Serikali: Tunafuatilia suala la Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini kuzuia ndege ya ATCL. Ni kufuatia Hermanus P. Steyn kufungua shauri

Duu hizi ndege bana dah mara imekamatwa Canada ikalipwa mabilioni ya shilingi ,Mara sijui dreamliner litabeba mbuzi kwenda Uarabuni
Mara sijui ka bombardier kako Zanzibar wiki ya pili hakaruki
Mara sijui tumetolewa IATA

Mara Airbus imezuliwa South

Huyo bundi aliyepo ATCL waombeni wazee wamchinjie wamuombe msamaha

Inashikiliwa kwa sababu zipi ? Au tunadaiwa hela za watu tunajifanya wababe hatulipi ?

Hapa ndio namvulia kofia Shirima walau yeye kajitahidi biashara ya ndege ni pasua kichwa
 
Sababu zipi za msingi za kuzuia? NINGEKUWA PREZI DAA HAKI YA NANI KAMA SABABU NI ZAKITOTO NAFUKUZA UBALOZI WAO KWANGU KISHA NATOA WANGU KWAO HALAFU SIPELEKI NDEGE YANGU TENA HUKO! Nchi zipo nyingi za kupeleka watu.....
Labda ifanye safari za ndani. Mabeberu wapo kila mahali.
Taifa letu linamuhitaji Mungu, uovu ukikithiri kwenye taifa hata lililozuri lazima lizimwe na matokeo ya uovu. Uovu ni mbaya sana, matokeo yake yanaonekana live.
 
Kwani wanatudai au?
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ameomba radhi kwa usumbufu ulijitokeza kwa abiria wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) waliokuwa wasafiri kutoka Johannesburg kwenda jijini Dar

Ameomba radhi hiyo kutokana na abiria hao kushindwa kusafiri kutoka uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg baada ya ndege hiyo kushindwa kufanya safari kama ilivyopangwa kutokana na kuzuiwa

Kwa mujibu wa taarifa ambayo Serikali imepokea, ndege hiyo imezuiwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafuatilia ili ndege iachiwe

View attachment 1188590
 
Sababu ya kuzuiwa ni ipi???
 
Back
Top Bottom