Serikali kuzifuta taasisi za kidini zinazojihusisha na Katiba, Uchaguzi mkuu

Sikiliza Mkuu, waswahili hawakukosea pale waliposema mfa maji haishi kutapata. Tumeona hivi karibuni Wafanyabiashara na Madreva wakiiwekea ngumu hii Serikali na ikasalimu amri. Nimesoma mahali kwamba Wafanyakazi nao wanataka kuandaa mgomo nchi nzima, pia kuna hili la kutaka kuwanyamazisha viongozi wa taasisi za kidini. Hawa wote wakiwa na sauti moja kuelekea October 2015 basi October Watanzania wengi tutalia machozi ya furaha yaliyochanganyika na huzuni ya kuongozwa kwa miaka chungu nzima na wezi, wala rushwa, mafisadi, majangili, magaidi na wauza unga.
Sina tatizo na dereva, mwalimu au mfanyakazi akitoa pressure serikarini kudai haki zake kwanza ndio siasa zenyewe provided they do it responsibly sio kama mgomo wa madokta kutaka watu wafe kisa kudai haki.

Tatizo kama hao wote na madai yao yachanganywe na dini kama kitu kimoja badala ya kuwa swala la personal interest ambapo watu wadini zote waungane kudai haki zao zakikundi kama walivyofanya. Ukishaingia nyumba za ibada linageukea a religious one hilo alikubaliki dunia yoyote inayolenga kuboresha mshikamno wa jamii.
 
Naona Serikali imechanganyikiwa -Ila wakumbuke Vatican inaukubwa na Wakaazi kiasi gani ndani ya Italy na kwanini iwe na heshima ya kuwa Nchi.

Hatua hiyo ya kufuta taasisi za Kiraia -kama hawajui itawagharimu -Wakubwa zao waliko zoea kuomba omba watachukua hatua kama walivyo fanya kwa issue ya Escrow Account wachae mchezo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa hiyo wewe kwa mtazamo wako kila inachofanya serekali ni sahihi. Ni mara ngapi wananchi wanaporwa ardhi zao na serekali bila fidia stahiki ama hata hiyo fidia wasipate kabisa? Ni mambo mangapi serekali inafanya kwa double standard na bado hakuna hatua stahiki zinachukuliwa?
Sikusema kila inachofanya serikari ni sahihi bali lazima kiwe kisheria, kama wanafanya mambo kiholela na utaratibu ni jukumu la wanasiasa na wananchi sikuhizi wananchi pia wameamka wanaenda kufanya mazuio mahakamani na wakishindwa wanafanya appeals sehemu zingine. Changamoto ni hipo kwa raia zaidi kufahamu haki zao na dhamana waliyonayo serikari. Mfano ni sawa kusema watu wasiingize siasa kwenye dini na kuna sehmu kadhaa kwenye katiba zipo, lakini katiba inasema kuwe na uhuru wa kuamini kwa hivyo kufungia taasisi ni swala ambalo aliwezekani lakini kufungwa kwa kiongozi wa dini linawezekana kabisa kwa kosa la kuhubiri siasa.

Ama unadhani sisi ni wajinga kiasi hatuwezi kutambua kipi kinafanyika kwa usahihi na kipi serekali inafanya kwa hila. Wewe kwa sababu uko serekalini basi umejiweka kwenye kundi la walio juu ya sheria, ni mara ngapi sisi wakulima tunakopwa na serekali na malipo kufanyika kwa kuchelewa ama kutokufanyika kabisa na bado hakuna hatua stahiki zinachukuliwa na hiyo serekali.
Kama unawekewa bunduki wakati unakopwa sawa lakini kama kwa ridhaa zako unaweza kwenda mahakamani kudai haki zako au fidia ya kucheleweshewa hela ni swala la kibiashara kama lililo lingine lolote usichanganye siasa za jumla na interest zako binafsi.

Wewe hapa ulipo ninaona hujajua kabisa tunaongelea nini, sisi hapa tunaongelea hiyo serekali kutumika kuhujumu wananchi, hicho anachotishia huyo Chikawe sio sheria maana kama ingekuwa ni sheria anafuata kuna mengi sana yanakiukwa tena kimachomacho na hajawahi kuchukua hatua.
Kila kitu ni per case uwezi kuweka kila kitu kwenye kapu moja hapa na siasa kwenye majumba ya ibada.

