Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 643
- 433
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amerejea nchini leo, Oktoba 31, 2026, akitokea Moscow, Urusi, ambako alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na Urusi, uliofanyika Oktoba 28–29, 2026.
Soma Pia: 𝗪aziri Mkuu kumuwakilisha 𝗥ais Samia mkutano wa Afrika na Urusi
Mkutano huo ulilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano wa kiuchumi na biashara, pamoja na kupanua fursa za ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Urusi na nchi za Afrika.