B.G TANTAWI
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 496
- 379
Kumekuwa na chapuo la kutaka serikali mbili hasa kwetu sisi wana-ccm huku baadhi ya watu wakitaka serikali moja na wengine tatu. Ikiwa "Serikali Mbili Zilizoboreshwa" zitapita mambo yafuatayo yatatokea, kwanza, Muungano hautavunjika ila utatetereka na migogoro itaendelea tu! je ni kwa vipi Muungano huo utakavyokuwa?
Zanzibar tayari wana bendera, nembo na wimbo wao wa Taifa, hapa ni kama vile Tanzania bara imewafurahisha tu wazanzibar kwa sababu kuwa na vitu hivyo hakuna athari yoyote katika Muungano.
Ikiwa pendekezo letu la Serikali mbili litapita, Watanzania bara na wazanzibar watakuwa wanamchagua Rais wa jamhuri ya Muungano, sasa swali, Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa anashughulika na nini kwa huko zanzibar hadi wazanzibar wahusike kutuchagulia Rais? hapa kutakuwa na mgogoro kutoka Tanganyika.
Je ni Tanzania bara pekee yenye haki ya kutoa Rais wa Jamhuri ya muungano? hapa wazanzibar wanaweza kuanza tena mgogoro.
Katika mikataba ya kimataifa zanzibar itakuwa inadhaminiwa na Tanganyika, je ikiwa itashindwa kulipa deni lolote au ikikwama je nani atakayelipa kama si serikali ya jamhuri ya Muungano ambayo ni Tanganyika?
Pia mkataba wa Montevideo juu ya Haki na wajibu wa Nchi Ibara ya 2 inasema kuwa:
"The federal state shall constitute a sole person in the eyes of international law".
Ibara hii inamaana kuwa, Nchi zilizoungana na kuform serikali mbili au Tatu au zaidi
katika uwakilishi au macho ya kimataifa lazima ijitambulishe kama nchi moja.