Serikali msupport Mziki wetu bado sanaa

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari wana JF.Sekta ya burudani imeendelea kukua kwa kasi sana. Nikijikita katika mziki hasa(Bongo Fleva).

Ni moja ya sehemu ambayo imekuwa ikiwapa vijana ajira lakini pia imechangia upatikanaji wa mapato kwa serikali kwa kiasi kikubwa sana.

Wanamuziki wetu wa muziki huu wa kizazi kipya wamekuwa wakipambana sana lakini support wanayopata serikalini ni ndogo sana.

Tukichukulia mfano Serikali ingewajengea ukumbi maalumu wa kufanya matamasha(Arena)unaochukua watu wengi zaidi na wenye vifaa vingi na wa kudumu.

Kwanza ungeingiza mapato zaidi na kuitangaza sekta ya mziki na Tanzania kwa ujumla.

Lakini kuwatumia wanamuziki kwenye kampeni tu haitoshi. Wasanii katika nchi za ughaibuni wanawaachia wanasiasa kampeni Ila huku kwetu kampeni ndo kama jukwa a la wasanii.

Wasanii katika nchi za wenzetu wanapewa heshima kubwa ikiwemo kushiriki katika masuala makubwa ya kidunia mfano kampeni za kupinga ubaguzi,kampeni za kulinda amani lakini sisi eti kampeni.

Lakini hata hivyo muziki bado haulipi kisawasawa.

Kwa mfano kwa wanaoujua wimbo wa "Despacito" by Luis Fonsi ndio wimbo uliotazamwa zaidi Duniani.

Huyu jamaa faida aliyoingiza katika wimbo ule huwezi hata kulinganisha na mafanikio ya Diamond Platnumz kwa miaka 10..

Sasa je kama wimbo mmoja unamlipa kiasi hiko unadhani baada ya miaka kadhaa atakuwa wapi?

Serikali yetu hii na Basata wanafungia nyimbo zetu Kwa sababu eti hazina maadili wakati huo huo tunatazama nyimbo za Kina Nick Minaj na Cardi B kwenye vituo vyetu vya TV je za wenzetu kwani zina maadili.

Maadili hayawezi kujengwa na Basata bali wazazi wa watoto. Wasanii hawafanyi kazi kwa uhuru kabisa
 
Assist ya serikali ku-support mziki ni katika kipindi hiki cha kampeni

Bila kuishobokea ccm na kuunga juhudi utafeli, kumbuka zali hili huja mara mbili kila baada ya miaka kumi
 
Nyimbo za bongo zina quality ndogo sana na mashairi yake yameegemea ngono zaidi mtu mwenye kujielewa ni ngumu kusikiliza pia kuendeleza mmomonyoko wa maadili kwa vijana.
 
Uzi wa hovyo 2020
Hawa wanani sjui mambugila kutwa wao ndy wanataka waonwe, kutwa wao ndy kulialia
Cha ajabu wao ndy wanabebwa lkn sijui hawalioni hilo
NGUVU kubwa wanayofanyiwa haifanyiki kwa wakulima na wengineo

Ova
 
Kwa hiyo unataka serikali ilazimishe watu wanunue muziki au???
US watu wananunua muziki na sio kucopy kwny flash disks kama bongo, pakiwa na show/tour watu wanalipa kumuona msanii wao pendwa.
 
Badala tuache kuwalilia wakulima madaktari manesi walimu tuwalilie nyie wadangaji

Ova
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom