Serikali ya CCM inaongozwa na Chadema's Think Tanks | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya CCM inaongozwa na Chadema's Think Tanks

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 18, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wananchi wengi hivi sasa wameamini kuwa Chadema ni majembe na kwa asilimia kubwa wanaiongoza nchi bila kuwapo ikulu. Haya yamedhihirika kutokana na mambo kadha wa kadha ambayo Chadema iliyaamini,iliyahubiri, iliyatete na kuyasimamia. Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo: -

  1. Kuanzisha mchakato wa Katiba mpya
  Katika Ilani ya uchaguzi ya CDM 2010 suala la Katiba mpya lilikuwepo wakati katika Ilani ya CCM suala hili halikuzungumziwa, hivyo kutokana na ushawishi, ubunifu na upeo mkubwa wa CDM, Serikali ya CCM ikaona iibebe hoja hiyo kwa shingo upande na kuitekeleza.

  2. Kurudishwa Bungeni sheria ya kusimamia uundwaji wa Katiba mpya
  Hili ndilo limefurahisha watu wengi sana kwani wabunge wa CDM kwa uchache wao walipinga muswada husika hadi dakika ya mwisho na hata kutoka bungeni lakini wabunge wa CCM walipitisha muswada huo mbovu na hatimaye Rais akausaini ukawa Sheria. CDM na wanaharakati wengine wakamshawishi Rais naye akaridhia kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na wabunge wa CCM kuwa ni mbovu na hivyo Rais akairudisha tena Sheria hiyo Bungeni ili ifumuliwe na kuingiza mapendekezo yaliyoletwa na wapinzani hususan CHADEMA pamoja na wanaharakati wengine. Kimsingi, Suala hili limewashushia hadhi sana sana wabunge wa CCM ambao walionekana kama wanafki wakati wa kuijadili sheria hiyo mara ya pili, kwa kweli Shame on them.

  3. Suala la Posho
  Katika vikao vya bunge baada ya uchaguzi 2010 suala la kuwapo kwa posho za vikao (Sitting Allowance) lilipingwa vikali na wabunge wa CDM huku Wabunge wa CCM wakizitetea vikali posho hizo na hata kubeza wabunge wa CDM wanaozipinga posho hizo. Sakata hili la Posho hizo lilichukua sura mpya baada ya mihimili mikuu ya serikali kutoa kauli tata tena zisizo na aibu wala hekima pale Waziri Mkuu na Spika wa Bunge walipotudanganya kuwa Rais kazipitisha. Baada ya Rais kusema kuwa hajazipitisha wote waliotudanganya wamenywea na sasa mkakati unaoendelea ni kuzifuta kabisa posho hizo kama ambavyo Chadema walishauri kwa mara ya kwanza.

  4. Suala la Ufisadi

  Chadema ilikuwa ya kwanza kutaja orodha ya Mafisadi, na kusimamia kidete suala la ufisadi. Tunakumbuka jinsi Chadema ilivyovumbua ufisadi wa Richmond, EPA etc, serikali ikapinga sana hoja hiyo lakini mwisho wa siku Serikali ya CCM walikubali na kutekeleza kile Chadema ilichotaka ingawa sio kwa ufanisi. Aidha, Serikali ya CCM ikadandia hoja kama kawaida yao na walienda mbali kwa kuanzisha kampeni ya kujivua gamba, kampeni ambayo ilionekana kama ingetekelezwa kama ilivyokusudiwa huenda CCM kingeparaganyika maana unahitaji darubini kali kumtafuta kiongozi wa CCM asiye na doa la ufisadi. Kimsingi kila kiongoz wa CCM anadhohofisha chama kwa namna moja au nyingine.

  Mambo haya manne yananifundisha kuwa CCM kimechoka kimawazo, kifikra na hata kimvuto hivyo kinahitaji kusaidiwa sana sana mana tusipowasaidia nchi yetu ndio inazama. Wabunge wa CCM wamejisahau kama wapo bungeni kuwatetea wananchi, badala yake wamejikita katika kutetea maslahi ya chama kama Makatibu waenezi badala ya kutetea maslahi ya wananchi waliowachagua na kuwatuma Bungeni.

  Aidha, navishauri vyama vya siasa hususan Chadema kutumia nafasi hii kuwaandaa wapiga kura wapya wa 2015 mana CCM kurudi madarakani tena kwa kweli itakilazimu kuiba kura tu kwani kimepoteza sifa ya kushika dora na hata mvuto katika jamii. Raia wema wanaona CCM kuwa ndicho chanzo cha umaskini wetu, wananchi wana hasira na uzalendo umewatoka.

  Kwa ujumla CCM kimechoka kinahitaji kuondolewa mana hata kiking'ang'ania kama kilivyofanya 2010 hakiwezi kututoa hapa tulipo. CDM inabidi kiicharge Serikali ya CCM consultation fee mana serikali yetu inasaidiwa kufikiria na CDM.
   
 2. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hongera kwa uchambuzi yakinifu......... Ila duh! Haulali?!
   
 3. D

  Dik JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivi washauri wa jk huwa wanafanya kazi gn?jk anahtj wabung w ccm mmuongoze lkn cha ajabu anashauriwa na chdm!nyie hamuyaoni haya?hii nchi n yetu sote na hata std seven anaona ****** unaofanywa na ccm.nawashauri msimame kwny haki na mumshauri jk ipasavyo na kuacha ushabik usio na tija
   
 4. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Mkuu huo ndo ukweli,CCM kushney,CCM wapo ikulu ila CHADEMA wapo mioyoni mwa watanzania walio wengi.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki CHADEMA.
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mimi nawashauri washauri wa JK hata kama wana cognitive ndogo, basi wawe wanachama wa JF
  kwani humu watachota hekima at ZERO COST na kwa kutumia hizo cognitive ndogo walizanazo
  ku-improve kutoa ushauri MAKINI kwa JK. Ingawa JKnaye hatakiwa kwa mfano kusubiri ushari wa
  kufuta posho za vikao, kupunguza safari za nje wakati huu ambao SERIKALI inanuka UKATA. Unless na
  yeye huko upstair there is something wrong!
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  hana mshauri kwa sasa,hii ni tangu shehe yahaya afariki!
   
 7. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nashkuru ni mapenzi na Taifa langu yanayonifanya nisipate usingizi. Yaani usiku silali na nikilala naiota Tanzania.
   
 8. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  You are very right, JK anapitia kipindi kigumu ktk uongozi wake kwa kumpoteza Mnajimu aliyekuwa akimpa ushauri wa majini na nguvu za giza.
   
Loading...