SERIKALI mnakera SANA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SERIKALI mnakera SANA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kyindokyakombe, Jun 1, 2012.

 1. K

  Kyindokyakombe Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SERIKALIi yetu mnakera na msipokuwa makini mtaanza kukera hata WALIOKWISHA KUFA.Haiingii AKILINI kwa mtu mwenye akili kusikia WATUMISHI mbalimbali wa SERIKALI yetu wanaidai SERIKALI huku SERIKALI ikitumia PESA hovyo.Mfano pesa zinazotolewa kama rambirambi kwa KANUMBA huku mkijua KANUMBA hata hakuwa mtumishi wa serikali.WAALIMU,MADAKTARI,WANAFUNZI VYUONI,WAKULIMA-MTWARA na WENGINEO wanadai ila serikali haiwathamini wao kwanza inaanza kumthamini marehemu.Serikali yetu inaonyesha KIPAUMBELE chake ni sisi tufe tuwaachie hii nchi wao watanue.WANANCHI amkeni WATUMISHI Zindukeni sasa tukusanye nguvu tuwawajibishe hawa kabla hawajatumaliza.
   
 2. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jiunge kwenye kada ya usanii uonekane kwenye luninga uone kama mambo yako hayatakuwa supa, pole sana wewe piga kazi tu utalipwa na Mungu mbinguni
   
 3. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  50yrs ni usanii mtupu cha kukushauri toa elimu ya uraia kwa jamii inayo kuzunguka ili tuweze kuikomboa hii nchi
   
 4. Kayabwe

  Kayabwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 338
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kaka umenena,nafikiri TUCTA wameisikia basi walimu,madaktari n.k tuungane tuklipwe,na mwaka ujao kima cha chini kiwe 315,000/=
   
 5. f

  fered mbataa JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 240
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hela zipo mpc magamba na matawi yce yote yawe magwanda Mungu ibaric M4C na watu wace
   
 6. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  mimi sishangai sana kaka maana hii ni serikali ya kisanii,kama unakumbuka kwenye mgomo wa madaktari rais alienda kula kuku na hakuna kiongozi hata mmoja aliyehusika kwa uharaka kushughulikia lile tatizo wakati wananchi waliopoteza uhai ni wengi zaidi ya kanumba lakini cha ajabu mzee wa mipasho kusikia msanii mwenzake amefariki aliahirisha safari akaenda kuhani msiba pamoja na wapiga vibuti wenzake (makamu na mzee wa kulia)
   
 7. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Ila jamani Kanumba alitangaza Tanzania nje ya nchi na kusaidia kutuweka ktk ramani kwenye vichwa vya watu. Nani mwingine anafanya alichofanya yeye?
   
 8. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  je unajua ni watu wangapi walioitangaza tanzania waliopoteza maisha?je dunia nzima tunapenda maigizo?waeza kuitangaza sehemu yako kutumi hobby yako, je mwanariadha hatangazi nje?mfanyabiashara je?muongoza watalii je(tour guide) n.k
   
 9. Rabi wa Leo

  Rabi wa Leo Senior Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe 100%..Hoja ya msingi hapa si Kanumba,tunachopaswa kuangalia ni kipaumbele..Mwalimu,Daktari,Polisi,Muuguzi na makundi mengine yanafanya kazi kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri..Nchi inayumba sana wanapofanya migomo hata kama ni kwa muda mfupi tu.Kwanini wasiangaliwe kwa jicho la haki na kupewa wanachostahili?Au tunangoja wafe tukatoe rambirambi?Juzi amefariki Daktari,anayeokoa maisha ya takribani watanzania 12 kila siku,jana kaondoka mwalimu,anayetoa ujinga wa zaidi ya watanzania 200 kila siku..Nani amepeleka rambirambi ya milioni kadhaa?Leo Sajuki.,msanii mahiri yuko India,hoi!!Vipi,tunatuma ujumbe wa serikali kwenda kumsaidia kimatibabu?Au tunasubiri kwenda kutangaza milioni 50 za rambirambi? Taifa linapaswa kuwa Scale of Preference.,lasivyo hatuwezi kwenda mbele..
   
Loading...