Serikali: Marufuku kutumia mifuko ya plastiki kunzia Januari 01, 2017

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SERIKALI imepiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, kuanzia Januari Mosi mwakani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM).

Mwalongo alitaka kujua lini Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira itakaa na wadau wa mazingira kujadili suala la uzalishaji na matumizi ya mifuko hiyo ambayo imekuwa ikiongoza kwa uchafuzi wa mazingira.

January alisema sasa wanaendelea kufanya majadiliano kuhusu suala hilo na kwamba Januari Mosi mwakani itakuwa mwisho wa uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Awali, akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Luhaga Mpina alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wenye viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizowekwa.

“Wadau wote, wazalishaji na viwanda wanatakiwa kuhakikisha wanazalisha mifuko inayoruhusiwa yenye unene usiopungua mikroni 50, tutachukua hatua kwa viwanda vitakavyokiuka ikiwemo kufunga viwanda hivyo,” alisema Mpina.

Alisema elimu itaendelea kutolewa ili kuwakinga wananchi na madhara yanayotokana na matumizi ya mifuko hiyo.
 
Tangu Bunge lidhibiti kurusha matangazo yake LIVE sina hamu hata kusikia kinachoendelea
 
Serikali imepiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, kuanzia Januari Mosi mwakani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM).

Mwalongo alitaka kujua lini Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira itakaa na wadau wa mazingira kujadili suala la uzalishaji na matumizi ya mifuko hiyo ambayo imekuwa ikiongoza kwa uchafuzi wa mazingira.

January alisema sasa wanaendelea kufanya majadiliano kuhusu suala hilo na kwamba Januari Mosi mwakani itakuwa mwisho wa uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Awali, akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Luhaga Mpina alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wenye viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizowekwa.

“Wadau wote, wazalishaji na viwanda wanatakiwa kuhakikisha wanazalisha mifuko inayoruhusiwa yenye unene usiopungua mikroni 50, tutachukua hatua kwa viwanda vitakavyokiuka ikiwemo kufunga viwanda hivyo,” alisema Mpina.

Chanzo:Mtembezi
 
Ila itakera sana bachelors kama Mimi ilikuwa inanipiga TAFU, kuwashia moto wa mkaa, kubebea mahitaji n.k wamenikwaza KWA kweli
 
kumbe muda mwingine haka kajamaa huwa kana akili aisee. This has come too late! ila better late than never, hongera Makamba. Jiji limekuwa chafu Sana, piga faini atakaekiuka hili agizo, weka ndani ikibidi!
 
Hili ni tatizo kubwa, ukitilia maanani athali kubwa inayopatikana kutokana na mifuko ya Plastiki. Hata kabla ya Januari sisi tunaokelwa na kuathilika na hili tunapaswa kuiacha mapema kulinda mazingira yetu. Mwisho wa siku muathilika mkubwa ni sisi na si watengenezaji wa mifuko hiyo, wao wataendelea kupiga pesa.
 
Mbadala wake??!!

Zipo aina nyingi tu za mifuko unaweza tumia kuhifadhi vitu vyako. Mifuko ya karatasi ngumu, mifuko yakufumwa kwa mkono, vitambaa vilivyoshonwa vizuri kuhifadhia vitu/bidhaa nakadhilika. Hapa Arusha yupo rafiki yangu anatengeneza mifuko mizuri kabisa kwa ku-recycle karatasi na mchanganyiko wa kinyesi cha Tembo. The products are of high quality na zinadumu.

Makampuni yanayozalisha Plastic bags yanafanya hivyo for a simple reason, utengenezwaji wake ni RAHISI kwasababu raw materials ni rahisi kupata. Hapa hawajali lolote kuhusu madhara hasi kwa mazingira.

Watanzania tujitahidi kununua/ku-support bidhaa ambazo ni rafiki kwa mazingira. Hata kama ni ghali, jua bidhaa bora hudumu zaidi.
 
Kama nawaona wa hindi wa hapo PPTL Tanga walivyo ipokea kwa simamanzi habari hii but all in all rambo hazitakiwi kabisa sio mjini wala kijijini
 
Mbadala wake??!!
Ukizuia jambo fulani lazima uweke ufumbuzi/mbadala wake,kwani suala ni mifuko inayofaa na si mifuko ya plastic.Hivyo ikikosa kabisa na kusiwe naa mbadala watu watabuni kitu kingine ambacho hatukijui...... Huenda kikawa na athari za kimazingira pia.Ubunifu kwanza
Naamini hilo kama viongozi makini na timu za wataalamu wao wamekwishalizingatia kabla.
HATU NZURI
 
Na pombe za viroba nazo zitakuwa marufuku, vichupa vya juice na soda za plastic je sio uchafu?
 
Back
Top Bottom