Mtyela Kasanda
JF-Expert Member
- Oct 13, 2018
- 554
- 819
Hili halina mjadala. Polisi wanajikimu kupitia kodi zetu na kazi yao ni kuhakikisha usalama wetu. Kawaida ikitokea ajali askari wanatakiwa kuwahi kufika eneo la tukio na kufuata taratibu za kiusalama.
Kama ajali imetokea, watu wamechomoa betri ya gari, watu wanakunywa mafuta askari haonekani kwenye barabara kuu
Serikali iwajibike. Mungu aepushie mbali inawezekana kuna mtu alikua hana hata mpango na mafuta na amelipukiwa na moto. Tunakuaje na askari wachache kwenye nchi ambayo maslahi ya askari ni kidogo?
Tunakuaje na askari wasiofika mahala husika kwa kukosa usafiri kwenye nchi ambayo tunajenga sgr? Mimi ni mwana-ccm na damu hii ni ya uzembe wa serikali inayojitanabaisha kwa utendaji.
Ajali imetokea sawa, ila ajali imetokea halafu baada ya dk10+ ndo imeua watu kwenye barabara kuu, lipeni tu fidia hapo aisee.
Tena fidia ya maana.