Kaka, kumbuka, mshikaji ana uraia wa Belgium.
DRC ilikuwa koloni ya Belgium. Leo hii, Belgium ni nchi inayotegemea DRC kwa kiasi kikubwa. Hivyo basi, atakaaje Belgium kama raia, ikiwa hajawatengenezea mazingira mazuri?
Pili, ujue rais kama rais, anakuwa na kamati ya uongozi. Ikibishia jambo fulani,yeye hana maamzi ya kupinga. Je, unadhani aachie mashariki tu hivi hivi?
Je, unadhani uwezo wa kurudisha eneo lile anao? Yote jibu ni hapana. Kikubwa ni kwamba maji yamemfika shingoni, hivyo anajaribu kuonyesha uwezo wake.
Sema tu, iwe Kabila, iwe jirani, wote wanajeshi. Unadhani ubavu wa kupambana nao anao? Pia,zingatia, ushawishi wa Kabila, ni mkubwa kuliko wa rais wa sasa.