spartacus
JF-Expert Member
- Sep 26, 2010
- 428
- 142
habari,
hivi karibuni baada ya maandamano ya wanamtwara tarehe 27/12/2012, kupinga uamuzi wa serikali kusafirisha gesi kwenda mkoani dar es salaam, umezuka mjadala mkubwa ambao pia umefanya watu watoe maoni yao mbalimbali juu ya uamuzi huo.
hii imepelekea hata baadhi ya wahariri wa magazeti kuandika makala mbalimbali wakisema wanamtwara wanakosea, kwa kutaka gesi ibaki mtwara....kiukweli kwa ufahamu wangu mdogo na utafiti wa siku 7 nilizokaa mtwara, nimegundua kuwa si kweli kwamba wanamtwara hawataki gesi iende mkoani Dar es salaam, bali wanataka iende sehemu tu ya gesi hiyo kwa ajili ya matumizi mengine, ila kwa suala la umeme,ni vema serikali ikajenga power plant mkoani humo, ili mkoa uwe na umeme wa uhakika, na kuvutia uwekezaji ili mkoa huo ujiinue kiuchumi, baada ya tegemeo lao la zao la korosho kunufaisha wachache...
kiukweli kwa mtwara, raslimali pekee waliyobaki nayo ni hiyo gesi, wanajiuliza, kama wameanza kuuza korosho tangu miaka ya 60 haijawasaidia, gesi hii ikiondoka, mkoa huu utabaki na nini??
mrahaba wa gesi unaochukuliwa na halmashauri husika, ni asilimia 0.3, yani kwenye tshs 100,000, halmashauri inapata tshs 3,000/=....hayo maendeleo yatafika lini.....
afu, hivi kiwanda kikijengwa mtwara, viwanda vingine vya wawekezaji vikajengwa mtwara, je mapato ya kodi yatachukuliwa na mtwara?? je kuna MTWARA REVENUE AUTHORITY?? Jibu ni hapana, regardless, kiwanda kijengwe wapi, mapato yanaingia taifani....kumbe hoja kubwa ya watu wa mtwara, si kupata mapato yatokanayo na gesi hiyo, hapana, bali, ni fursa za ajira, ambazo serikali yao haijawahi kuwapa tangu enzi za utawala wa hayati JK NYERERE.
waharirir waliondika makala kupinga madai ya wanamtwara, pengine wafanye tafiti na kueleza watanzania, mrahaba wa gesi ya songosongo na somanga, umewafikia watu wa wilaya ya kilwa mkoani lindi?? na je lindi, imenufaika na nini kinachoonekana..?? wafanye hivyo hivyo kwa kidatu, panapozalishwa umeme na kupelekwa dar es salaam.
alafu, serikali inakiri kuwa dar es salaam inazalisha 80% ya mapato ya nchi, je ni halali kwa serikali kufurahishwa na jambo hilo, nchi yenye mikoa zaidi ya 30 kutegemea mapato ya mkoa mmoja?? kwanini wasianzishe dar es salaam zingine hata tano, kwa maana kuwe na mikoa mingine zaidi ya mitano yenye kuzalisha mapato ya aina hiyo..?? ni hadi lini wasomi wote watabaki dar es salaam, ni hadi lini dar es salaam iendelee kufurika wakazi kwa kutafuta ajira na kubanana, itafika siku mji huo utafurika, hivi sasa wakazi wanatoka bagamoyo na mlandizi kwenda kufanya kazi kkoo na posta, je 2020 watatokea wapi? kwa nini serikali isitengeneze sehem nyingine ya kupeleka watu kwa lengo la kuinua uchumi wa maeneo husika na taifa kwa ujumla??