Serikali ya CHADEMA ni kubwa mno!

Serikali ya CHADEMA ni kubwa mno!

Malafyale

Platinum Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
13,910
Reaction score
11,316
Hata kwenye kampeni za kugombea U-Rais mwaka jana,mgombea wa nafasi hiyo kupitia CHADEMA Dr Slaa alikuwa akitusisitizia umuhimu wa Tanzania kuwa na serikali ndogo isiyozidi mawaziri 15 na kwa kweli mm binafsi nilikubaliana na yeye kwani kama utakuwa na baraza dogo la mawaziri ni dhahiri utaokoa fedha nyingi sana za walala hoi kwenye mishahara na posho!

lkn mbowe juzi katangaza baraza la mawaziri kivuli lenye watu zaidi ya 24 na kupingana kabisa na ahadi zao za kampeni!kama tunailaumu CCM kwa mambo mengi ikiwemo ukubwa wa serikali yake,ni kwa nini CHADEMA wasingewaonyesha CCM kwa vitendo ni kiasi gani wapo makini kuokoa fedha za walipa kodi kwa kuunda serikali ndogo kama wakitwaa madaraka?

Je kwa serikali kubwa kivuli kama hii haitaingia akilini mwa wa Tanzania kuwa hata CHADEMA nao wakishinda U-Rais wataunda serikali kubwa kama CCM na kuzmidi kumtwika mzigo Mtanzania wa kawaida na hivyo kujipunguzia kura kwenye uchaguzi wa 2015?

Serikali kubwa kivuli ya CHADEMA ni hii hapa:

Msemaji ofisi ya Raisi: Freeman Mbowe,
Msaidizi: Silinde David
Uwekezaji na Uwezeshaji: Matiko
Ofisi ya Waziri Mkuu: Vicent Kiboko
Ofisi ya Raisi: Said
Ofisi ya Raisi & Utawala Bora: Mch Nakse wa Karatu
Ofisi ya Makamu wa Raisi: Gekulu
Ofisi ya Raisi & Mazingira: Leticia Nyerere
OFisi ya Fedha: Zitto Kabwe Msaidizi: Christina Lissu
Mambo ya Ndani: Lema
Katiba ya Sheria: Tindu Lissu
Kimataifa: Wenje
Jeshi la Ulinzi: Seladhini
Mawasiliano: prof Kayili
Makazi: Mdee
Maliasili: Mch Peter Msigwa
Nishat na Madini: Mnyika
Ujenzi: Machemli
Uchukuzi: Mhonga Said
Viwanda: Olenywa
Elimu na Mfunzo: Mtinda
Afya: Dr Gilbert Mbasa
Maendeleo ya Jamii: Naomi Kaiula
Vijana na michezo: Mbilinyi Mr Two
Kilimo: Meshack Obulugwa
Maji: Haines Kiwia
 
Mkuu sijui kama unaelewa maana ya serikali kivuli, hayo majina na wizara yanaendana na wizara alozitangaza kikwete kila waziri anakuwa na waziri kivuli wala si kwamba wakiingia madarakani watafanya hivyo. Fuatilia kama kuna wizara ambayo ni tofauti na ile ya kikwete!
 
Mkuu Malafyale, ni kubwa ukiilinganisha na ipi??? Sababu kwanza hao walotajwa ni nusu ya wanaowasimamia!!!
 
ungejijuza kwanza maana ya serikali kivuli ni nini.
 
Mkuu sijui kama unaelewa maana ya serikali kivuli, hayo majina na wizara yanaendana na wizara alozitangaza kikwete kila waziri anakuwa na waziri kivuli wala si kwamba wakiingia madarakani watafanya hivyo. Fuatilia kama kuna wizara ambayo ni tofauti na ile ya kikwete!

If so,mbona hamna serikali kivuli ya wizara nyingi tu nikianzia ya jumuia ya africa mashariki inayoongozwa na mzee samwel sitta?
 
hicho ni kivuli cha kikwete kama huelewi.wapeni chadema madaraka muone kazi kwa vitendo.
 
