Serikali, Makinikia bado yapo Bandarini au yameondolewa kimya kimya?

CHLOVEK

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
542
1,110
Hoja ya Tundi Lissu kuhusu makinikia kuondolewa bandarini kimya kimya inanichanganya/inatuchanganya wale wote tuliokuwa nyuma ya Rais kuhusu sakata hili.

Ili tusivunjike moyo, tunaomba ziara ya kushtukiza ya mkuu wetu bandarini ili kutuonyesha ghilba za Tundu Lissu hazitakiwi kusikilizwa.

Ikishindikana, basi msemaji wa serikali atoe ufafanuzi wa jambo hili kama ilivyo kawaida ili sisi wananchi watiifu tusiyumbishwe na porojo za mgonjwa wetu.

Tupo njia panda, tusaidieni ufafanuzi.
 
Habari za makinikia na trilion mia nne zilikuwa pofesufuri rabishi!
Wakati kontena za samani zinaingia, zile za makinikai ndio zikasabulimeti...
 
Hakuna kitu, na hutasikia wakizungumzia makinikia. Ni aibu.

Kukurupuka sio kuzuri.
 
Hoja ya Tundi Lissu kuhusu makinikia kuondolewa bandarini kimya kimya inanichanganya/inatuchanganya wale wote tuliokuwa nyuma ya Rais kuhusu sakata hili.

Ili tusivunjike moyo, tunaomba ziara ya kushtukiza ya mkuu wetu bandarini ili kutuonyesha ghilba za Tundu Lissu hazitakiwi kusikilizwa.

Ikishindikana, basi msemaji wa serikali atoe ufafanuzi wa jambo hili kama ilivyo kawaida ili sisi wananchi watiifu tusiyumbishwe na porojo za mgonjwa wetu.

Tupo njia panda, tusaidieni ufafanuzi.
Unaambiwa hakuna kiongozi yeyote anayeweza kusema tena neno Makinikia , hilo neno ni kaa la moto !
 
Nimecheka kwa sauti sana. Tulijaribu kuwaambia watu kuwa hizo ni siasa tena zisizokuwa na kichwa wala miguu. Hakuna kitu kama hicho. Kwa sababu wealth tu ya kampuni haifikii hizo $190b, sasa huo ukwepaji wa kodi mpaka kufikia huko umetoka wapi.

Make ukiangalia tu zike tani walizotuambia zimeibwa kwenye report ya Mruma zinafikia ounce troy ya dhahabu 60m. Nimesoma hii Geology na kufanya sana mineral resource assessments huo mgidi wa Bully wenyewe haufikii kabisa hiyo wealth, ambao kwa Tanzania ndo classic deposit.

Tulikuwa tunapozeana muda kabisa.
 
Back
Top Bottom