Serikali ya Awamu ya 4

dkn

Senior Member
Oct 7, 2010
139
42
Nchi iko kwenye wakati mgumu sana na mambo mengi au tuseme yote ni kwa sababu ya serikali ya awamu ya 4. Tunaona matatizo mengi hasahasa human rights violations, tumesikia ya Ulimboka, Kibanda, Mwangosi, kuchomwa kwa makanisa, kuuliwa au kutishiwa viongozi wa dini lakini hatuoni mabadiliko ila tu kesi ipo ni yale yale ya wala rushwa, hela za mafisadi kufichwa nje. Kwa sababu watanzania ni rahisi kusahau, tunaangalia ya sasa labda Kibanda au Lwakatare wakati kuna mambo chungu nzima yanatuzunguka.


Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa sana, ningependa sana Rais JK awe international figure fulani baada ya kumaliza muda wake ila naona nafasi ni ndogo sana kama hataweza kufanya haraka kuhakikisha haki za binadamu hazivunjwi. Tumeona wanasema he is Western darling in EA, hawa sijui Wamerekani wamefumba macho wakijua interest zao zimekaa sawa, tumeanza kukaribisha FBI kufanya uchunguzi ndani ya nchi yetu, kuruhusu mazoezi ya kivita/coast guards kwenye nchi yetu. Hii ni moja ya surveillance Western wanafanya.


Haitakuwa rahisi kwa Rais JK kuishi kwa amani baada ya muda wake kama haya mambo yataendelea hivi, ni wazi kabisa kuna kutoelewena ndani ya serikali na chama, na ambao watakuwa imposed ili walinde maslahi ya wakubwa watakuwa na wakati mgumu sana kwani Tanzania ya leo si ya 1985; kizazi cha kutishiwa kuvunjika amani kilishapita watu wanaangalia tofauti ya tajiri na maskini ni kubwa sana na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi anaonekana waziwazi, siku wananchi wataamua mbinu zote za kutishia demokrasia hazitakuwa kitu. Tulinde heshima ya Tanzania kuwa nchi yenye amani siyo ya kinafiki wakati waandishi wa habari, wapigania haki wanateswa au kunyamazishwa na kutumia propaganda ya old age..movie ya Lwakatare inaonyesha upinzani umewekewa barriers usiendelee ila yote yatawezekana ila siku ya mwisho itafika, walianza hivyo viongozi wengine sasa hivi wako wapi? Saif al-Islam Gaddafi na uongozi wa Gaddafi ulimalizwa katika hali ya kusikitisha lakini angalau hao walifanya mazuri kwa nchi yao ingawa bado wananchi walibaguliwa, sisi tumefanya nini? Watoto wame fail mitihani, shule zimekuwa nyingi na ajira hakuna, frustration hizi zikizidi tutaona kizazi kilichobadilika na kuwajibisha serikali siyo kwa debates tena bali kwa njia ya sanduku la kura na wizi wa kura hauweza kufanya chochote kama asilimia 90 ya young generation haitakubali tena utawala mwingine kama huu wa sasa.
 
Back
Top Bottom