Ni kweli ni kubwa lakini ni kwa sababu mbili

1. Ya kwanza ni kwasababu unatakiwa kuchagua watu wakusimamia kila wizara. hivyo kama wizara kubwa vilevile serikali kivuli itakuwa kubwa.
2. Haina Gharama: Hawa jamaa ni wabunge hivyo hawalipwi kwa kuwa Mawaziri vivuli!! hivyo haiongezei gharama serikali hata shillingi moja.
 
Wasi wasi wangu na hasa kama Mbowe anaruhusiwa kuunda serikali kivuli aitakayo yeye kikatiba;je isingekuwa vyema kuunda serikali ndogo kivuli ili mwaka 2015 watumie kama case study kuwaeleza wa Tanzania ni jinsi gani wapo serious kwenye kuokoa fedha za umma?
 
Nadhani mkuu Malafyale amesukumwa zaidi na ushabiki katika kuandika malalamiko yake hapa. Kuna mambo mengi hakujiuliza kabla ya kuandika. Pole mkuu.
 
Wasi wasi wangu na hasa kama Mbowe anaruhusiwa kuunda serikali kivuli aitakayo yeye kikatiba;je isingekuwa vyema kuunda serikali ndogo kivuli ili mwaka 2015 watumie kama case study kuwaeleza wa Tanzania ni jinsi gani wapo serious kwenye kuokoa fedha za umma?

Oya mbona watu wanakueleza huelewi? Kivuli ni reflection ya halisi, ya Africa mashariki ipo covered kwenye mambo ya nje. Sio unakurupuka tu kishabiki halafu hutaki kuzielewa comments. Acha uvivu wa kufikiri!!
 
Gazeti la tanzania daima limeandika hivi

"Akitumia kanuni ya 14 (2) toleo la mwaka 2007 Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alitangaza baraza dogo kivuli lenye Mawaziri na Manaibu 26 na kusema wametekeleza ahadi ya kuundwa kwa baraza dogo kama ilivyo kwenye ilani ya chama chao".

"Kanuni hiyo inaeleza kwamba ‘Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni atateua wabunge wa chama chake au wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambao watakua wasemaji wakuu wa kambi ya upinzani kwa wizara zilizopo za serikali"
"Idadi ya Mawaziri na Manaibu Mawziri wa serikali ni 50 uteuzi wangu umezingatia hilo na kuwateua wasemaji wakuu na manaibu wao wasiozidi 29 ili kuishi kivitendo; kilio chetu cha muda mrefu cha kuwa na baraza dogo la mawaziri… natambua uwezo mzuri wa waheshimiwa wabunge wetu lakini ni vema kutenda tunayohubiri," alisema Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai"(mwisho wa kunukuu)

kikatiba kiongozi Mkuu wa Upinzani Bungeni anaweza kuunda serikali kivuli kwa jinsi anavyoona yeye na chama chake inafaa;kwa hiyo madai kuwa Serikali kivuli lzm i-reflect ilivyo serikali halisi hazina msingi wowote!

ingawaje Mbowe kasisitiza kuwa kaunda serikali ndogo lkn kwangu bado watu 26 ni wengi sana,angepunguza hadi at least 15-20!
 
Mkuu sijui kama unaelewa maana ya serikali kivuli, hayo majina na wizara yanaendana na wizara alozitangaza kikwete kila waziri anakuwa na waziri kivuli wala si kwamba wakiingia madarakani watafanya hivyo. Fuatilia kama kuna wizara ambayo ni tofauti na ile ya kikwete!

Wengine uwezo wao wa analysis of issues ni questionable and leaves a lot to be explained. Mtoa mada ni mmoja wao!
 
Gazeti la tanzania daima limeandika hivi

"Akitumia kanuni ya 14 (2) toleo la mwaka 2007 Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alitangaza baraza dogo kivuli lenye Mawaziri na Manaibu 26 na kusema wametekeleza ahadi ya kuundwa kwa baraza dogo kama ilivyo kwenye ilani ya chama chao".

