Serikali sasa ijifunze toka Tigo kwa wanaovujisha siri zake nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali sasa ijifunze toka Tigo kwa wanaovujisha siri zake nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by security guard, Aug 13, 2012.

 1. s

  security guard JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 80
  KUFUNGIWA kwa gazeti la MwanaHalisi, Jumatatu ya wiki iliyopita kumekwenda sambamba na kuwatambua na kufukuzwa kazi kwa maofisa 31 wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Tanzania jijini Dar es Salaam.

  Katika toleo lake la mwisho wiki mbili zilizopita, gazeti hilo linatuhumiwa kuandika habari ya uchochezi dhidi ya serikali kwa kuichafua Idara ya Usalama wa Taifa, uchonganishi na ugombanishi kwa watu huku pia likihatarisha maisha kati yao kwa kuwatuhumu kuhusika na utekaji nyara, utesaji wa kikatili na jaribio la kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka Juni 26, mwaka huu.

  Sitaki kurejea habari hiyo wala kukumbushia machungu ya unyama aliofanyiwa daktari huyo hasa kwa vile suala hilo lenyewe linashughulikiwa na vyombo vya dola, halafu kuna kesi inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya mmoja kati ya watu wanaodaiwa kufanya ukatili huo kutiwa mbaroni mwezi uliopita.

  Ninachotaka kuzungumzia hapa ni hatua iliyochukuliwa na kampuni ya Tigo ya kuwatimua kazi mara moja baadhi ya maofisa wake, wale ambao wanadaiwa kutoa nje siri za wateja wa mwajiri huyo kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

  Wanatuhumiwa kuvujisha siri za mawasiliano yaliyofanywa na baadhi ya wateja wake na Ulimboka kwa gazeti hilo ikiwemo kutoa namba za simu zao, muda waliowasiliana naye kwa namna moja ama nyingine na majina yao, kisha wakahusishwa na madai ya kumteka, kumtesa, kujaribu kumuua na kumtelekeza katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  Tumesikia kelele nyingi zilizopigwa kijinga na baadhi ya watu wakiishutumu serikali kwa kulifungia gazeti hilo. Tumeona baadhi yao wanavyokwenda mbali zaidi kwa kutaka ilifungulie, wengine wakisema ifanye hivyo “mara moja na bila masharti yoyote” kwa madai kuwa adhabu hiyo ni ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari nchini.

  Wanazungumza kipuuzi kwa kauli za kijinga dhidi ya mamlaka halali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanajifanya eti hawafahamu kuwa vyombo vyote vya habari vinaendesha majukumu yake siyo kwa ridhaa zake vyenyewe isipokuwa kwa matakwa ya kisheria bila ya kujali kama ni mbovu kama wanavyodai na hata vinginevyo.

  Magazeti yote nchini yanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, ileile inayopigiwa kelele nyingi ikisemwa imeshapitwa na wakati na kandamizi, lakini ileile na vilevile inapotumika kusajilia magazeti hakuna anayedai au kusema kuwa ni kandamizi ama kwamba inatakiwa ibadilishwe.

  Udikteta wa sheria hiyo na maneno mengine ya shutuma dhidi yake unakuja tu wakati gazeti linapochukuliwa hatua zote halali za kisheria na serikali ikiwemo kuonywa, kufungiwa au kufutwa kabisa kutoka kwenye orodha ya magazeti pindi linapokwenda kinyume cha weledi pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

  Hapo ndipo kelele zinapoanza kutoka midomoni mwa baadhi ya watu wakiongozwa zaidi na wanasiasa na wanaharakati nchini, wote wakifanya hivyo siyo kwa nia njema isipokuwa kwa ujinga wa kutumiwa na magenge yanayoitwa wahisani na wafadhili kutoka nje ya nchi.

