Serikali wanasoma JF?

Serikali wanasoma JF?

JF ni kila kitu nchi hii wakiwa wametapakaa popote ufikiriapo wewe LAKINI YOTE NI KWA MANUFAA YA SEHEMU YA JAMII ISIYOKUA NA SAUTI na asiyejua hilo shauri yake!!!!!!!!!!

Nitajikita zaidi na maamuzi ya PM Pinda kuwasimamisha Mganga mKuu wa serikali na Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii, blandina nyoni.

Nanukuu:"

Sababu ya kuwasimamisha watendaji hao ni tuhuma za kuingiza nchini robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini na tuhuma za kuanzisha kampuni ya kusambaza nguo kwa madaktari na kuiingiza kinyemela kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili"

mwisho wa kunukuu.

Haya yote yalilipotiwa na jf hapa mwishoni mwa mwezi januari yakapuuzwa lakini baada ya ile tume ya bunge kuchunguza imebaini yaleyale yaliyolipotiwa hapa jf.


Mungu awape maisha marefu wanajf.

 
leo itv nimemsikia mtangazaji analalama eti ata watoto viongozi wamefeli na wameandikiwa kwenye mitandao ya kijamii..mmmh jf inausika hapa.

jf ni kwa ajili ya jamii nzima na kwa kuwa watoto wa vigogo ni sehemu ya jamii hivyo basi jf kuwaandika au kuwajadili hakuna tatizo lolote. ila ingewaacha kuwajadili JF ingekuwa si ya jamii bali ya watu wachahce na mambo machache. tutaendelea kujadili chochote na yeyote kwa mustakabali wa maendeleo na mabadiliko ya taifa letu. wasitutishe na wasiitishe JF.
 
Back
Top Bottom