Serikali: Tutaajiri askari wapya 3,103

Serikali: Tutaajiri askari wapya 3,103

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,646
Serikali imetoa kibali cha kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuajiri askari polisi wapya 3103 mchakato ambao unaendelea kwa sasa kwa askari hao kuajiriwa kwa kuzingatia vigezo na masharti ya ajira za serikali.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamzo Chillo bungeni jijini Dodoma na amesema sababu zinazochangia askari kupungua ndani ya Jeshi la Polisi ambazo ni kustaafu, kufariki dunia, kufukuzwa kazi na wengine kuacha kazi.

Mhe Chillo amesema Mchakato huo wa ajira kwa askari hao wapya utazingatia kwa mikoa yote kwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kwa kupata ajira hizo mpya na watapangiwa kazi kulingana na mahitajo ya eneo ikiwemo yale yenye vitendo vingi vya uhalifu.
 
Sio walimu tena na wauguzi huko kwenye maboma wanayojenga kwa hela za tozo? Hee ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Mama, nadhani ni kupaniki kutokana na jinsi mwamba Hamza alivyowanyoosha , yaani mtu kajifunzia ugaidi kwenye video kawakalisha 4 je angeenda kozi si angeua batallion nzima. HATARI SANA
 
Janja weed una utani na binaadamu wewe😂😂
 
Sio walimu tena na wauguzi huko kwenye maboma wanayojenga kwa hela za tozo? Hee ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Mama, nadhani ni kupaniki kutokana na jinsi mwamba Hamza alivyowanyoosha , yaani mtu kajifunzia ugaidi kwenye video kawakalisha 4 je angeenda kozi si angeua batallion nzima. HATARI SANA
Ungeshauri waajiri wenye uwezo wa kutumia akili na weledi ,wasio bambikia wala kunyanyasa katika majukumu yao angalao ningekuelewa.
 
Sio walimu tena na wauguzi huko kwenye maboma wanayojenga kwa hela za tozo? Hee ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Mama, nadhani ni kupaniki kutokana na jinsi mwamba Hamza alivyowanyoosha , yaani mtu kajifunzia ugaidi kwenye video kawakalisha 4 je angeenda kozi si angeua batallion nzima. HATARI SANA
Tulia usiwe na kiherehere muda wa kukamilisha maboma walimu wataajiriwa tu

USSR
 
Wanajihakikishia ulinzi wa kusalia madarakani, kwenye sekta muhimu za maendeleo ya nchi kuna upungufu mkubwa wa watumishi hasa baada ya zoezi la kupunguza wafanyakazi kupita kipindi cha magu, leo hii kipaumbele kimekuwa ni kuajiri askari zaidi......hii nchi ina maajabu sana.
 
Serikali imesema itaajiri askari polisi 3103 ili kuliimarisha jeshi hilo kwa kuliongezea idadi ya askari.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani.

Source: Radio One
Nchi ya hovyo kabisa hii,hizo ajira zitajaa watoto wa line polisi watupu,sie wa maneromango,Mtambaswala,ushirombo,kyelwa,kamsamba tutazisikia kwenye bomba tu.
 
Hata huku Kazuramimba sijui kama zitatufikia, achilia pale kawekamo.
 
Wanajiandaa na ugaidi rasmi na sio huu wa kupaka mafuta!!!Wamemuua Hamza wanajua fika wamekosea sasa Ndugu wa Hamza will strike back for vegeance!!!
 
Serikali imesema itaajiri askari polisi 3103 ili kuliimarisha jeshi hilo kwa kuliongezea idadi ya askari.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani.

Source: Radio One
Kuajiri askari wengi sio kulifanya jeshi hilo kuwa imara bali na mafunzo pia yawe katika standard pamoja na kutoa mafunzo yatakayoendana na dunia ya sasa.
 
Sio walimu tena na wauguzi huko kwenye maboma wanayojenga kwa hela za tozo? Hee ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Mama, nadhani ni kupaniki kutokana na jinsi mwamba Hamza alivyowanyoosha , yaani mtu kajifunzia ugaidi kwenye video kawakalisha 4 je angeenda kozi si angeua batallion nzima. HATARI SANA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bila shaka itakuwa ni sehemu ya reform ya jeshi letu.... ni vyema hili liendane na uboreshaji wa mtaala pale CCP na utaratibu mpya wa kuajili..

Ni vyema pia maslahi ya polisi yaboreshwe, wakapewa meno na mamlaka kulingana na kazi yao...jamii iwaheshimu na kutii sheria hasa viongozi wa ngazi za juu..
 
Back
Top Bottom