Serikali: Uchunguzi wa mabehewa ''feki'' 274 unaendelea

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
51,980
114,297
DAKTARI Leonard Chamuriho ambaye ni Katibu Mkuu wa Idara ya Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema, uchunguzi kuhusu kesi ya uagizwaji wa mabehewa 274 yaliyoingizwa nchini, bado haujafika tamati..Dk. Chamuriho ametoa ufafanuzi huo ikiwa ni siku moja tu baada ya Jeska Kishowa Kafulila, Mbunge Viti Maalum (Chadema) kusimamishwa vikao viwili mfululizo kuanzia jana baada ya kuishambulia serikali kuhusu uingizwaji wa mabehewa hayo.
Kishowa alisimamishwa na Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Bunge kwa madai ya kushindwa kutoa uthibitisho juu ya madai yake kuwa Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Waziri wa Uchukuzi karika serikali iliyopita, alitumia Sh. 238 bilioni kununua mabehewa mabovu.

Dk. Chamuriho amesema, uchunguzi unaoendelea na kwamba hakuna ushahidi wa kutosha hadi sasa.

“Shauri la kwanza linahusu uongozi wa TRL kukiuka sheria ya manunuzi ya Umma ya 21 pamoja na kanuni zake mwaka 2014, kuhusiana na manunuzi ya mabehewa 25 ya aina ya Ballast Hopper Bogie Wagons kutoka Kampuni ya Hindustan Engineering and Industries LTD,” amesema Chamuriho na kuongeza;

“Shauri hili lilikuwa linachunguzwa na Takukuru, uchunguzi huo umekamilika na faili limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP).”

Mabehewa hayo 274 yalinunuliwa na Shirika la Reli Tanzania (TRL) kutoka Kampuni ya Hindustan Engineering and Industries LTD mwaka 2015.

Hoja hiyo iliibuliwa kwa mara ya kwanza bungeni na Kishowa tarehe 01 Februari mwaka huu katika mkutano wa pili wa Bunge la 11.

Hoja hiyo iliibuliwa na Kishowa (Viti Maalum) wakati akichangia Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/2017.

Kuhusu mashitaka ya ununuzi wa mabehewa feki 274, Dk. Chamuriho amesema uchunguzi wake bado unaendelea na umegawika sehemu tatu.

“Uchunguzi umegawanyika sehemu tatu, mabehewa ya mizigo yaliyofunikwa 174, mabehewa ya mafuta 50 na mabehewa ya kubebea makontena 50,” amesema.

Hata hivyo, Dk. Chamuriho ameshindwa kutoa maelezo kuhusu idadi ya mabehewa yaliyoharibika na kudai kuwa, sheria ya uchunguzi haimruhusu kuongea chochote kuhusu hilo.

“Kama nilivyosema awali, siwezi nikatolea ufafanuzi suala hili sababu lipo nje ya uwezo wangu, nikieleza sasa nitakuwa nakiuka sheria na taratibu za uchunguzi. Kilichonileta ni kutoa taarifa kwamba, uchunguzi bado unaendelea ukikamilika kila kitu kitajulikana,” ameeleza.
 
H

hii Dhambi kubwa ya kuwabebesha zigo watu wengine wakati Mwakyembe ndiye alifaidi mgao mtalaaniwa sana.
 
Wa
wanapanga kumkwepesha waziri mzigo Mwakyembe
laana itamkumba kila mwenye nia ya kukwepesha zigo la Mwakyembe kwenda kwa wanyonge wasio na uwezo wa kujitetea hata wakifurukuta watakandamizwa tu ili kumwokoa Mwakyembe.
 
Nchi hii imekosa maendeleo kutokana na Tabia mbaya za kubebana ikumbukwe hata Kikwete anajua kuwa Dili la mabehewa lilipigwa na Mwakyembe ndiyo maana alimtoa Wizara ya uchukuzi na kumpeleka kwingine, mkitaka ushahidi mzuri Nendeni Msoga Kikwete akitulia ataweza kuwapa A-Z kwani kitendo kilichomponza mpaka kuhamishwa wizara ni hiyo hiyo kashifa ya mabehewa, huyo Katibu mkuu na yeye atakuwa JIPU kwa kutetea Uovu.
 
Katibu mkuu huenda akawa JIPU kubwa huko anakoelekea asipokuwa makini na hilo sakata la mabehewa chakavu.
 
Mwakyembe alikwenda kwa mkuu wa kaya na kumwambia dili lote lilivyokuwa na akasema yeye alilazimishwa na akampa mifano mingine kama ule wa uuzaji wa nyumba za serikali na ununuzi wa Mv Dar.
 
Back
Top Bottom