Serikali ya Awamu ya Tano na kilimo

Bwana Mpanzi

Senior Member
Jun 28, 2019
180
165
Habarini za leo Wanajamvi?

Poleni kwa majukumu, labda niende kwenye lengo langu.

Zimepita awamu nyingi kilimo kilikuwa kinachukuliwa kwa mtazamo mkubwa mmoja yaani wasio au kwa ajili ya walala hoi lakini hii Awamu imebadilika maana kila mtu kwa sasa ana zao lake na analiita zao la ndoto.

Kwa maana idadi ya wasomi na wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo wanazidi kumiminika mashambani kila siku na wanapambana haswa haswa ili kuhakikisha mkono unaenda kinywani. Hakuna masuala ya kilimo kwa wajinga au wasio na Uwezo tena . Ila kwa ufupi wa hii zamu ni kuwa kuna mazao hayajafanya poa sana na kufanya wananchi wa maeneo hayo wanajutia na wanalalama mfano nyakati tofauti wadau wa kahawa wamelalama sana na korosho na kulaumu bodi zao.

Kuna mazao yamefanya vizuri na kuwa maarufu mfano Parachichi kwa nyanda za juu kusini kwa kuwepo soko la kuaminika.

Sasa tubadilishane mawazo hapa zao lipi lilikusaliti sokoni au shambani na sababu ni nini?

Kwa wale walioshauriwa kuingia shamba unadhani mshauri wako au mentor wako alikushauri vizuri au alikuuza?

Na wale walio njia panda wanaogopa kubet nao wanasemaje?

FB_IMG_1608181859538.jpeg
 
Hakuna msaada wowote kutoka serikalini, mafanikio ya kilimo cha parachichi nyanda za juu kusini ni kutokana na juhudi binafsi za mkulima na makampuni ya ununuzi 100%
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom