Serikali ya CCM isiwatumie wajinga na wapumbavu kwenye mambo muhimu

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
.

Mwaka 2019 nilikishauri CHAMA changu-CCM kuacha kuwatumia watu wajinga katika mambo makubwa na ya muhimu. Niliwaambia, kazi aliyopewa Cyprian Musiba ni kazi nzuri na ya muhimu lakini kwa sababu imepewa mtu mjinga itaharibiwa vibaya na kugeuka sumu. Kazi ya kukitenganisha Chama na mtandao wa mabepari ilikua kazi ya muhimu sana kufanywa na mtu mwenye akili na hadhari kubwa. Ni bahati mbaya sana kwamba CCM mpya haikunisikiliza, leo Cyprian Musiba analia, CCM tunalia. Wote tunalia kwa sababu ya matokeo ya ujinga wa Cyprian.

Ni kama PEPO lilelile limerudi tena ndani ya Serikali ya CCM. Maajabu ya CCM ni kwamba, inafundisha watu halafu haiwatumii. Inatumia watu isiowafundisha halafu wanaharibu. Kosa hili limekuwa likiendelea kila kukicha bila kukoma. Well, unaweza ukauliza; inawezekanaje CCM ifundishe watu halafu isiwatumie itumie isiowafundisha? Jibu ni rahisi, mtu aliyefundishwa anatumwa ndani ya utaratibu. Ukimtuma kazi yako inaishia hapo, mtu aliyefuzu mafunzo vizuri hafundishwi kazi katikati ya kazi kwa sababu ni rahisi kuharibu kazi. Mtu asiyefundishwa, anatumwa vyovyote hata nje ya utaratibu wa kazi. Hashauri wa kukataa mambo yenye kuweza kuharibu kazi. Bahati mbaya CCM inapenda kutuma watu nje ya utaratibu!!

Kama ilivyokuwa wakati wa Cyprian Musiba wakati huu kazi kubwa za muhimu zimepewa mjinga mwingine. Huyu wa sasa anaitwa Stive Nyerere. Yamkinika, huyu ni mjinga kuliko Cyprian Musiba. Inavyoonekana, Stive Nyerere ametumwa kufanya kazi tatu. MOSI. Kuzuia watu wasifikirie Urais wa 2025, PILI. Kuzuia watu wasifikirie madai ya Katiba mpya na, TATU. Kushawishi watu kuchanja J&J. Kazi zote hizi ni za muhimu lakini zimepewa mtu mjinga, matokeo yake zote zitaharibika na kugeuka sumu.

1. Kazi ya kwanza ya kuzuia watu kufikiria Urais wa 2025 imeharibika tayari. Njia anayoitumia Stive inavunja Katiba ya CCM na Katiba ya nchi. Kusema anawaonya watu wenye kufikiria Urais katika CCM ni sawa na kusema kuwa anawaonya watu kufikiria kutumia HAKI yao ya msingi ndani ya CCM, kuchagua na kuchaguliwa. Watu wenye akili watampuuza, watamcheka halafu wataongeza speed.

Kama hiyo haitoshi, Stive amepiga marufuku watu wa CCM kufikiria kuanzisha Chama kingine cha Siasa. Huu ujinga hata Msajili wa Vyama vya Siasa hawezi kuufanya. Hii ndio hasara ya kuwatumia watu wajinga katika mambo makubwa. Kwa kifupi, kauli za Stive zikiendelea zinakwenda kuigawa CCM kabla ya mwaka 2025. Stive haelewi hali ya CCM ilivyo kwa sasa!!

2. Kuhusu Katiba mpya nadhani sipaswi kuongea zaidi. Watu wenye akili hawawezi kumsikiliza mtu mwenye kupinga madai ya Katiba mpya bila kuwapa sababu. Sababu anayoitumia Stive ya kujenga uchumi haina maana yoyote. Uchumi wa nchi sio sababu ya wenye madai ya Katiba mpya. Mtu ana madai yake na wewe unampatia madai yako wapi na wapi? Kwa vyovyote hawezi kukusikiliza. Stive awaambie udhaifu wa madai yao ya Katiba mpya, hiyo ndio hoja yao. Ni bahati mbaya kwamba uwezo huo hana na hawezi kuupata. Hii ndio hasara ya kutuma vilaza kwenye mambo makubwa na muhimu.

