Serikali na wizara husika bado hamjaliona hili utoaji wa pembejeo za kilimo?

Mmanu

JF-Expert Member
Feb 11, 2015
1,684
917
Tunajua kuwa serikali kupitia wizara zake wanayo nia thabiti ya kuhudumia wananchi wake kwa kuwapatia huduma stahiki ili kuleta ustawi imara wa jamii yake katika nyanja mbalimbali kama eneo la kilimo, afya n.k.

Ila hoja yangu ipo katika suala la utoaji wa pembejeo za kilimo ambapo kumekuwa na ucheleweshwaji wa kutoa huduma hiyo kwa wakulima bila kuzingatia muda sahihi wa kuzipeleka kwa wakulima huku wakitambua wakati muafaka wa mahitaji ya pembejeo hizo kutokana na hali ya hewa ya maeneo tofauti ya nchi.

Mfano, suala la mbolea za kilimo hapa nazungumzia zile za kupandia na kukuzia kama Dap na Urea kwa mkoa wa Mtwara maeneo yake mengi huanza shughuli za kilimo hasa kwa mazao ya muda mfupi kma mahindi, karanga n.k kuanzia mwezi wa 12 ambapo wakulima wengi wanajiandaa kuweka mbegu chini lakini mpaka kufika muda huo hizo mbolea bado zinakuwa zipo kwenye makontena bandarini zikisubiri kusambazwa ambapo huanza kupelekwa kwa wakulima mwezi wa 4 wakati ambao mazao yanaanza kuvunwa

Pia katika pembejeo za salfa na viuatilifu katika zao la korosho, imani niliyonayo ni kwamba serikali kupitia wizara husika wanatambua wazi kabisa ni wakati gani wakulima wa mkoa wa Mtwara wanaanza upuliziaji wa mikorosho ikiwa ni kuanzia mwezi wa 4 lakini kinachotushangaza ni kuletewa hizo pembejeo mwezi wa 6 wakati ambao mikorosho imeshapoteza Maya tayari.

Je serikali kupitia wizara ya kilimo hamulioni hili kama mnawafelisha wakulima kwa kutowapelekea hizo pembejeo kwa wakati huku mkijinasibu kwamba ni serikali inayowajali wakulima wake?

Au hamuoni kama mnawafanya wakulima kukosa mazao mengi na bora ili waweze kujiepusha na njaa inayoweza kuletwa na upungufu wa chakula?

Hata katika eneo la uchumi pia hamuoni kama mnawafanya hawa wakulima kuendelea kuwa masikini kila siku na kuishi maisha ya utegemezi wakati tukiamini kwamba zao la korosho ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara katika nchi yetu yanayoliingizia taifa letu pato kubwa na ushuru mbalimbali lakini bado wazalishaji tukiwaacha na umasikini uliokithiri?

Lini yataonekana haya yote
 
Back
Top Bottom