Serikali Ya Belarus yauwekea vikwazo Umoja wa Ulaya

Serikali Ya Belarus yauwekea vikwazo Umoja wa Ulaya

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,285
Reaction score
9,337
Belarus leo imesema kuwa inauwekea Umoja wa Ulaya vikwazo kama jawabu la umoja huo kuwawekea vikwazo maafisa wake kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata uliompa tena ushindi rais Alexander Lukashenko.

Mapema Ijumaa, viongozi wa Umoja wa Ulaya waliidhinisha vikwazo vya usafiri na kushikiliwa kwa mali za maafisa 40 wa serikali ya Belarus ambao wanasema walihusika katika wizi wa kura kwenye uchaguzi huo wa Agosti 9 na pia katika kuwashambulia waandamanaji waliokuwa wanapinga uchaguzi huo.

Angela Merkel ni Kansela wa Ujerumani na kiongozi wa baraza la Ulaya kwa wakati huu."Tunaweza kusema leo kwamba vikwazo dhidi ya wahusika Belarus vitakuwa na tija, hii inamaanisha kwamba Umoja wa Ulaya unawachukulia hatua wale wanaopinga demokrasia na nafikiri hii ni ishara muhimu sana.

"Uingereza na Canada tayari zimeshawawekea vikwazo maafisa wa Belarus ila Umoja wa Ulaya haujamuwekea vikwazo Rais Alexander Lukashenko mwenyewe.
 
Hii akili ya ajabu hiyo serikali ya Belarus itakuwa imejifunza mahala fulani kwa serikali fulani ya ajabu yenye kiongozi wa ajabu iliyopo ninapoandika hii comment.
 
Ukiwa Mzalendo kulinda raslimali za Nchi Mabeberu yanakuita dikteta

Ila ukiahidi kuwapa raslimali wanakuita rafiki
Kwanini mataga mnawaunga mkono madikteta na wezi wa kura popote duniani?
 
Ukiwa Mzalendo kulinda raslimali za Nchi Mabeberu yanakuita dikteta

Ila ukiahidi kuwapa raslimali wanakuita rafiki
Kwanini mnaunga mkono wizi wa kura?Nyerere japo aligoma kuachia rasilimali alikuwa rafiki mkubwa wa mataifa ya Ulaya na Marekani!
Na Nyerere alikuwa mzalendo kweli kweli!
 
Na sisi bado siku chache tu kuungana na hiyo nchi ya Belarus kuwekewa vikwazo. Kwa namna ccm inavyo lazimisha ushindi hata kwa bao la mkono, sidhani kama Mabeberu wataendelea kuuvumilia huu uhuni.
 
Sasa hawa Chadema ndio washinde Urais ? Ambao hawana hata uwezo wa kupata wabunge watatu

Vijana wa Chadema mtaokota makopo huu mwaka
Na sisi bado siku chache tu kuungana na hiyo nchi ya Belarus kuwekewa vikwazo. Kwa namna ccm inavyo lazimisha ushindi hata kwa bao la mkono, sidhani kama Mabeberu wataendelea kuuvumilia huu uhuni.
 
Marafiki wa kweli duniani ni china na urusi tu

Waafrika tuachane na ulaya na USA
Kama tuna taka maendeleo . malafiki wa kweli ni US na ulaya wote walio wafata wapo mbali kiuchumi pia waliwezeshwa na hao jamaa hapo juu.
Kuna jamaa alindika ili tuweze kufika mbali ni lazima kuwa chukulia kama wadau wa maendeleo si mabeberu.
 
Hayo yatatuletea Ushoga
Kama tuna taka maendeleo . malafiki wa kweli ni US na ulaya wote walio wafata wapo mbali kiuchumi pia waliwezeshwa na hao jamaa hapo juu.
Kuna jamaa alindika ili tuweze kufika mbali ni lazima kuwa chukulia kama wadau wa maendeleo si mabeberu.
 
Sasa hawa Chadema ndio washinde Urais ? Ambao hawana hata uwezo wa kupata wabunge watatu

Vijana wa Chadema mtaokota makopo huu mwaka

Usisahau tu mwaka huu mabeberu wamewakalia kooni hivyo ile janja janja yenu ya kuiba kura, haitakuwepo. Kitendo cha kuwajaza makada kwenye ile tume yenu mbovu hakitawaokoa kamwe! Sasa wewe jipe tu moyo.

Mgombea wako hali ni mbaya kutokana na pumzi yake kukata mara kwa mara, ila wewe unajifanya bado ni jasiri huku ukiufahamu ukweli. Tutaona nani atakaye okota hayo makopo. Hamtakuja kumsahau Lissu enyi maccm mlio laaniwa.
 
Sasa hawa Chadema ndio washinde Urais ? Ambao hawana hata uwezo wa kupata wabunge watatu

Vijana wa Chadema mtaokota makopo huu mwaka
Binafsi nimependa uamuzi wa huyo Rais wa nchi hiyo. Mambo mengine yanasumbua sana. Uingereze imechemka Umoja wa Ulaya, alafu wajifanye wana demokrasis , wapi na wapi? Uturuki iko hapo inasumbua Syria/ Yemen lakini haifanyiwi kitu cho chote!
 
Wazungu ni wanafiki, mwisho wao unakaribia
Binafsi nimependa uamuzi wa huyo Rais wa nchi hiyo. Mambo mengine yanasumbua sana. Uingereze imechemka Umoja wa Ulaya, alafu wajifanye wana demokrasis , wapi na wapi? Uturuki iko hapo inasumbua Syria/ Yemen lakini haifanyiwi kitu cho chote!
 
Kama kuna Bngo bahati mbaya basi hata ulaya bahati mbaya pia ipo.
 
Back
Top Bottom