Faith Luvanga
Member
- Aug 21, 2018
- 14
- 15
Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango juu ya matokeo ya utekelezaji wa Serikali ya awamu ya Tano(2015-2020) katika sekta mbalimbali imeangazia Sekta ya Afya ambapo Ripoti hiyo imelinganisha hali ilivokuwa mwaka 2015 na mabadiliko yaliyofanyika ndani ya miaka mitano ya Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sekta hiyo.
Idadi ya Hospitali za Rufaa mwaka 2015 ilikuwa ni hospitali 22 nchini kote na mpaka kufikia mwaka 2020 idadi ya Hospitali hizo imefikia 28, ambapo kuna ongezeko la hospitali 6 sawa na 27.3%
Idadi ya Hospitali za Halmashauri ilikuwa ni Hospitali 77 mwaka 2015 na mwaka 2020 idadi hiyo imeongezeka kufikia Hospitali 178 ambapo kuna ongezeko la Hospitali 101 sawa na 131.2%
Mwaka 2015 idadi ya vituo vya Afya ilikuwa 718 na mwaka 2020 idadi hiyo imeongezeka mpaka kufikia vituo 1205, ikiwa kuna ongezeko la vituo 487 sawa na 67.8%
Idadi ya Zahanati mwaka 2015 ilikuwa 6044 na mwaka 2020 idadi hiyo imeongezeka na kufikia vituo 7242 ambapo kuna ongezeko la Zahanati 1198 sawa na 19.8%
Bajeti ya Dawa kwa mwaka 2015 ilikuwa Bilioni 31 na mwaka 2020 imeongezeka hadi kufikia Bilioni 270 ambapo kuna ongezeko la Bilioni 239 sawa na 771.0%
Idadi ya safari za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa mwaka 2015 ilikuwa 683 na mwaka 2020 idadi hiyo imepungua na kufikia safari 64 ambapo kuna upungufu wa safari 619 sawa na 90.6%
Asilimia ya upatikanaji dawa kwa mwaka 2015 ilikuwa 53% huku mwaka 2020 imefikia 94.5% ambapo kuna ongezeko la 42% sawa na 41.5%
Mwaka 2015 upatikanaji wa Damu salama ulikuwa 79% huku 2020 ikiwa 97.0% ambapo hali hiyo imeongezeka kwa 18% sawa na 18.0%
Idadi ya watumishi wa Afya walioajiriwa kwa mwaka 2015 ilikuwa 86,152 wakati mwaka 2020 serikali imeajiri watumishi 100,631 ongezeko likiwa ni watumishi 14,479 sawa na 16.8%
Ripoti hiyo inaeleza kuwa,tangu mwaka 2015 hadi 2020 Serikali imetumia zaidi ya bilioni 232.1 kununua vifaa tiba katika vituo vya ngazi mbalimbali kuanzia afya ya msingi hadi taifa. Pia kupungua kwa idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka 2015 - 2019 kumeiwezesha Serikali kuokoa jumla ya shilini Bilioni 329.