyokaa madarakani sioni mafanikio yoyote yale ambayo Kikwete anastahili kusimama hadharani na kujisifia kwa kujipiga kifua, labda wamefanikia kuja na kauli nzuri kama (tumethubutu, tumeweza tunasonga mbele, ari mpya nguvu mpya na kasi mpya & Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana) lakini kauli zote hizi hazina mshiko wowote ule katika jamii ya Watanganyika.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mkuu BAK
  Amejitahidi kukpunguza kwa kiwango kikubwa ujambazi nchini
   
 10. j

  junior05 Senior Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi huyo dk Bana, haitokei akasema ukweli wa hali halisi sa anatetea nn, au ndo kuvbizia ubalozi au nafasi yoyote akimaliza utumishi wake
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  jhabari yoyote inayohusu serikali ikiandikwa na tz daima la mbowe usipoteze muda kuisoma mana ni uzushi mtupu..haitakaa itokee padre slaa amsemee kikwete in a positive way hata hao maaskof na mapadre wenzake
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  chadema pia ilipwaya sana.iliwadanganya watanzania kupinga posho huku kwny uhalisia wamekomba.ilikurupuka ikafukuza madiwani arusha sasa inajutia.ikakimbia bungeni ili ikanye juice ya ikulu
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  jhabari yoyote inayohusu serikali ikiandikwa na tz daima la mbowe usipoteze muda kuisoma mana ni uzushi mtupu..haitakaa itokee padre slaa amsemee kikwete in a positive way hata hao maaskof na mapadre wenzake
   
 14. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Na hii imekuwa mwaka mmoja tu baada ya uchaguzi hao watendaji wakuu wa serikali wanachofikiria ni Urais 2015 nani baada ya JMK sasa sijui hii miaka ijayo kama kutakuwa na utendaji wowote wa maana serkalini kwani ndo tunasogea 2015.I think wananchi inatupasa kufanya kitu hapa vinginevo zawadi kuu atakayotuachia Jakaya ni Machafuko ndani ya Tanganyika!
   
 15. a

  albert jr Member

  #15
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu acha ushabiki ucokua na mana!!andika habari yako uonekane wewe kweli ni great thinker,hivi kweli uisifie serikali ya kikwete kwa maisha haya ya sasa ya mtanzania?wake up 2jenge nchi na upya
   
Loading...