3. Kuhusu CHANJO. Nchi yetu imebarikiwa kuwa na Mawaziri wajinga-wajinga sana. Mawaziri wetu hawawezi kutofautisha mambo ya umaarufu na utaalam. Waziri mmoja kwa ujinga wake aliwateua Hamisa Mobeto, Mbwana Samatta na Eddo Kumwembe kuwa mabalozi wa elimu ya KODI nchini. Kwamba watu wasiofahamu lolote kuhusu kodi wakafundishe watu umuhimu wa kulipa kodi. Ni miezi miwili sasa mabalozi hawajulikani waliko na kodi inakwepwa kama kawaida.

Ujinga huohuo umehamishiwa kwenye jambo la Afya za watu. Unamtuma Stive Nyerere anishawishi MIMI kuchanja J&J wakati hana elimu yoyote ya utabibu. Mimi nisiyetaka kuchanja kwa sababu sijafahamu uhakika wa usalama wa J&J kwa miaka mitano au kumi ijayo kwa kuwa hakuna utafiti wa kutosha Stive atawezaje kunishawishi Mimi nisiyetaka kuchanja kwa sababu Serikali haitaki kubeba mzigo wa matokeo ya chanjo kwangu Stive anawezaje kunishawishi nichanje? Nadhani huu ni mzaha katika afya za watu. Kuna tofauti kubwa kati ya kushawishi watu na kuchekesha watu. Watu walioshindwa kumuelewa Waziri wa Afya na Naibu wake ambao ni wataalam wa afya hawawezi kumuelewa mtu mwenye kashfa ya kula rambirambi katika misiba.

Mambo makubwa ya muhimu namna hii katika nchi yote yanakwenda kuanguka kwa sababu amepatiwa mtu mjinga kuyawezesha. Matokeo yake vita ya Urais itakolea ndani ya CCM kwa kauli za Stive, madai ya Katiba mpya yataendelea na yatapanda thamani zaidi kwa sababu ya kauli za akina Stive na CHANJO itakosa wateja kabisa kwa sababu ya ujinga wa Stive Nyerere. Badala ya kushawishi watu yeye anafarakanisha watu. CCM ikiendelea kuwatumia watu wajinga katika mambo makubwa na muhimu namna hii, ijiandae kuanguka katika kila jambo. Ushauri wangu, Stive Nyerere, Kihongos na wenzao wapewe mambo yenye kulingana na vimo vyao. Majuto ni mjukuu!!
Inatafakarisha Sana
 
Kihongosi kuwa katibu mkuu umoja wa vijana hapo kweli CCM yetu ilibugi Sana .Huyu kada hana hekima yeye anaamini katika ubabe kitu ambacho kwa siasa za wakati huu hazijengi .Hiyo nafasi anatakiwa mtu mwenye nguvu ya ushawishi wa kihoja ili kuwavuta watu.
 
kijani tunapenda mambo makini na ya uhakika lakini hatutaki kutenda kwa umakini na uhakika hapo ndipo tabu ilipo sasa
 
Mkuu vigezo vya Mtu kua Mjinga na Vipi? Nami Nijipambanue Kama Nipo Kundi La Wajinga au Lah!.
 
Hivi kwa nini kiongozi akiwa hajui kitu huchagua magarasa? A.k.a majokeri
 
Toka lini ccm wakatumia wenye akili,angalia prof kabudi,prof ndalichako,prof kitila,dk gwajima wote watu wa hovyo hovyo tu...Steve,Gwajima,Lusinde,Msukuma,Dk Gwajima wote hawa elimu yao ni sawa, CCM imejaa vichaa sema hawajuani
 
Hongera umetoa ushauri mzuri kwa chama chako, ingawa hakuna mtu mwerevu atakayekubali kutumika kwenye Mambo ya kijinga
 
Ni maoni mazuri sana kwa chama chako, lakini hakuna mtu mwerevu atakubali kutumiwa kwenye Mambo ya kijinga
 
Badala ya kuwatukana na kuwadhalilisha watu ambao hawakujiteua wenyewe, sifa hizo ungewapa wateuaji na taasisi zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom