Serikali kuwafunda Manabii wanaodai kufufua Maiti

Tutanota

Member
Aug 5, 2020
18
77
Ni hatari kwa taifa Mtu wa Imani ya dini nyingine kulitumia bunge kuwananga viongozi wa dini nyingine

Mtu wa Imani ya dini nyingine kujinasibu kuwafunda viongozi wa dini nyingine ni tangazo la vita vya kidini, likemewe haraka sana kabla mambo hayajachafuka

Haya mambo tuliyasahau, Nani anayaleta? Anayaleta kwa maslai gani

Dini nyingine haitakubali


=====

Swali "Je serikali haioni sasa wakati umefika wa wale manabii ambao wanadai wanao uwezo wa kuwafufua waliokufa ili kukaa nao kwa karibu ili kuweza kuwafufua wapendwa wetu"- Khalifa Mohamed Issa

Jibu "Anaweza akatokea mtu akasema anaweza kufufua, akachukua pesa za watu na mtu akazikwa mwisho wa siku ni migogoro, tuko tayari kukaa nao hao manabii ili tuwaeleweshe kwamba mwenye uwezo wa kuondosha na kurejesha ni Mungu pekee"- Hamza Chilo, Naibu Waziri, @wizaramnn
 
Wewe ndio mdini.

Ulevi wenu wa "kidini" utaisha lini.

Acheni ARGUMENT AD HOMINEM kisa tu mtoa hoja "HAFANANI NAWE".

Hivi shule mlikwenda na mkafundishwa MIDAHALO NA KANUNI ZAKE?

BUNGE NI TAASISI HURU na wananchi si mahakimu wa kila kisemwacho bungeni.

Ndio maana BUNGE lilizuiwa kurushwa LIVE kwa sababu ya watu aina yenu.

Mnapenda kuwalisha maneno watu wengine na kutaka wanene mnenavyo khaaaaa.

Kweli waafrika wengi tuwajinga tunaopenda "kudemkia" mambo KOKO YA "UDINI".

Siempre Tanzania!
 
Hakuna udini kwenye Swali ama jibu la Waziri, hakuna mwanadamu anaweza kufufua wafu, aliyefanya hivi ni Kristo mwenyewe wakati anaishi duniani kama binadamu wa kawaida !! hawa wanaojiita manabii wanaosema wana uwezo wa kufufua wafu ni wa kuangalia kwa makini mno yaweza kuwa ni wapigaji.

Hata kuna muda wanafunzi wa Yesu walishindwa kufufua wafu na hata walishindwa kutoa mapepo - hadi wanamuuliza Yesu kwa nini wewe waweza na sisi twashindwa?

Soma Marko 9:14-37 itakusaidia sana kuelewa mambo haya kwa undani.

 
Hakuna udini kwenye Swali ama jibu la Waziri, hakuna mwanadamu anaweza kufufua wafu, aliyefanya hivi ni Kristo mwenyewe wakati anaishi duniani kama binadamu wa kawaida !! hawa wanaojiita manabii wanaosema wana uwezo wa kufufua wafu ni wa kuangalia kwa makini mno yaweza kuwa ni wapigaji...
Sio Yesu pekee aliyefufua haya Elia alifufua pia
 
Mm nawasiliana na mwanasheria wangu nataka kuwashitaki manabii wanaotusema kila siku sisi washirikima mbo a sisi hatuwasemi wanatuharibia madel yetu mshana jr atakuwa shahidi namba moja katika shauri hili nimeathirika sana kiuchumi.... au wajameni niende tume ya usuluhisi na upatanisho ili waonywe... sisi hatujawahi kuwasema popote maana utaratibu wetu ni one on one session wao wana platform....
 
Kazi ipo, kazi iendelee..

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Back
Top Bottom