Leo hii anapojifanya kwamba anafuata mambo ya sheria za nchi kama serekali, mbona hivi majuzi hela zimechotwa kimachomacho bila kufuata sheria pale stanbic (escrow) na mpaka leo hakuna aliyetajwa achia mbali kukamatwa.
Binafsi msimamo wangu akukuwa na kesi kwenye sakata la escrow ni kulazimisha mambo tu na kutoleana mifano, kuna swala la morality kuhusu baadhi ya viongozi wetu lakini hakuna kesi ya wizi (hili limejadiliwa sana na halina uhusiano na hoja za siasa na dini).

Hayo macho ya Chikawe na serekali hayakuliona hili? Ama hizo sheria hazifanyi kazi kwenye hilo la wanasiasa? Acha hizo ndugu hapa unajidhalilisha tu na ufafanuzi wako wa kizee.
Acha kuchanganya mambo hoja.
 
Endelea kuamini hivyo waambie wazifute waone gharika lao. Ukandamizaji ukizidi kupita kiasi wananchi hufikia wakati wakasema sasa basi liwalo na liwe. Hakuna nguvu ya jeshi itakayoshinda nguvu ya umma.

Sina tatizo na dereva, mwalimu au mfanyakazi akitoa pressure serikarini kudai haki zake kwanza ndio siasa zenyewe provided they do it responsibly sio kama mgomo wa madokta kutaka watu wafe kisa kudai haki.

Tatizo kama hao wote na madai yao yachanganywe na dini kama kitu kimoja badala ya kuwa swala la personal interest ambapo watu wadini zote waungane kudai haki zao zakikundi kama walivyofanya. Ukishaingia nyumba za ibada linageukea a religious one hilo alikubaliki dunia yoyote inayolenga kuboresha mshikamno wa jamii.
 
Endelea kuamini hivyo waambie wazifute waone gharika leo. Ukandamizaji ukizidi kupita kiasi wananchi hufikia wakati wakasema sasa basi liwalo na liwe. Hakuna nguvu ya jeshi itakayoshinda nguvu ya umma.
Siungi mkono hoja ya kufungiwa kwa taasisi nzima bali naunga mkono hoja ya wahubiri wa siasa ndani ya taasisi za dini kuchukuliwa hatua.
 
Na wakati huo huo mafisadi, wezi, wapokea rushwa hadi ndani ya Ikulu na Bunge wakiendelea kupeta mtaani!!! Only in Tanzania

Siungi mkono hoja ya kufungiwa kwa taasisi nzima bali naunga mkono hoja ya wahubiri wa siasa ndani ya taasisi za dini kuchukuliwa hatua.
 
Na wakati huo huo mafisadi, wezi, wapokea rushwa hadi ndani ya Ikulu na Bunge wakiendelea kupeta mtaani!!! Only in Tanzania
we unaonekana mkorofi hapa tunaongelea dini na siasa hayo ya mafisadi yanatikiwa thread yake.

Me out.
 
Serikali imejitia za mtonga sasa Maji ya dafu itaoshea donda !!tunakokwenda karibu tulipo toka na katiba pendekezwa na watu pendwa itatufanya tuamini bora al shaabab
 
Mkorofi kwa kukwambia wakati Serikali inataka kuwanyamazisha viongozi wa dini lakini wakati huo huo inaangalia pembeni na kupindisha sheria kwenye swala la wezi, mafisadi na wapokea rushwa ambao wapo mpaka ndani ya Ikulu na hivyo kuwaachia wapete mtaani!?

we unaonekana mkorofi hapa tunaongelea dini na siasa hayo ya mafisadi yanatikiwa thread yake.

Me out.
 
Hata hivyo, viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu waliozungumza na gazeti hili jana kuhusu kauli hiyo, wamesema taasisi zao zinawakilisha watu, na hivyo zina haki ya kikatiba na kisheria kupinga jambo lolote zitakaloona linakwenda kinyume na maslahi ya Taifa na kwamba ziko tayari kukaguliwa.

Serikali kuzifuta taasisi za kidini zinazojihusisha na Katiba,Uchaguzi mkuu - Kitaifa - mwananchi.co.tz

we unaonekana mkorofi hapa tunaongelea dini na siasa hayo ya mafisadi yanatikiwa thread yake.

Me out.
 
Mbona kwenye bunge la katiba walikuwepo hao viongovi wa dini. Kwanini sasa wakataliwe kutoa msimamo wao katika katiba pendekezwa. Mbona mnajichanganya hivi. Kwani katiba ni ya serikali tuu??? Mbona tbc na serikali wanasema tuipigie kura ya ndio kwahiyo wao ni malaika??? Sasa kama mlitaka jibu liwe ndio kwanini iwepo kura ya maoni????


