GE2025 Serikali ya awamu ya sita imetoa Bilioni 5.7 ujenzi wa shule mbili Mkoani Mara

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mkoani Mara ambazo ni shule ya Sekondari ya Wasichana Mara pamoja na shule ya Amali Butiama (Butiama Technical Sec School)

Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi huo ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) mkoani Mara kwa ajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 kuhusu kuongeza uandikishaji wa wananfunzi wa wanafunzi kidato cha kwanza hadi kidato cha nne pia kidato cha tano na sita

Kati ya fedha hizo jumla ya shilingi Bilioni 4.1 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya sekondari ya Mara wasichana iliyojengwa katika kijiji cha Bulamba kata ya Butimba wilayani Bunda

Katika shule ya Sekondari ya Mara wasichana serikali imekamilisha miundombinu mbalimbali ikiwemo Jengo lenye vyumba vya madarasa 2, majengo 3 yenye vyumba vya madarasa 2 na ofisi 1, madarasa 2 na vyoo, maabara ya fizikia na chumba cha jiografia, maabara ya kemia na biolojia, jengo la utawala, vyoo vya wanafunzi matundu 16, chumba cha jenereta, bwalo, nyumba ya mwalimu yenye vyumba 3, nyumba ya mwalimu (2 in 1), mabweni 8, jengo la wagonjwa pamoja na ujenzi wa uzio

Katika hatua nyingine serikali imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Amali Butiama (Butiama Techinacal Sec School) wenye jumla ya majengo kumi na nane 18

Fedha hizo zinaendelea kutumika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Vyumba vinne (04) vya madarasa bila ofisi, Vyumba vinne(04) vya madarasa na ofisi, Jengo la Utawala na stoo ya site, Maabara mbili(02) Kemia na Baiolojia, Nyumba moja(01) ya mwalimu(single), Makataba moja(01), Chumba cha TEHAMA kimoja(01), Mabweni manne(04), Bwalo na Jiko, Vyoo matundu nane(08), Karakana ya Mechanics & Metal fabrications, Karakana ya Ufundi uashi na Tanki la Maji

maraaa.png

Chanzo: Jambo Tv
 
Asante kwa taarifa,ingependeza uwajibikaji ukaongezeka.
 
Hizo shule ziwekwe vipaji maalumu,
Moja ya wakaka moja wadada
 
Back
Top Bottom