  Wanafanya hivyo kwa kutaka kuivuruga serikali ili ishindwe kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kile ambacho katika ujumla wao wanapenda kiondoshwe madarakani mwaka 2015 huku chaguo lao hivi sasa likiwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachotaka kuleta ushoga nchini!

  Nikirudi katika maudhui hasa ya makala yangu hii, napenda kuipongeza kampuni ya Tigo Tanzania ilivyochukua hatua za haraka kuwawajibisha watumishi wake kwa kuvujisha nje siri za wateja wake, jambo linaloweza kusababisha watu wengi waikimbie na kujiunga na mitandao mingine ya simu maana ipo mingi na tayari ushindani miongoni mwa makampuni hayo ni mkubwa kupindukia.

  Tayari kuna kampuni mbalimbali zikiwemo kubwa za Vodacom, Airtel na Zantel huku nyingine zikianzishwa na kuingia sokoni, jambo ambalo litaongeza ushindani ambao ni pamoja na uaminifu, uadilifu, unyenyekevu; nafuu ya gharama za kupiga, kupokea ama kutumia ujumbe mfupi wa maneno na ubora wa mawasiliano kwa wateja wake.

  Haiwezekani mwajiri aendelee kuwakumbatia watumishi waliokosa uaminifu na kufikia mpaka hatua ya kutoa nje siri za wateja wake ambao kimsingi uwepo wao ndio maisha yao ya kila siku, familia zao na ndugu zao wenyewe, lakini wanakuwa na ujinga wa kutumiwa na waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati kutenda kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

  Sifahamu endapo kampuni hiyo ina utaratibu wa kuapisha watumishi wake iwe kwa mdomo au maandishi na kumbukumbu hizo kuhifadhiwa, lakini hata iweje ni ujinga na kinyume cha utumishi mahali popote duniani kwa mfanyakazi awe wa ndani au shambani kutangaza kitu chochote kinachofanywa na mwajiri mahali popote bila idhini yake mwenyewe.

  Kama jambo hilo lingekuwa halina tatizo hakika wafanyakazi wenye mchezo huo wa ovyo wangekuwa wanavujisha kwanza siri zao wenyewe na wake zao nyumbani, waume zao au wapenzi wao, vinginevyo wangekuwa wanaeleza wanavyokiuka sheria na kanuni za ajira zao kwa hujuma zote wanazofanya.

  Kila wakivujisha nyaraka zisizotakiwa kutoka nje ya ofisi au kwa watu wasiotakiwa siku zote wangekuwa wanatangaza walichofanya, lakini hawafanyi hivyo kwa vile wanaelewa kuwa hairuhusiwi katika hali zote na hilo ni kosa la jinai kwa sheria zote za kazi.

  Ndiyo maana naipongeza kampuni hiyo kwa kuwachukulia hatua za haraka kuwang’oa na kuachana nao mara moja. Naishukuru kwa sababu imetimiza wajibu wake halali unaopaswa kufanywa na waajiri wote duniani kuanzia sekta binafsi hadi za umma ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  Mchezo wa kuvujisha siri za ofisi sehemu za kazi umegeuzwa kuwa mchezo wa kawaida kuanzia wizarani hadi bungeni, taasisi za fedha na idara takribani zote za serikali.

  Leo utasikia “nyaraka tulizonazo” au “habari za ndani zilizopatikana kutoka” wizara hiyo, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na kadhalika.

  Huko ndiko zinakotoka siri nyingi za serikali na kuangukia mikononi mwa wanaharakati wa masuala ya kijamii ingawa ukweli ni wanaharakati wa kisiasa, viongozi wa vyama vya siasa na makundi mengine yakiwemo haramu.

  Ndiyo maana kwa mfano haishangazi kusikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa au Mwenyekiti wake, Freeman Aikaeli Mbowe wakitamba kukamata nyaraka za serikali na kuongeza uongo na uzushi juu yake.

  Wanadai nyaraka hizo ni maelekezo maalum ya serikali kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa, Miji na Wilaya ya kuwashughulikia wapinzani huku wakijua ni uongo ila wanafanya hivyo kwa malengo ya kisiasa na kupotosha ukweli.

