Serikali ya CCM itekeleze ilani yake ya uchaguzi ya kuanzia 2015/2025 juu ya umeme

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
ILANI YA CCM 2015-2020
Kupunguza gharama za kuunganisha umeme vijijini kutoka TSH 454,000 mpaka TSH 27,000

ILANI YA CCM 2020-2025
63(h) kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme na wa gharama nafuu.

Serikali ya CCM imetekeleza ilani yake kwa %ngapi? Jana nimeona mojawapo ya mitambo ya gesi asilia imewashwa ili kuongeza megawatt 185 kwenye grid ya Taifa ni hatua nzuri.

Katika bajeti iliyopitishwa na wizara husika bungeni 2022/2023 inaonyesha idadi ya meter za kufunga umeme majumbani ni meter 700,000 kwa nchi nzima. Ukizigawanya kwa mikoa, Wilaya, kata hadi zifike vitongojini zitafika kama 200 kwenye kitongoji ambazo ni chache sana ukilinganisha na wananchi ambao hawajaunganishiwa umeme na wanahitaji kuunganishiwa umeme.

Rai yangu ya kumaliza hii kero, mkopo tuliopewa wa trillion 2.4 ungeunganishia wananchi umeme ambao hata maeneo mengine utasaidia kuvuta maji ardhini kwa ajili ya matumizi mbalimbali, kama ule mkopo wa awali ulivyotumika kujenga miundo mbinu ya madarasa.

Naomba kuwasilisha.
FB_IMG_1655474509613.jpg
 
Back
Top Bottom