Serikali: Mafundi wa simu wasajiliwe

Serikali: Mafundi wa simu wasajiliwe

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,426
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kusajili mafundi wanaotoa huduma za matengenezo ya simu za mkononi kwa mujibu wa sheria zilizopo na kuhakikisha huduma wanaozotoa kwa wananchi zina viwango stahiki.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano Dk Jim Yonaz leo Jumatano Disemba 5, alipokuwa akiwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya miezi mitano kwa mafundi simu 68 yaliyotolewa katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia (DIT).

Dk Yonaz amewataka mafundi simu hao kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hayo wakaitumie kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu mkubwa na kuwa mfano kwa mafundi wa aina hiyo hapa nchini.

“Kuanzisha mafunzo haya ya kurasimisha ufundi wa simu za mkononi kutawasaidia mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufahamu lakini pia itaisaidia TCRA kutoa leseni kwa mafundi ambao kiwango chao kinafahamika.

“Yamekuja kwa wakati muafaka na naomba yaendelee kusimamiwa vyema ili mafundi simu za mikononi nchini kote waweze kupata elimu hii, ” amesema Dk Yonaz.

Aidha Dk Yonaz ametoa rai kwa wadau wa Mawasiliano nchini kubuni mipango endelevu ya kushirikiana kuchangia katika kufanikisha mafunzo hayo.
 
Gia hiyo!!! Si muweke wazi tu kuwa mnavizia kuanza kuwatoza kodi mafundi simu....hahahaha.... Mkimaliza hao mhamie kwa mafundi baiskeli aisee.....
 
Kodi TRA na mapato ya leseni kutoa TCRA ndio vinasakwa hapa
 
Kodi kodi
Watu wanataka waendelee kutembelea maVX, prado na migari ya kifahari, full ving'ora

Ili hayo yote wayafanikishe ni lazima wanyonge wakamuliwe kweli kweli
 
Hii nchi kila mtu ni lazima alionje joto la jiwe.
 
Kodi Za Ajabu Ajabu Zinarejea Kwa Kasi Ya Mwendokasi. Leseni Mpaka Kut Repair Viatu Vilivyoisha?
 
Kuflash simu ku unlock ni makosa.ukifanya mchezO unagongwa nyundo kadhaa.

Ila kodi nayo ni muhimu.
 
Faida moja ya fundi simu kujisajili na kuwa na leseni ni pale tatizo linapo tokea ni lazima leseni ukilinde.
Mfano? Mafundi wapo miaka dahari wanapiga hela tu. Matatizo gani ulisikia wamepata na wakashindwa kuyatatua ati sababu hawana leseni?? Kuweni straight kuwa tunahitaji kodi kutoka kwao. Kwani ni kosa kuwadai walipe kodi? Nchi hii si ni yetu sote! Mbona mnazunguka mbuyu?
 
Back
Top Bottom