  Wanatumia nyaraka hizo kufanya uchochezi kwa nia ovu, uchonganishi na ugombanishi ili wananchi waichukie serikali yao na CCM kwa kuwapandikizia majungu, uzushi na fitina zote wanazoweza kuzifanya wakati wowote na mahali popote.

  Bila kujifunza kutoka kampuni ya Tigo na kuanza kuwafuatilia watumishi wote wa serikali na taasisi zake wanaovujisha nje siri za ndani ikiwemo kudurufu nyaraka, kuwakabidhi wanasiasa au watu wengine kinyume cha sheria na kanuni za ajira, kisha kuwatimua kazi na tena kwa haraka na kupoteza haki zao zote kamwe hawawezi kukoma.

  Hiyo ndiyo kazi inayopaswa ianze sasa na kusimamiwa moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Ikijifunza kutoka Tigo isijifunze kuchukulia watu sheria tu...ijifunze na matakwa ya utawala bora. Halafu Tigo haina ukubwa ilionao serikali...keep that in mind as well
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii habari yako umejichanganya sana, pia inazidi kuonyesha kuwa Kufungiwa kwa Mwanahalisi na sasa kufukuzwa kwa wafanyakazi 31 wa Tigo ni ya kisiasa zaidi kuliko sheria husika. Kitendo cha kuongelea wanasiasa bila vidhibitisho, unaonesha upande uliopo na jinsi usivyopenda uhuru wa habari kutekelezwa ambayo ni haki yetu ya msingi sisi raia. Sikunyingine ukitaka habari yako ilete mafundisho/ujumbe wenye mantiki jaribu kuwa neutral (ama kuficha itikadi yako).
   
 4. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  ww ni kchekesho' upo kisiasa zaidi...
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nimeacha kusoma habari yako na kufahamu wewe siwezi to add up 2 and together, pale uliposema mtuhumiwa wa utekaji na utesaji wa Dr. Ulimboka yuko mbaroni.

  Kama nyinyi ndiyo future DCs wa Tanzania, no wonder Watanzania tunataka cheo hiki kiondoshwe kwenye katiba mpya. DC gani wewe usiyeweza ku connect DOTS!!!!
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mada yako nilitaka kui-group kwenye zile mada za ma-independent great thinkers. Tatizo haka ka-paragraph, ila siyo mbaya sana uelewa wako siyo mbovu sana kama wa akina Nape Moses Nnauye
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  100% perfect.
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wewe acha udini wako huo, biashara yako ya kitimoto imedorora kwa sababu wewe unauzia watu viporo.
   
 10. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hivi viporo vya kitimoto nilikuwa naviuza hata kabla ya mfungo, kwanini kwasasa biashara inadorora? inahusuano gani na huu mfungo tukufu? nahitaji kufanya utafiti kwakweli
   
 11. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Very simple tuu hii yote ni Udhaifu wa Serikali, Serikali yoyote makini duniani haiwezi ikawa na madudu kama Serikali yetu Corruption imetawala sana wananchi nao wanafika mwisho wanachoka nao wanaamua kutoa siri watazitunza mpaka lini jamani.

  Kama watu tulio wapa dhamana ya kutuongoza wanatu nyongea kati mwategemea nini? Hao hao ndio wanafanya nchi hii iwe inayumba kila kukicha ukinyanyua mdomo wana ku Kolimba au wana kuulimboka sasa tena mchana kweupe live.

  Sasa hapo nani mchochezi Serikali inafungia gazeti kwa ushahidi wake mwenyewe kuuficha then unasema fulani ni mchochezi khaaaaa this is PATHETIC. Kwanini leo wananchi wasiwe na imani na kila chombo cha serikali?? ni kwaajili ya upuuzi kama huu.

