Serikali: Mwenyekiti wa maimamu ni muhuni

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,662
20,416
...
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan, wamenusurika kipigo baada ya kutokea vurugu kwenye kikao cha kujadili muswada wa mabadiliko ya Katiba mpya visiwani Zanzibar.

Vurugu hizo zilitokea katika ukumbi wa Shule ya Haile Selassie mjini Zanzibar jana, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, kuchangia kwa maneno makali na baadaye kuuchana hadharani muswada huo na kutoka nje ya ukumbi.
Tukio hilo lilisababisha baadhi ya wajumbe kuzichana nakala za muswada huo huku wengine wakinyanyua viti juu wakiashiria kwamba mkutano huo umekwisha na baadhi yao wakimfuata Sheikh Farid nje ya ukumbi wa mkutano.


Akizungumzia vurugu hizo, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, alisema waliofanya vurugu hizo ni wahuni. Alisema kikundi hicho cha wahuni kilikwenda katika mkutano huo kwa malengo maalumu, ili ionekane watu hawataki Muungano.... Source: Tanzania Daima 10/04/2011
Haya sasa maimamu, tunasubiri tamko either muendelee kuiunga mkono serikali au kuipinga. Kazi kwenu.
 
Ni kweli pengine hatuwajui wazanzibar Vizuri sana, ila tunasikia kwamba ni kikundi cha watu wachache kutoka visiwa jirani na Tanganyika ambao tamaa yao kubwa ni kufaidi kikamilifu mali za watanganyika kama ardhi , ajira Serikalini na Elimu ya juu kwa kisingizio cha muungano huku wakikataa kuruhusu watanganyika kufaidi mali za zanzibar (kama Ardhi, Mafuta hewa N.k),

just thinking aloud!
 
Serikali na sherikh yupi muhuni? Ccm na serikali yake ni wahuni kupindukia.
 
Back
Top Bottom