Serikali na shule za kata vipi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na shule za kata vipi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Yona F. Maro, Aug 5, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mimi sio mtaalamu wa masuala ya elimu , lakini kuna suala moja limenigusa nalo ni hili la shule za kata , katika miaka karibu 5 iliyopita shule za kati zimekuwa kwa wingi sana hapa nchini , watu mbali mbali wamepeleka watoto wao katika shule hizo , shule hizo nyingi hazina walimu wa kutosha na wale wenye uzoefu na kazi hizo matokeo yake ni kwa watoto wanaosoma katika shule hizi kutokumaliza shule au kufeli kwa wingi na matatizo mengine mengi .
  Sijapata kuona ripoti yoyote inayoonyesha mafanikio ya shule hizi za kata ambazo zimezagaa sana nchini kwa sasa , zaidi ya kusikia habari za kutisha na kusikitisha toka katika wanafunzi wanaosoma humo au wazazi waliokuwa na wanafunzi katika shule hizo
  Vile vile katika elimu ya juu ni nadra sana kukuta mwanafunzi pale aliyetoka katika shule za kata au katika masoko ya ajira nayo ni vile vile tumezoea kuona wanafunzi wa shule zile zile toka wakati wa uhuru
  Serikali imejipanga vipi kuhusu matatizo ya shule hizi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na mipango ambayo sio endelevu ya wizara husika pamoja na maslahi mengine ya kisiasa zaidi kuliko mambo halisi ?
  Serikali imejiandaa vipi na suala la ajira huko mbeleni kwenye jumuiya ya afrika ya mashariki wakati wanafunzi wengi wa shule za kata ambao wangeweza kuleta ushindani huko mbeleni wanaishia njiani kutokana na mipango hii ?
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Shy ni EL na sisi m. wanaoweza kukupa jibu sahihi au uwe tayari kupata maumivu kwa hasara ya shule hizi.
  Lakini sikiliza hotuba ya hawa jamaa majukwaani wanavyojinadi! si unasikia hata wewe?
  Wakati mwingine huwa napandwa mzuka nikisikia ngonjela zao kuhusu elimu na shule za kata.
  P*****u sana.
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya mkuu.
  Umesomeka japo kwa shida.
   
 4. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Suala hilo mkuu wala halihitaji utaalamu wa unajimu. Kweli Wizara imechemka na inaonekana kama vile hawakujipanga.

  Ingawa kuna wakati niliwahi kuhoji hili nikaambiwa kwamba kulikuwa na politics kwenye uanzishwaji wa shule hizi kama mnakumbuka kuna wakati ilitoka katuni iliyokuwa ikimuomyesha EL na sera zake za shule za kata (UYOGA) sijui alikuwa akifikiri nn ingawa kweli zimesaidia watoto wengi licha ya kwamba sasa imekuwa budden kwa Wizara cha msingi serikali lazima ihakikishe kwamba wanaweza kuweka uwiano sawia wa walimu la sivyo hali nafikiri itazidi kuwa mbaya kwenye suala la Elimu kwa ujumla wake
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nadhani matokeo ya kwanza ya form four ya shule za kata za Lowasa yatakuwa ni 2010. Hapa ndipo wataona ukweli ambao pamoja na kuujua wameuficha.
  Kwa kuwa suala la elimu limekuwa politized naogopa kwamba watakuja na hoja ya kufuta mitihani ya form four kwamba haina maana tena kama walivyofanya ile ya form two, ili kuficha aibu yao. Na I guess watakuja na sera ya kwamba mtu akimaliza form four basi ajue kamaliza shule, na anayetaka kuendelea aombe kufanya mtihani special wa kwenda form five au college. Akishinda sawa asiposhinda basi.
  Hii bila shaka itaficha aibu kubwa inayowasubiri karibuni.
  grrrrrrrrrrrhhhhh
   
Loading...