Serikali: Walimu hawapaswi kuomba nyongeza ya mshahara kwa miaka ambayo haikutolewa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Tanzania imesema walimu hawapaswi kudai malimbikizo ya nyongeza ya mwaka ya mashahara kwa miaka ambayo nyongeza hiyo haikutolewa.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 10 bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mwita Waitara wakati akijibu swali kwa niaba ya waziri wa utumishi, menejimenti ya umma na utawala bora.

Wabunge wengi walisimama kutetea maslahi ya walimu, lakini Waitara akasema Serikali itaendelea kutoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wote kadri uwezo wa kulipa utakavyoruhusu.

Katika swali la msingi, Mbunge Viti Maalumu (Chadema), Zainab Mussa Bakar alitaka kujua ni lini walimu watalipwa nyongeza (increment) ya mishahara kwani tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani haijawalipa.

Naibu Waziri alisema kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni za kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009, nyongeza ya mishahara haipaswi kuombwa au kudaiwa na walimu bali Serikali ina jukumu la kutoa au kutokutoa.

Amesema nyongeza hiyo haikutolewa kwa watumishi katika miaka 2003/2004 hadi 2016/17, lakini imetolewa kwa watumishi wote wakiwamo walimu mwaka wa fedha 2017/18.
 
Hata wasipoongeza, stress wanazo wenyewe. Huku wanakalia haki za watu, huku sgr imekwama, kule wafadhili wamesusa, huku Uchumi unashuka kwa mujibi wa IMF, milioni hamsini kwa kila kijiji zimeyayuka....na 2020 hiyo hapo...watawaambia nini watu????
 
inapendeza sana..
tena wasipandishwe mpk Stone atoke madarakani hata kama atakaa miaka 100!
 
Back
Top Bottom