SERIKALI na BUNGE wanatekeleza maagizo ya Kambi ya Upinzani nusu nusu!

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Wakuu wana JF

Sakata mchakato wa ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme kwa TANESCO bado ni bichi. Serikali na Bunge wanatekeleza ushauri/maagizo yaliyotolewa na Kambi ya Upinzani Bungeni, kupitia kwenye hotuba ya Nishati na Madini, iliyosomwa na Waziri Kivuli, Ndugu John John Mnyika! Kama ilivyaondikwa hapa;

Mheshimiwa Spika; hata hivyo hatua hizo dhidi ya Mkurugenzi wa TANESCO na watendaji waliohusika zisigeuzwe kuwa kafara ya kuficha uzembe na udhaifu wa Serikali kwa ujumla wake kwa kuwa taarifa za utendaji wa TANESCO kuhusu mpango wa dharura wa umeme pamoja na ununuzi wa mafuta uliokuwa ukifanyika zilikuwa zikiwasilishwa kwenye vikao vya Wizara ya Nishati na Madini na hata vikao vya baraza la mawaziri.

Hivyo, ili ukweli wa kina uweze kujulikana Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa bunge liazimie kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza masuala yote ya ukiukwaji wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka na tuhuma za ufisadi katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na ununuzi wa mafuta wa ajili ya mitambo ya umeme. Uchunguzi huo uhusishe pia mkaguzi mkuu kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi (Forensic Audit) kwa malipo yaliyofanywa na makampuni ya BP (Sasa PUMA Energy), Oryx na Camel Oil ili kubaini iwapo kuna vigogo zaidi wa serikali waliojinufaisha kwa kisingizio cha dharura ya umeme.

Izingatiwe kwamba masharti ya ibara ya 27(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamtaka kila mtu "… kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja (na) kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu….".

Ukisoma habari iliyoko ukurasa wa mbele wa Gazeti la Habari Leo la Jumatatu leo unaweza kuelewa kuhusu PPRA kutaka kufanya uchunguzi wa mchakato wa zabuni. Lakini pia hatua ya bunge kuunda kamati kuchunguza kilichojiri ni kuchakachua ushauri mzuri uliotolewa kwa manufaa ya taifa ili ku unfold uchafu mwingi/makando kando yote yanayoendelea wizarani.

Sasa badala ya kuufanyia kazi ushauri huo kwa dhati kusimamia maslahi ya Watanzania wote, wanachangua vipengele pengele, nusu nusu kwa namna wanavyotaka wao, kulinda maslahi yao binafsi, ya chama chao na serikali yao, badala ya maslahi ya umma wa Watanzania!
 
Back
Top Bottom