Serikali TOKA usingizini Mkomboe mwananchi wako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali TOKA usingizini Mkomboe mwananchi wako!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Apr 18, 2011.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wapendwa watanzania wenzangu, Nimeshuudia kwa takriban miaka miaka saba sasa Tangu Benjamini William Mkapa akabidhi nchi kwa JK, Hali ya mwana nchi mpiga kura inaendelea kudorora na hatua madhubuti azichukuliwi kumsaidia. Ninachoshuudia ni matajiri na wezi wa uchumi wa nchi ya wananchi watanzania wakiendelea kunona na kujimilikisha .
  Maendeleao yanaporomoka na pata la taifa linashuka. Hotuba za rais ni tamu , na utekelezaji 0%.
  Tupo katika jumuiya ya afrika mashariki, lakini kwa ufupi sisi ndio waathirika wakubwa wa bei ya bidhaa za petrol. Burundi na Rwanda hawanda bandari lakini mafuta ni rais kuliko Dar.
  Kwa sasa Kenya nchi imeamua kupunguza bei ya mafuta ili kuwezesha raia na wawekezaji kupunguza makali ya operational costs (Source :Daily Nation:*- Business News*|Respite for consumers as Govt cuts fuel tax)
  Je serikali yetu inawazo gani la kuwawezesha raia wake ili tuweze kuwa na sura sawa za ushindani katika africa ya mashariki?
  Nawakilisha mada.
   
 2. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Watu tuliowapa dhamana ya kutuongoza wameshindwa kutimiza wajibu tuliowapa na sisi tunaendelea kuwakodolea mimacho bila kuwawajibisha,wametufanya mabwege.Kwani haiingii akilini pamoja na ugumu wa maisha,ufisadi,huduma mbovu za jamii,kuporomoka kwa uchumi na udhaifu mkubwa wa bunge letu ingawa tunaona hali za maisha na jitihada za nchi majirani kuboresha na kupunguza hali ngumu kwa raia wao sisi tuko kimya bila hata ya kupaza sauti zetu na kuwawajibisha viongozi wetu!INAUMA SANA....
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  As long as hawa jamaa wako madarakani SAHAU kwani naamini "improvement is impossible without a change"
   
Loading...