  Mfano mzuri mkirudi Nyuma maksikiliza Hotuba za Baba wa Taifa Mwl Jk Nyerere utadhani alikuwa anaongea jana tu kuhuu issue flani na ndio haya yanajitokeza sasa viongozi kama walishindwa kujifunza that time ya Mwl.JK nyerere leo ndio wataweza maana sikuhizi tumeamua kuiita SERIKALI SIKIVU
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Registration ya namba za simu si ndio matumizi yake haya, sasa kwa nini wafukuzwe? Hawakujua kama ku-register simu ingekula na kwao?!
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sidhani. JK alishasema biashara ya kitimoto inadorora sana wakati wa ramadhani, sababu wateja wengi huwa wamefunga. Au hukumbuki?
   
 14. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Namshukuru MUNGU aliyeniwezesha kufuta maneno yangu ya kwanza niliyoandika (nadhani usingependa kuyasoma).
  Kwanza hakuna ushahidi kwamba hao watu ndio waliohusika kuwapa taarifa tigo (injustice and unfair termination)
  Mwanahalisi lazima lifunguliwe wewe!
  Kama unaogopa siri zako zisivuje basi usifanye uhalifu!
  Magazeti ya habari za kichunguzi hajaanzia Tanzania. Na vyazo vyake cku zote ni vya siri. We unafikiri bila kuwa na vyanzo vya siri na uhakika, ufisadi utaisha? Mnataka habari tunazozisoma ziwe zile za kuwaita waandishi na kuwaambia mnayojisikia kwamba ndiyo yanafaa tuyajue!? Enzi hizo zimeshapita, amka!
  Mwanahalisi litarudi tu, kwa jina lake au kwa jina lingine!
  Yaani tungekuwa tumekaa karibu halafu ndio unaongea hayo maneno uliyoandika hata sijui kungetokea nn!
   
 15. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hivi Mods ule mtindo wa kumerge ID mmeacha siku hizi? Au detector yenu iko outdated? Haiwezekani dunia ya leo mshindwe kumerge ID za huyu "First Class Degree" wa uchumi kutoka UCC!
   
 16. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Very sad kumbe ilani ya ccm ni pamoja na kutesa na kuua watu dah nilikuwa sijui,leo mleta thread ndio umenifumbua, kwamba kutaja watekaji na watesaji ni kuzuia ilani ya ccm kutekelezeka,ni kweli tutaona na kusikia mengi yaliyojificha
   
 17. Brine

  Brine JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimepoteza bure mda wangu kusoma hii habari ambayo haina kichwa wala mguu
   
 18. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hata kama watumishi wa Tigo na Mwanahalisi wasingezungumzia habari hii (kwa mujibu wa mleta mada), WIKILEAKS ingefumua tu hakika!
   
 19. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wachache wasio elewa wanakosea sana katika red hapo na kwa bahati mbaya sana hawa watu wamepenyeza kwa wingi sana kwenye nafasi za maamuzi katika taifa hili.

  Sasa kwa vile walijipenyeza kwa kutumia mbinu 'bandia' wanaendelea kujiaminisha kuwa wanaweza kuendelea kuwepo huko kibandia bandia ambalo ni jambo gumu sana.
  Vyote vinaweza kufanyika lakini kuuzuia ukweli ujulikane ni vigumu sana sana sana....

   
 20. z

  zanga Senior Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  jamani, hao watu ni majambazi, wauaji,sioni mantiki ya kuwaficha,tume wekwa wazi, ukweli upo dhahiri,walio mtesa dr ulimboka washajulikana, binafsi nawapongeza wote walio toa taarifa juu ya majambazi haya yanayo jiita usalama wa taifa, hebu tufikirie tena, jamaa walio toa taarifa wamefanya kazi nzuri, uongo umejitenga, namba zao na majina tumeyajua, hakuna haja ya kuficha siri za wauaji, wawekwe wazi watu tuwajue, sio kusingiziana na kina joshua mulundi,
   
Loading...