chibuga mugeta
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 1,176
- 1,055
Ni jambo la kushangaza kuona kodi zetu zikitumika vibaya katika shirika la TBC. Taasisi za serikali karibia zote ukienda mapokezi wamefungulia CLOUDS au EFM, kwenye basi za mwendokasi hivyo hivyo na kwenye treni hivyo hivyo. Sasa hadi kwenye stendi za daladala kama mawasiliano na Ubungo mkoa hivyo hivyo.
Hii redio na TV zinajitangazaje? Bora zifutwe au wajiunge na EFM au CLOUDS maana wao ndo kila sehemu unawasikia. La sivyo tunaomba kodi zetu zisipelekwe huko. Hadi nahisi kuna mkono wa mtu au kuna viongozi wana hisa na hivi vyombo vya habari vingine na wanaihujumu serikali.
Mbaya zaidi mkurugenzi wa TBC na timu yake imelala fofofo. Kama mmeshindwa kuendesha msituharibie kodi zetu la sivyo laana itawajia ninyi na kizazi chenu.