Nawashangaa sana hawa CCM, tatizo hawaelewi hata maana ya siasa. Ni mfumo wa maisha ambao jamii/nchi imeamua kuufuata kufanya maamuzi na kuweka uongozi. Kama wanaona demokrasia inatoa uhuru mpana kwa makundi mbalimbali kujitambua nafasi zao katika kuokoa jahazi la taifa hili basi waachie madaraka kwa watu wanaoweza kazi.

Utashangaa katika mchakato wa Mahakama ya Kadhi wamesikiliza maoni ya pande za dini na hatimaye kuamua KUUONDOA MUSWADA BUNGENI. Hapo hawakuona kuwa viongozi wa dini wameingilia SIASA

Suala la KATIBA na UCHAGUZI MKUU ndio pekee vinawatia HOFU.

mimi kanisa langu likifungwa maana yake yale waliyoyasema wangozi wa dini ni sahihi kwa asilimia 100%, hivyo nitajiandikisha na KUIKATAA KATIBA YA CHENGE na hatimaye kumuondoa HERODE kupitia sanduku la KURA
 
Yaani una mawazo ya kizee ile mbaya. Kwanza kumbuka hivi vyama vya siasa vyenyewe vinatugawa kutokana na itakadi zao na utanzania wetu uko palepale. Sasa sijui unashangaa nini kama hata hizo dini zikitugawa na bado tukabaki na utanzania wetu. Tatizo ninaloliona ni kwamba nyinyi wanasiasa ndio mmejipa hati miliki ya hii nchi. Yaani mnaona kwamba eti nyinyi ndio wenye uwezo wa kuamua kila mlitakalo bila kujali mamlaka yanatokana na utashi wa umma na huo umma haujali dini. Ama mtu akiwa muumini hapaswi kuikosoa serekali? Nyinyi wanasiasa mkumbuke mpewa nchi kama dhamana na sio kama mali yenu, na sio kwamba kila mnachotaka nyinyi ni lazima umma mzima uwakubalie. Tukiona mnafanya mambo mnavyotaka tuna haki ya kuwakataza ama kukataa upuuzi wenu bila kujali tunatoka kwenye kundi la viongozi wa dini, wakulima, wafugaji nk. Hii tabia yenu ya kujifanya eti nyinyi wanasiasa ndio sauti ya mwisho dhidi ya umma sasa ndio itafikia mwisho kwani tumechoka.

Ukijaribu kuangalia mikataba mingi mibovu mmeingia nyinyi wanasiasa, mambo mengi ya hovyo na sheria zinatekelezwa kwa makundi mengine ila zikifika kwa wanasiasa zinagonga mwamba. Leo hii wanasiasa mnajipangia malipo makubwa kutoka kwenye pato la taifa na hakuna kundi lolote linaweza kuwauliza, kisa eti nyinyi mnajifanya ndio wenye haki. Iweje mbunge ama waziri kupata mshahara mnono kulinganisha na kada nyingine kama madaktari, maprofesa, wakulima, wafanya biashara nk. Nani aliyewapa hayo mamlaka ya kujipendelea kutoka pato la taifa? Kama pato ni dogo iweje nyinyi muwe na pato mara 50 zaidi toka pato la mwananchi mwingine wa kawaida? Mnadhani makundi mengine ya jamiii tutaendelea kukaa kimya kwa dhamana tulizowapa wenyewe huku mkiendelea kufanya mtakavyo kwa kisingizio cha kulinda amani fake? Hivi majuzi hela zimechotwa toka stanbic kwenye sakata la escrow, mbona hatuoni hatua stahiki ama mnadhani huo wizi hauwezi kuvuruga amani ya nchi? Wanasiasa mmekuwa mkijipendelea huku mkidanganya umma eti maamuzi yanafanywa na nyinyi, sheria zimetungwa kwa wote mbona kwenye wanasiasa/watawala zinakuwa butu? Halafu mnakuja na vitisho vya kufunga taasisi nyingine, unadhani sisi umma hatuna uwezo wa kufunga hiyo taasisi yenu ya siasa ambayo mnajitwalia sheria mpendavyo?

Mkuu umeongelea mambo mengi ya muhimu sana ambayo yote umeyaweka kwenye maswali kwa hao wanasiasa, ningetemani wajipe majibu ya kila swali ulilouliza labda watabahatika kujua wajibu wao na nafasi yao nini kwenye nchi.

