Kama serikali yetu ina busara ni vyema kuachana na hii mitambo ya DOWANS.
1.Kwanza sheria ya manunuzi hairuhusu kununua vitu chakavu (mitumba) na kwa sasa mitambo ya DOWANS ni mitumba haitakiwi kununuliwa kwa fedha za walipa kodi.
2. J Makamba anaonekana msomi asiyeelimika na anatumia nguvu nyingi kuliko akili, jambo dogo tu la kufikiria, kama kweli serikali ina nia ya kununua mitambo ingeweza kununua mitambo mipya kabisa tena pengine ya kisasa zaidi kuliko hii ya DOWANS.
HATUHITAJI MGWATT. 100 tunataka zaidi ya hizo ili kukidhi mahitaji ya umeme kwa nchi nzima na siyo Dar es salaam pekee.
3. Inaonyesha wazi kabisa kuwa kamati nzima imerubuniwa na 10% na ndiyo hiyo wanapigania usiku na mchana, na pengine tayari wameshatanguliziwa KILEGEZA KOO sasa wana haha kutetea FISADI mwenzao apate hiyo tenda.
4. Watanzania ni watu wa KUKURUPUKA KAMA NDEGE KIOTANI, yaani kila jambo kukurupuka tuuu, halafu kufuata upepo kama manyoya na bendera. Badala ya kufikiria mahitaji ya umeme ya miaka 300 ijayo, watu wanafikiria eti tupate umeme kesho halafu....?
Ndiyo maana unakuta mipango mingi sana ya KITANZANIA haitekelezeki.
Wabongo ni wazuri sana katika planning lakini utekelezaji ni ZEROOOOO.
PLAN ZETU WAKIZICHUKUA WENZETU NA KUZIFANYIA KAZI HUWA ZINAWANUFAISHA SANA, mfano mzuri ni mpango wa makao makuu DODOMA ambao Wanigeria waliuchukua na kuumodify na kujenga mji wa kisasa kabisa wa Abuja, ukweli ukifika Abuja utapenda sana. Sie tunaimba tu makao makuu makao makuu, sasa yamekuwa MAKALIO MAKUU HOVYOOOO, MJI HOVYOOOO, MIUNDOMBINU HOVYOOOOO KILA KITU HOVYOOOO!
Mfano mwingine ni wa BOMOA BOMOA inayoendelea sasa, iwe kupisha ujenzi wa barabara, kujenga viwanda n.k.
Hivi wale walioplan mwanzo WAKO WAPI? JAMANI, yaani kama wajinga vile, tunaona kabisa sehemu inajengwa isivyo kihalali tunanyamaza, eti baada ya miaka 50 tunaibuka kama vicheche kutoka shimoni na kudai kuwa hapo hapakujengwa kihalali na kuanza kuwavunjia watu nyumba zao. Hizi mie naona ni akili za Kizezeta.
Nasema haya kwa uchungu sana nikiwa na mie Mtanzania. Sina dhamana kubwa sana kazini lakini sehemu ninayofanyia kazi naona kabisa naimudu na ninafuata misingi na taratibu za kazi. Baadhi ya wenzangu huniona mnoko lakini bora iwe hivyo kwani HASARA TUNAYOIPATA TZ INATOKANA NA ''INDIVUDUAL PEORSON", YAANI MTU MMOJA NATOA MAAMUZI YASIYO SAHIHI NA KUATHIRI WATU MILIONI 40 JUST THINK ABOUT THIS!
NASEMA TENA, YAANI JITU MOJA LENYE UROHO, TAMAA NA KIBURI LINAHARIBU MAISHA YA WATU MILIONI 40 KWA FIKRA ZAKE POTOFU.
HALAFU JITU HILO HILO ETI LINAENDA KANISANI AU MSIKITINI AU LINAABUDU CHOCHOTE KILE!
USHAURI WANGU:
1. Wa TZ tutulize vichwa tupange vitu vinavyoendana na wakati na kuzingatia wakati ujao wa vizazi vyetu la sivyo tutazidi kulalamika mpaka tunaingia kaburini na hata huko ahera tutalamika tu.
2. Hasa wale wenye dhamana zenu, hebu kila unapotaka kufanya jambo litafakari kwa undani na siyo kukurupuka tu kama ndege na kutoa maamuzi yasiyo ya haki.
3.Asilimia kubwa ya Viongozi Wa TZ ni WATU WASIOPENDA 'KUSHARE' IDEAS NA WALE WANAOWAONGOZA. Yaani hujiamulia mambo wakiwa mezani peke yao bila kuwashirikisha watu/wafanyakazi wa ngazi ya chini. wanasahau kuwa wale wanaowaongoza pengine wana akili na maarifa kuwazidi wao, cheo ni dhamana tu hata mbumbumbu anaweza kupewa. basi ni vyema kujenga tabia ya kuwashirkisha wafanyakazi wa ngazi ya chini ambao wanaweza kutoa ushauri mzuri na wenye tija kwa Taifa.
Baadhi ya taasisi huendesha mikunano ya ndani ya wafanyakazi kila wiki ili kupata michango na maoni yao, taasisi kam hizi hufanikiwa sana.
Ninayo mengi sana ya kusema, lakini naona bora niishie hapa nisiwachoshe.
TAFADHALI NAOMBA MTOE MAONI TU KWANI HAYA NI MAWAZO YANGU BINAFSI NA SIMLAZIMISHI MTU KUFUATA MSIMAMO WANGU.
Ahsanteni-