"Kanuni hiyo inaeleza kwamba ‘Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni atateua wabunge wa chama chake au wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambao watakua wasemaji wakuu wa kambi ya upinzani kwa wizara zilizopo za serikali"
"Idadi ya Mawaziri na Manaibu Mawziri wa serikali ni 50 uteuzi wangu umezingatia hilo na kuwateua wasemaji wakuu na manaibu wao wasiozidi 29 ili kuishi kivitendo; kilio chetu cha muda mrefu cha kuwa na baraza dogo la mawaziri… natambua uwezo mzuri wa waheshimiwa wabunge wetu lakini ni vema kutenda tunayohubiri," alisema Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai"(mwisho wa kunukuu)

kikatiba kiongozi Mkuu wa Upinzani Bungeni anaweza kuunda serikali kivuli kwa jinsi anavyoona yeye na chama chake inafaa;kwa hiyo madai kuwa Serikali kivuli lzm i-reflect ilivyo serikali halisi hazina msingi wowote!

ingawaje Mbowe kasisitiza kuwa kaunda serikali ndogo lkn kwangu bado watu 26 ni wengi sana,angepunguza hadi at least 15-20!

Kwani ni nini maana ya kivuli? Je, Unaweza kuwa na kivuli bila object?
 
Kama ingewezekana kwa serikali ya CDM kufanya shughuli zote zinazofanywa na serikali kwa mawaziri 15 sasa hao vivuli wanashindwa nini kufanya hizo shughuli zinazofanywa na baraza la CCM. Ningetemea kwa kuwa hao mawaziri ni vivuli tu, CDM ingekuwa nao hata watano tu kuwakilisha wote 40 plus wa CCM ili waishi wanayoyasema.
 
Wengine uwezo wao wa analysis of issues ni questionable and leaves a lot to be explained. Mtoa mada ni mmoja wao!

Tumia kila aina ya maneno ya hovyo hovyo unayo yaona yanakufaa wewe;lkn ukweli unabaki pale pale kuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani Bungeni akishauliana na chama chake anaruhusiwa kikatiba kuunda serikali kivuli kwa jinsi atakavyo na ndiyo maana hapo juu Mbowe kasema kuwa katekeleza ilani ya CHADEMA kwa kuunda serikali ndogo yenye mawaziri 26 mbayo mm bado nailalamikia kuwa ni kubwa sana!

CHADEMA itajengwa kwa kukosolewa wala siyo kwa siasa za "ndiyo mzee"
 
If so,mbona hamna serikali kivuli ya wizara nyingi tu nikianzia ya jumuia ya africa mashariki inayoongozwa na mzee samwel sitta?

Afrika Mashariki nayo ipo. Wewe umeorodhesha wizara 26 wakati wao wana wizara 29 ina maana umeacha wizara 3
 
Kwani ni nini maana ya kivuli? Je, Unaweza kuwa na kivuli bila object?

Gad oneya;

CHADEMA walipaswa kuzichanganya baadhi ya wizara pamoja na kupata wizara si zaidi ya 20 then wakati wa kujibu bajeti ya serikali waziri mmoja kivuli anajibu wizara lets say 2;vile wa Tanzania watakuwa wanafuatilia mambo haya wataishangaa CCM kwa baraza lao kubwa la mawaziri ili hali CHADEMA wakiwa na baraza dogo tu wameweza kujibu hoja na pengine hata kuleta ushauri wa jinsi gani mawaziri wa CCM waendeshe wizara zao efficiently!

Nina imani kuwa CHADEMA wangepata political scores kama wangeunda baraza dogo kivuli la mawaziri!
 
Afrika Mashariki nayo ipo. Wewe umeorodhesha wizara 26 wakati wao wana wizara 29 ina maana umeacha wizara 3

Afrika Mashariki is just like a department in the foreign affairs and international cooperation!
 
Ugonile malafyale? Twa mbombo? Naona ndugu yangu malafyale una wivu wenzio wakitawala kwa kuwa jina lako lina maanisha mtawala. Kama huelewi maana ya kivuli pole sana, kesho jua likiwaka angalia kivuli cha jua.
 
CHADEMA itajengwa kwa kukosolewa wala siyo kwa siasa za "ndiyo mzee"

Kwa hapa JF hii ni totally the opposite, nadhani iliuonekane ni mpiganaji ni lazima uunge mkono hata madudu ya viongozi wetu, huwa naogopa sana aina ya demokrasia inayojengwa humu.
 
Back
Top Bottom