Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Blogs) kuwa chombo rasmi cha habari nchini. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka na Mafunzo ya Tanzania Bloggers Network (TBN), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana Jumatatu.

"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema Dkt. Abbas.

Dkt. Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.

Katika hatua nyingine Dkt. Abbas alisema Blogs hazina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weledi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.

Dkt. Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana asubuhi.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.


Mkurugenzi Mkuu wa mtandao wa Jamii Forums Bw. Maxence Melo akitoa moja ya somo katika mafunzo hayo.


Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano,mafunzo hayo.
 
Ila chuki ya bwana yule kwenye mitandao itakuwa ipo pale pale.

Maana habari nyingi mpaka za mapambano ndani ya familia yake zinaanikwa humu.
 
Serikali haipendi mitandao ya jamii.Serikali inapenda wote tusikilize radio tanzania na TBC tu.
 
Wanatambua rasmi kama chombo cha habari ili waunganishe kenye sheria Yao ya vyombo vya habari? Maana sizonje aliomba malaika wajewafunge Mitandao ya kijamii
 
Wamechelewa.
Mitandao ya kijamii ni kioo cha watawala kujiangalia wapi wapo sawa au wanakosea.
 
Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali” alisema Abbas.
Watambue wasitambue ukweli ndo huo mitandao ya kijamii inanguvu kuliko chombo chochote
 
Back
Top Bottom