Serikali: Tunafuatilia suala la Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini kuzuia ndege ya ATCL. Ni kufuatia Hermanus P. Steyn kufungua shauri

Badala ya kupeleka Mawakili 16 kupambana na Lissu katika kutetea ubunge wake.

Sasa hao Mawakili wapewe Mikoba wakakomboe ndege yetu.

Hiyo ndio kazi yao

===================

Mawakili wa Serikali 15 wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Clement Mashamba wamewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu kupinga maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuhusu Ubunge wake.

====================
 
Hawa watu wasitake kucheza na Kodi zetu.., wanaopaswa kufuatilia wafuatilie haraka iwezekanavyo na waje na majibu yanayoeleweka.., hii tu sio matumizi mabaya ya kodi zetu bali pia ni kupoteza uaminifu kama watu wanaanza safari hawajui nini kitatokea.....
 
Niliposoma heading, nilitarajia serkali ingetoa ufafanuzi wa kwanini ndege yetu nime shikiliwa ama kuzuiliwa.

Binafsi naona kama hii kuwaomba radhi wasafiri ilitosha tu kuwatangazia huko huko walipo kama katibu hakuona ulazima ama umuhimu wa waTanzania kujuwa kwanini ndege imeshikiliwa/zuiliwa
 
Back
Top Bottom