Serikali ya awamu ya tano imegeuka kuwa msaliti kwa uchumi wa nchi yetu

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Wakati wanaingia marakani walikuja na kauli mbiu ya hapa kazi tu, na tukaji aminsha kuwa wachapa kazi wameingia, kumbe badala yake wamekuwa wachapa uchumi wa nchi yetu, aibu kubwa.

Akina polepole wamejaribu sana kutetea wizi huu ili usijulikane, matokeo yake wakajikuta wanakonda tu mwili wote umetokwa mishipa utadhani mizizi ya mmea fulani.

Hii awamu haita faninikiwa kwa lolote ,kwani wamejipatia laana wenyewe, kwa matukio ya hovyo kabisa ambayo wamewafanyia watoto wazalendo wa nchi yetu.

Usitegemee taifa kupata mafanikio huku ndo linakuwa la kwanza kuteka wananchi wake na kuwapoteza kabisa kama sio kuwauwa.

Ardhi imepokea DAMU zao na hivyo laana imeitafuna nchi.

Vilio vya ndugu zao vimefika mbinguni na Mungu amevipokea .

Kwa mtindo huu ,usitegemee kuona uchumi unakua , badala yake tutaona ukizidi kudidimia.

Viongozi wetu wa dini nao pia ni mfano wa yuda , wanaungana na serikali kila siku kuunga mkono mambo maovu, badala ya kusimamia ukweli na kuwaambia viongozi wetu watubu ili laana isiendelee kuitafuna nchi.

Hii ni aibu kwa viongozi wa dini kushindwa kuwa mawakili bora wa Mungu hapa nchini, na wala sina shaka kwa kusema kuwa kama kiongozi wa dini kweli anashindwa kukemea maovu, basi huyo anamtukia shetani na wala sio Mungu wa Mbinguni.

Wameshindwa kuutumia mfano wa Nabii Eliya aliye simama mbele ya mfalme Ahabu na kumkanya juu ya maovu yaliyo kuwa yakiendelea ktk taifa lao .

Itoshe tu kusema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini ndani ya nchi yetu pia wameungana na serikali yetu kuwa Yuda Ikariyote.

Eeee Mungu muuba wa Mbinguni na ardhi tuna kusihi utuepushe na balaa hili katika awamu hii ya tano, Amina.
 
Sasa ifanikiwe mara ngapi maana mpaka sasa imeshafanikiwa kwa asilimia 80 najua huezi kuona kwasababu hauna macho,hizo ni kelele za chura ambazo hazimzuii tembo kunywa maji,ko nyie endeleeni kupiga kelele humu jamiiforum wenzenu wanaendelea na kazi
 
sasa ifanikiwe marangapi maana mpaka sasa imeshafanikiwa kwa asilimia 80 najua huezi kuona kwasababu hauna macho,hizo ni kelele za chura ambazo hazimzuii tembo kunywa maji,ko nyie endeleeni kupiga kelele humu jamiiforum wenzenu wanaendelea na kazi

Imefanikiwa kabisa. Ila kwa kufanya vitu vyenye negative impact kwenye uchumi. Nyie kina comical Alli endeleeni kusifia; lakini hali halisi inazidi kuwaumbua. Na mtaendelea kukiri ukweli kadri siku zinavyosonga kama mlivyokiri kuwa ATCL inaendeshwa kwa hasara kiasi kwamba ina mtaji hasi miezi michache baada ya kututangazia kuwa imepata faida ya bilioni 22.
 
Huna haki ya kusema lolote juu ya shutuma dhidi ya mtu hadi uwe na uthibitisho,mnabwabwaja tu je mbowe siyo mwizi?

Sent using Jamii Forums mobile app

"Wizi" wa Mbowe - na hujathibitisha au kutoa tuhuma dhidi yake - unahalalisha wizi unaojulikana wa Magufuli? Nyumba za serikali alihusika nani - na kuna ushahidi hadi wa majina ya hawara zake ambao hawakuwa watumishi wa serikali lakini "waliuziwa" nyumba za serikali? Nani aliesababisha hasara kwa kuvunja mikataba (hadi bombadier ikashikiliwa Canada)? ,Niendelee?
 
Sasa ifanikiwe mara ngapi maana mpaka sasa imeshafanikiwa kwa asilimia 80 najua huezi kuona kwasababu hauna macho,hizo ni kelele za chura ambazo hazimzuii tembo kunywa maji,ko nyie endeleeni kupiga kelele humu jamiiforum wenzenu wanaendelea na kazi
Kazi gani ya kutupiga risasi mchana kweupe na watu kutekwa na kuuawa,..mbavu sana.
 
Kakuibia mama yako?majizi wanaomuibia baba yako huyo mama yako huyaoni??ukosefu wa nidhamu kwa viongozi wenu kunawatafuna

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa mada hajatumia lugha chafu kama wewe ,na unasema niukosefu Wa nidhamu,na hapo ndipo ilipo tofauti yako wewe na ujinga wako,na weredi Wa mtoa mada,jibu hoja kwa hoja,nilichokigundua kwako ni uelewa dhaifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ifanikiwe mara ngapi maana mpaka sasa imeshafanikiwa kwa asilimia 80 najua huezi kuona kwasababu hauna macho,hizo ni kelele za chura ambazo hazimzuii tembo kunywa maji,ko nyie endeleeni kupiga kelele humu jamiiforum wenzenu wanaendelea na kazi
Ah ah hizo data kazipika your mother tena yule muongo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom