Serikali tatu ni zaidi ya katiba???

Grace Komba

Senior Member
May 26, 2013
131
48
Takribani wiki mbili sasa, tangu tume ya katiba, chini ya uenyekiti wa jaji mstaafu WARIOBA, watangaze rasimu ya kwanza ya katiba mpya.

Tume hii imekuja na mapendekezo kadhaa ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika kuyajadili ili kama taifa tuweze kufanikisha suala hili.

Ila baada ya uzinduzi wa rasimu hii, ghafla makundi hasa ya wanasiasa na vyama vyao wametokea kulivalia njuga suala la serikali tatu, na hata baadhi yao kulihusisha na uhai wa muungano wetu,(Zanzibar na Tz bara).

NASISITIZA, SIPINGI kwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla kujadili suala hili la serikali tatu, kama ilivyo pendekezwa na tume ya katiba.

Kinachonipa HOFU ni nguvu kubwa itumikayo na wanasiasa katika kuivuruga jamii kupitia suala hili la serikali tatu.

NI KWELI, Kujadili mifumo ya serikali zetu, na sura ya muungano wetu ni jambo muhimu na linalo hitaji umakini.

JE, suala la serikali tatu ndio PENDEKEZO PEKEE kwenye rasimu hii??

Kwanini HATUJADILI RASIMU HII KWA MAPANA YAKE??

Naomba Kuwasilisha...
 
Kweli dada, hapo umelitumia jicho la tatu ipasavyo....

WANASIASA wamejikita juu ya muundo wa serikali na sura ya muungano, kwa shabaha moja tu, ya kulinda nafasi zao za kiutawala na kisiasa kiujumla...

big up Grace Komba, Umeona Mbali Sana.
 
Back
Top Bottom