Serikali mna mpango gani na vijana?

Serikali mna mpango gani na vijana?

Jimmy George

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
1,733
Reaction score
1,650
Shikamooni wakubwa zangu na wengine habari yenu?

Lengo la uzi huu si kuwafundisha kazi serikali au viongozi wetu najua wana mipango yao. Serikali inataka vijana wafanye nini au wawe wezi? Maana baadhi ya kazi wanazofanya kujipatia kipato wanaingiliwa.

Mfano wapiga debe siyo kwamba nawatetea ni kweli wengine ni wezi lakini kuwakamata na kuwafukuza mnataka wakafanye kazi gani?

Wengine waliokuwa wanaosha magari sehemu za barabarani nao mnawakamata na wamachinga nao tunajua ugomvi wao na migambo na askari. Wengine kusubiri ajira kumekuwa kama mazoea sasa.

Mnapotaka kuwatoa vijana wasifanye kazi fulani jaribuni kuandaa mipango au semina ya nini cha kufanya, kutoa mikopo ya riba nafuu au kubuni miradi mbalimbali ambayo mtawashirikisha vijana ndipo muwatoe au kuwakataza kufanya shughuli husika.

BILA KUWAPA NJIA MBADALA VIJANA WATAENDELEA KUICHUKIA SERIKALI NA KUENDELEA KUTUKANA TU.
 
Nchi hii VIJANA wote ni kama WAMEVAMIA, Wanafukuzwa fukuzwa kama WEZI. Kila wanachofanya WANAKIMBIZWA na KUDUMAA KILA SIKU
- Ajira Hakuna
- Wakipata viwandani, wanakuwa manamba wa 3,000 bila mikataba
- Wakiwa MACHINGA, Wanapigwa na kufukuzwa

- Wakifungua biashara wanakabwa hapo hapo na TRA, TFDA, BRELA, COSOTA, FIRE, NEMC, nk mpaka wahakikishe umefunga KIOSK chako
- Mikopo hakuna BENK Inawaamini, Ya HALMASHAURI ina MASHARTI Kibao mara mnataka kuwa KUNDI Mara sijui nini
- TANZANIA KUWA KIJANA NI "ADHABU" KUBWA SANA, HAKUNA FUTURE. Ni kama TUKO MOTONI
 
Yote ni CCM Mkuu hakika naichukia sana sijaona mazuri yeyote kwao.
 
Nchi hii VIJANA wote ni kama WAMEVAMIA, Wanafukuzwa fukuzwa kama WEZI. Kila wanachofanya WANAKIMBIZWA na KUDUMAA KILA SIKU
- Ajira Hakuna
- Wakipata viwandani, wanakuwa manamba wa 3,000 bila mikataba
- Wakiwa MACHINGA, Wanapigwa na kufukuzwa

- Wakifungua biashara wanakabwa hapo hapo na TRA, TFDA, BRELA, COSOTA, FIRE, NEMC, nk mpaka wahakikishe umefunga KIOSK chako
- Mikopo hakuna BENK Inawaamini, Ya HALMASHAURI ina MASHARTI Kibao mara mnataka kuwa KUNDI Mara sijui nini
- TANZANIA KUWA KIJANA NI "ADHABU" KUBWA SANA, HAKUNA FUTURE. Ni kama TUKO MOTONI
Aiseeeee.!!
 
Back
Top Bottom