hata kwenye kampeni za kugombea u-rais mwaka jana,mgombea wa nafasi hiyo kupitia chadema dr slaa alikuwa akitusisitizia umuhimu wa tanzania kuwa na serikali ndogo isiyozidi mawaziri 15 na kwa kweli mm binafsi nilikubaliana na yeye kwani kama utakuwa na baraza dogo la mawaziri ni dhahiri utaokoa fedha nyingi sana za walala hoi kwenye mishahara na posho!
Lkn mbowe juzi katangaza baraza la mawaziri kivuli lenye watu zaidi ya 24 na kupingana kabisa na ahadi zao za kampeni!kama tunailaumu ccm kwa mambo mengi ikiwemo ukubwa wa serikali yake,ni kwa nini chadema wasingewaonyesha ccm kwa vitendo ni kiasi gani wapo makini kuokoa fedha za walipa kodi kwa kuunda serikali ndogo kama wakitwaa madaraka?
Je kwa serikali kubwa kivuli kama hii haitaingia akilini mwa wa tanzania kuwa hata chadema nao wakishinda u-rais wataunda serikali kubwa kama ccm na kuzmidi kumtwika mzigo mtanzania wa kawaida na hivyo kujipunguzia kura kwenye uchaguzi wa 2015?
Serikali kubwa kivuli ya chadema ni hii hapa:
Msemaji ofisi ya raisi: Freeman mbowe,
msaidizi: Silinde david
uwekezaji na uwezeshaji: Matiko
ofisi ya waziri mkuu: Vicent kiboko
ofisi ya raisi: Said
ofisi ya raisi & utawala bora: Mch nakse wa karatu
ofisi ya makamu wa raisi: Gekulu
ofisi ya raisi & mazingira: Leticia nyerere
ofisi ya fedha: Zitto kabwe msaidizi: Christina lissu
mambo ya ndani: Lema
katiba ya sheria: Tindu lissu
kimataifa: Wenje
jeshi la ulinzi: Seladhini
mawasiliano: Prof kayili
makazi: Mdee
maliasili: Mch peter msigwa
nishat na madini: Mnyika
ujenzi: Machemli
uchukuzi: Mhonga said
viwanda: Olenywa
elimu na mfunzo: Mtinda
afya: Dr gilbert mbasa
maendeleo ya jamii: Naomi kaiula
vijana na michezo: Mbilinyi mr two
kilimo: Meshack obulugwa
maji: Haines kiwia