Kwa kuongezea tu; Amani ni rahisi kabisa kutoweka kwa kujaribu hizi njia anazopendekeza waziri wetu. Kujaribu kuziba midomo taasisi kwa kuzifuta ukitumia mianya ya kisheria iliyopo ni kosa kubwa. Huu ndiyo mwanzo wa kuzalisha itikadi kali za kidini, kajifunzeni katika nchi za kiarabu ambazo ziliamua kupiga marufuku makundi ya Muslim Brotherwood na matokeo yake kuzalisha itikadi kali sana za kidini.

Je tunakataa waziri kusimamia sheria za nchi? La asha; tunapinga matumizi ya sheria za nchi kusimamia masilahi ya vikundi ama vyama vya siasa. Waziri Chikawe chonde chonde, kuwa makini na usimamizi wako wa sheria juu ya hizo dini na usije kuwapa sababu ya kutuavurugia amani kwa kisingizio cha kunyimwa uhuru wa kuabudu.
 
sasa mtakubaliana na sisi kina gogo la shamba tunaposema kwamba,ccm imekataliwa hata na Mungu, inawaudhi wakristo na hata waislamu mpaka wale masheikh ubwabwa wameshtuka
 
Siungi mkono hoja ya kufungiwa kwa taasisi nzima bali naunga mkono hoja ya wahubiri wa siasa ndani ya taasisi za dini kuchukuliwa hatua.

Kiongozi wa dini anapotoa mahubiri yake kuwapongeza wanasiasa mara zote WANASIASA huwa wanashangilia sana tu na kuwapongeza viongozi hawa,je kupongeza wanasiasa siyo SIASA?Na iweje KUONYA tu ndiyo iwe issue?

Kwa hakika kazi ya viongozi wa dini ni KUONYA,KUASA,KUELEKEZA na KUPONGEZA hawa viongozi wetu,sababu na wao pia ni waumini wa taasisi hizo,hivyo wanahaki ya kuwaasa WATAWALA sababu ni waumini wao!

Hivyo SIASA na DINI ni vitu viwili vinavyotegemeana,kukiwa na tatizo haohao wanakimbia mbio kwenda kwa viongozi wa dini kuwaomba wasaidie kutatua migogoro na kuliombea TAIFA,hivi kuliombea TAIFA siyo SIASA?

Ifike mahali watawala wajue watanzania wote tunahaki juu ya nchi yetu ,na TANZANIA ni yetu sote,hata viongozi wa dini wanahaki ya kuongea kuhusu TAIFA lao.

Ningewaomba viongozi wetu wa dini waendelee kuwakosa hao watawala,tuone kama watakuwa na UBAVU wa kulifungia Kanisa au misikiti.
 
Sina tatizo na dereva, mwalimu au mfanyakazi akitoa pressure serikarini kudai haki zake kwanza ndio siasa zenyewe provided they do it responsibly sio kama mgomo wa madokta kutaka watu wafe kisa kudai haki.

Tatizo kama hao wote na madai yao yachanganywe na dini kama kitu kimoja badala ya kuwa swala la personal interest ambapo watu wadini zote waungane kudai haki zao zakikundi kama walivyofanya. Ukishaingia nyumba za ibada linageukea a religious one hilo alikubaliki dunia yoyote inayolenga kuboresha mshikamno wa jamii.

Hata hao viongozi wa dini ni WATANZANIA ,na kwenye majumba ya IBADA nidyo maeneo yao ya KUONYA na KUPONGEZA.

Hakuna sababu ya kuwafunga mdomo,viongozi wetu wameshalewa madaraka kiasi kwamba wanadhani wao tu ndiyo wanahaki ya kusema WATANZANIA waipigie kura ya NDIYO hiyo Katiba ya Chege na wengine hawaruhusiwi kupiga kampeni ya HAPANA,haiingii akilini kwangu.Kwanini wasipige marufuku wote wa NDIYO na HAPANA?

Ukitaka AMANI iwepo hakikisha tunda la HAKI lipo.Kwa Katiba ya Chenge ni MARUFUKU kusema HAPANA lakini ni sahihi kusema ndiyo.

Mwanasheria huyu amepotoka arudi tena ajiulize.....................
 
Chikawe anafurahisha genge tu,yeye anadhani anaweza kumkamata Pengo,Mwalasusa au mufti Simba?Hao si Gwajima,asicheze na kabisa katoliki, KKKT au Bakwata.

Kucheza na mtu unayemtegemea kwenye mashule, mahospitali na mambo mengine ya kijamii unajihatarishia uhai wako... Embu fikiri ulifute kanisa na RC...!
 
Back
Top Bottom